Natafuta bata aina ya Pekin

noel2512

Member
Feb 26, 2015
80
14
Habari za leo wadau wa JF,

Poleni sana na uchovu wa wikiendi. Natafuta mtu ambaye anaweza kunisaidia kupata bata wa aina ya pekin na nina maanisha pure white pekin duck. Nahitaji wasiopungua 50 kwa ajili ya kuanza kuwafuga kwa hiyo wale ambao ni wadogo kidogo kama miezi miwili ndio watakuwa wazuri zaidi. Kama kuna mdau anao au ama anafahamu tafadhali naomba mnijulishe kwa pm au hata hapa hapa kwenye huu uzi.. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu wanaJF.

MwanaJF..
 
Nipo Dar ila popote walipo wanaweza kufuatwa mkuu haina shaka kabisa.
Kuna jamaa ni rafiki yangu nilisoma nae anawafuga wengi sana hapo kilimanjaro mwanga niliwasiliana kama anawauza akasema yeye anayo order kutoka Kenya tu..Usikate tamaa endelea kutafuta
 
embu tuwekee picha maana mi najua bukini na baTA maji tu walai
 
kuna jamaa yangu mmoja anao anapatikana kimara Temboni.. ukiwa interested niPm nikupe no yake..
 
embu tuwekee picha maana mi najua bukini na baTA maji tu walai

Ricky-and-Lucy-sm.jpg


pekin-duck.jpg
 
Back
Top Bottom