Natabiri kuna siku Bernard Membe atarudi CCM

Machi 1995 mwaka wa uchaguzi, Augustine Mrema aliondoka CCM akasema atagombea urais upinzani.

Julai 2015 miezi michache kabla ya uchaguzi Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu aliondoka CCM akatangaza atagombea urais upande wa upinzani.

Julai 2020 mwaka wa uchaguzi, Membe Waziri Mambo ya Nje Mstaafu kaondoka CCM, kasema atajiunga upinzani na atagombea urais. Mwaka 2025 (nani?) ataondoka CCM ataomba kugombea upinzani, naye atarudi CCM?

Agosti 2015, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, alijiondoa CCM baadae akaomba kugombea Uenyekiti wa CHADEMA akakosa akarudi CCM.

Tofauti na hao kuna ambao walijiondoa CCM lkn wakabaki na misimamo yao, Kambona (RIP), Kingunge (RIP), Babu (RIP), Mtei, Maalimu Seifu nk.

Membe, hata kama italazimika upinzani kumpokea, ni sawa, lkn wawe makini sana wanapofanya naye siasa, kumbuka Membe ni jasusi mbobevu kama alivyo Mrema huwa hawasitaafu, akikosa anachokitafuta atarudi CCM kama kina Mrema, Lowassa, Sumaye na wengine wengi waliokuwa watumishi wa serikali.

Huu ni utabiri wangu tu, zingatia staili aliyoondoka nayo ya kuishukuru CCM ni kama anaweka mazingira mazuri pindi atakapoomba kurudi.

Wakati ni mwalimu mzuri sana.

Quinine.
===========≠
View attachment 1501866
Kwa katiba hii na sheria za nchi yetu huwezì toka CCM then ukafanya siasa never. Labda utoke CCM uamie kustaafu.
 
Hii hata mtoto angetabiri tulijua atarudi ccm baada ya magufuli kuondoka au kumaliza madaraka
 
Back
Top Bottom