Natabiri kuna siku Bernard Membe atarudi CCM

Kwani usalama wa taifa au usalama wa CCM kwahiyo akirudi CCM ndo amerudi usalama wa taifa mbona tuna mawazo mafupi sana kuona taifa ni sawa na CCM we unajua watu wangapi wanafanya kazi usalama wa taifa na wapo wapi? tuache hizi fikra kuwa usalama wa taifa ni CCM, Polisi CCM, jeshi ni CCM hivyo ni vyombo vya taifa sio vya CCM kuna viongozi wa hivyo vyombo wanakosa ueledi ndo maana unaona kama ni vyombo vya CCM ila sisi kama raia hatupaswi kutengeneza hii kasumba ya kuwamilikisha CCM inchi yetu na vyombo vyake, Membe apingwe kwa mengine sio eti kwasababu alikuwa afisa mwandamizi usalama wa taifa kazi aliyofanya kama raia mwengine yoyote kwani Marando karudi CCM.

Hakuna tofauti ya ccm na vyombo vya dola.
 
IMG_20200709_123418.jpg
 
Hakuna mtu anayekataa upinzani kusajili wanaccm hasa wenye ushawishi kama Membe, lkn tunatoa tahadhari tu kuwa wawe makini kwa sababu kuna matukio kama yake yameshatokea huko nyuma kwa wana CCM kujiunga na upinzani dkk za lalasalama kisha wakikosa wanachotafuta hurudi walikotoka.
Huyu Nasari je wa Chadema kuhamia CCM ,huwapi tahadhari CCM kwa wimbi la wapinzani kuhamia hamia na kuwacha wakisota ndani ya chama walioasisi na kukifia?
 
Hili si swala la utabiri, ni ukweli ulio wazi. Huwa wanatumwa kwenda kutibua upinzani, hupata nafasi ya kupima nguvu ya upinzani. Matokeo huwa ni mabaya kwa CCM na dola huingilia kuokoa jahazi. Mrema 1995 alikuwa achukue nchi, Dar uchaguzi ukafutwa. Dr Slaa yaliyotokea 2005 hayajasahaulika, kanisa liliingilia kati na kumwambia akubali yaishe nchi isiangamie. Mh Lowasa 2015 nae alitumwa, CCM ikiwa mguu upande, nchi kutahamaki inachukuliwa na Lowasa, wakaokolewa na Sheria ya mitandao, kituo cha kuratibu kura za bw Lowasa kikatekwa. Mwaka huu katumwa bwana Membe, ni muda utaamua.
 
Chanzo cha yeye kuhama ni nini? Kama ni mwenyekiti basi muda wa mwenyekiti huyu ukipita atarudi tu.
Ingekua chanzo ni system nzima ya CCM labda asingeweza kurudi.
Nawaza tu.
 
Machi 1995 mwaka wa uchaguzi, Augustine Mrema aliondoka CCM akasema atagombea urais upinzani.

Julai 2015 miezi michache kabla ya uchaguzi Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu aliondoka CCM akatangaza atagombea urais upande wa upinzani.

Julai 2020 mwaka wa uchaguzi, Membe Waziri Mambo ya Nje Mstaafu kaondoka CCM, kasema atajiunga upinzani na atagombea urais. Mwaka 2025 (nani?) ataondoka CCM ataomba kugombea upinzani, naye atarudi CCM?

Agosti 2015, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, alijiondoa CCM baadae akaomba kugombea Uenyekiti wa CHADEMA akakosa akarudi CCM.

Tofauti na hao kuna ambao walijiondoa CCM lkn wakabaki na misimamo yao, Kambona (RIP), Kingunge (RIP), Babu (RIP), Mtei, Maalimu Seifu nk.

Membe, hata kama italazimika upinzani kumpokea, ni sawa, lkn wawe makini sana wanapofanya naye siasa, kumbuka Membe ni jasusi mbobevu kama alivyo Mrema huwa hawasitaafu, akikosa anachokitafuta atarudi CCM kama kina Mrema, Lowassa, Sumaye na wengine wengi waliokuwa watumishi wa serikali.

Huu ni utabiri wangu tu, zingatia staili aliyoondoka nayo ya kuishukuru CCM ni kama anaweka mazingira mazuri pindi atakapoomba kurudi.

Wakati ni mwalimu mzuri sana.

Quinine.
===========≠
View attachment 1501866
Maisha yakiwa magumu tu atasema: "Ninarudi nyumbani".
 
Kwa mapenzi ya nchi Membe agembea Ubunge Mtama na asaidie kupata viti vingine kusini. Kina Kibajaji,Msukuma, Ally Kessy na wengine wakirudisha ile story tena kuwe na vigogo wa kupambana nao.

Mpambano wa Uraisi ukawa 2025.

Kwa kugombea Urais kwa sasa ni waste of Resources, Sijui kama Mkuu atakubali kutupa taulo hivi hivi.

