Nimekutana na kijana asub leo wakati natoka mazoezini akaniuliza;
"Kaka Nape mambo vipi? Mie mshabiki kufa wa Chadema lakini sijapata mtu wa kunijibu kwanini Chadema kila wakipanga maandamano wanapanga, Dar,Mwanza, Arusha na nimesikia wanakwenda Mbeya tar. 10. Kwanini hawapangi maandamano anakotoka muasisi wa Chadema Mzee Mtei?!!!"
Nikainama chini nikamuuliza uchaguzi ndani ya chama chenu lini?! Akastuka kidogo, akanambia hivi unatakiwa kuwa mwaka huu kweli!?!! "Mhhh hilo nalo swali! Lakini hivi tukifanya uchaguzi Chama chetu kitapona kweli?! Nadhani bora tusifanya uchaguzi mpaka tutakapokamata dola"! Alisisitiza kijana.
Nikamjibu "BWANA YESU KRISTO ASIFIWE"!
Mkuu Nape, endelea kuyasubiria!.
Moshi ndio Ngome Kuu ya Chadema!, CCM hata mkikesha usiku na mchana kwa siku 360!, hamuitikisi, hivyo kwa maoni yangu, Moshi haihitaji kabisa maandamano ya Chadema!.
Hilo la uchaguzi wa ndani nalo neno!.
Kwa uzi huu, Mkuu Nape, kweli nimeamini, kuna watu wa CCM, hamlali kwa kuiwaza Chadema!, yaani Chadema inawakosesha kabisa usingizi, hadi mkikosa chochote cha kuandika, basi unaandika chochote tuu kuhusu Chadema ali muradi umeandika!.
Japo najua CCM mtashinda uchaguzi mkuu wa 2015! kwa mbinu zile zile, nilidhani huu sasa ni wakati wa kuendesha siasa za ukweli zaidi na sio ghilba kama kawaida!, CCM itaendelea kuchaguliwa kwa mazoea na sio kwa track record!, kama wewe ndio mmoja wa vinara, unakuja na uzi kama huu!, na hii mentality yako ndio mentality ya CCM as a whole!, please don't under estimates us that much!, ni vizuri, mkae mkijua, Watanzania wa leo, sio wajinga kama mnavyowadhania, hata kama CCM imekuwa madarakani kwa miaka 50 iliyopita na inataraji kuendelea kuwepo madarakani kwa miaka 50 mingine ijayo!, japo CCM has been fooling some people for sometimes, but you can't fool all the people, all the time!.
Pasco.