Lissu is Perfect kwa sasa ili kuinua mood. Imagine Kwenye jukwaa moja anakuwa Lissu,Membe,Zitto, Mnyika,Mbowe, Maalim Seif na Wengine.

Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Machi 1995 mwaka wa uchaguzi, Augustine Mrema aliondoka CCM akasema atagombea urais upinzani.

Julai 2015 miezi michache kabla ya uchaguzi Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu aliondoka CCM akatangaza atagombea urais upande wa upinzani.

Julai 2020 mwaka wa uchaguzi, Membe Waziri Mambo ya Nje Mstaafu kaondoka CCM, kasema atajiunga upinzani na atagombea urais. Mwaka 2025 (nani?) ataondoka CCM ataomba kugombea upinzani, naye atarudi CCM?

Agosti 2015, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, alijiondoa CCM baadae akaomba kugombea Uenyekiti wa CHADEMA akakosa akarudi CCM.

Tofauti na hao kuna ambao walijiondoa CCM lkn wakabaki na misimamo yao, Kambona (RIP), Kingunge (RIP), Babu (RIP), Mtei, Maalimu Seifu nk.

Membe, hata kama italazimika upinzani kumpokea, ni sawa, lkn wawe makini sana wanapofanya naye siasa, kumbuka Membe ni jasusi mbobevu kama alivyo Mrema huwa hawasitaafu, akikosa anachokitafuta atarudi CCM kama kina Mrema, Lowassa, Sumaye na wengine wengi waliokuwa watumishi wa serikali.

Huu ni utabiri wangu tu, zingatia staili aliyoondoka nayo ya kuishukuru CCM ni kama anaweka mazingira mazuri pindi atakapoomba kurudi.

Wakati ni mwalimu mzuri sana.

Quinine.
===========≠
View attachment 1501866
Akimaliza kazi yake CDM hata akirudi sawa tu wengi huenda wengi hurudi na kwenda tena.
 
1. Mtu hachelewi kwake.
2. Nyumbani ni nyumbani
3. Maji hayasahu ubaridi
4. Mtaraka hatongozwi

Kati ya hizo ipi inakaa poa?
Kuna hizi pia:-
1.Ng'ombe akivunjika Mguu hurejea bandani.
2.Mwenda kwao si mtoro.
3.Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
4.Titi la Mama litamu.
5.Cha kuazima hakisitiri maungo.
 
Machi 1995 mwaka wa uchaguzi, Augustine Mrema aliondoka CCM akasema atagombea urais upinzani.

Julai 2015 miezi michache kabla ya uchaguzi Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu aliondoka CCM akatangaza atagombea urais upande wa upinzani.

Julai 2020 mwaka wa uchaguzi, Membe Waziri Mambo ya Nje Mstaafu kaondoka CCM, kasema atajiunga upinzani na atagombea urais. Mwaka 2025 (nani?) ataondoka CCM ataomba kugombea upinzani, naye atarudi CCM?

Agosti 2015, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, alijiondoa CCM baadae akaomba kugombea Uenyekiti wa CHADEMA akakosa akarudi CCM.

Tofauti na hao kuna ambao walijiondoa CCM lkn wakabaki na misimamo yao, Kambona (RIP), Kingunge (RIP), Babu (RIP), Mtei, Maalimu Seifu nk.

Membe, hata kama italazimika upinzani kumpokea, ni sawa, lkn wawe makini sana wanapofanya naye siasa, kumbuka Membe ni jasusi mbobevu kama alivyo Mrema huwa hawasitaafu, akikosa anachokitafuta atarudi CCM kama kina Mrema, Lowassa, Sumaye na wengine wengi waliokuwa watumishi wa serikali.

Huu ni utabiri wangu tu, zingatia staili aliyoondoka nayo ya kuishukuru CCM ni kama anaweka mazingira mazuri pindi atakapoomba kurudi.

Wakati ni mwalimu mzuri sana.

Quinine.
===========≠
View attachment 1501866
hili wala hata si la kutabiri. it's a starkly naked eventuality.

Membe ameondoka CCM baada ya kufurushwa na kuukosa urais.

October hii akiukosa urais kupitia opposition atakuwa hana incentive ya kuendelea kukaa huko "ugenini" kwenye madhira lukuki. atataka amalizie ubabu wake kwa kheri si shari - kama Lowasa & Sumaye walivofanya.

upinzani uachane na kupoteza muda wa kushirki uchaguzi ambao si Chadema wala ACT ambao japo wabunge wao watachaguliwa kwa kura nyingi za wananchi lakini DEDs hawatawatangaza na hakuna wa kusema fyoko. watakaojifanya sijui kubaki kulinda kura vituoni wataishia kuvunjwa vunjwa limbs zao tu kama panzi au hata "kufanywa asusa".

ni chungu kumeza but ndiyo ukweli wenyewe. sijui kwa nini wapinzani hawaoni matukio ya ule uchaguzi wa marudio Kinondoni yakijirudia (RIP Aquiline).
 
Back
Top Bottom