Nassari kortini kwa kuchoma bendera ya CCM

Nassari kortini kwa kuchoma bendera ya CCM

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,324
Reaction score
2,494
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) jana alifikishwa Mahakama ya Mwanzo Maji ya Chai na kusomewa shtaka la uharibifu wa mali na kuchoma bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yenye thamani ya Sh laki mbili na elfu tano.

Mbunge huyo alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu, David Mwita.

Ilidaiwa na upande wa mashitaka kuwa juzi saa 11:00 jioni Mbunge huyo alichoma bendera za CCM kwa makusudi zenye thamani ya Sh 205,000 huku akijua kuchoma bendera hiyo ni ukiukwaji wa kanuni na sheria za nchi.

Hata hivyo, Nassari alikana kuchoma bendera hiyo na kupewa dhamana, ambapo wadhamini watatu walijitokeza na kusaini bondi ya Sh milioni 1.5.

Mbunge huyo anatetewa na mawakili watatu, ambao ni James Millya, Charles Adiel na Marceline Bandiye. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 24, mwaka huu.

Chanzo:
Gazeti la Habari Leo

 
Uchaguzi umekaribia vituko vinaanza mradi kura zipatikane
 
Hakuna kitu hapo ina maana hawa mahakimu hawana kesi nyigine zenye tija za kufuatilia?
 
Hasira za dogo
wakati mwingine huwa namshangaa
  • alitaka Vijana waende Ikulu kwa miguu kutoka Arumeru hadi Magogoni
  • alitaka Nchi ya kaskazini tu ijitawale tena yenye mikoa mitatu tu
Su ajabu machalii wamempandisha munkari naye akachoma kweli
 
Sina tatizo na utekekezaji wa sheria kama kweli Nassari amefanya kosa. Ila ukitaka kuamini wazungu kutudharau ni haki yao ni hapa. Juzi kumetokea sakata la escrow, imesemekana wengine walibeba hela mpaka kwenye mifuko ya rambo lakini hatusikii mtu kapelekwa mahakamini. Sasa unajiuliza kama ni kesi ya kukimbiza mahakamani ilikuwa ni ipi kwa maslahi ya taifa, bendera ya ccm ama fedha ambazo zingejenga shule, kununua dawa, kujenga miundo mbinu? Hapo ndio unaangalia upeo wetu waafrika ulipofikia, sio wasomi au ambao hawakusoma wote ni wapuuzi tu. Kwa mawazo na tabia za namna hii unategemea kupata wazo la watu hata kujenga viwanda ili kutoa ajira? Ama utaishia kuona viongozi na wasomi kwenda kwenye ushirikina ili wabaki kwenye madaraka yao. Hapo utaona wabunge na viongozi wa ccm wanasimama bungeni wanasema wapinzani hawataki maendeleo kisa kachoma bendera wakati pesa zilizoibwa na zinazoweza kuleta maendeleo watasema sio za wananchi!!!
 
Kwenye photo library yangu nimekosa ile picha Mh. Rage akimpiga kijana wa cdm
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    36 KB · Views: 1,050
Huyu mpuuzi ndio maana walimtafuna kampeni za Makuyuni.
 
kila siku nawaambia ccm huu sio wakati wa hila, unaacha kuwafikisha mahakamani watu walioiba mamilioni ya fedha unampeleke mtu aliyechoma bendera tene kwa ulinzi mkali
 
Yale Yale ningeleta hii thread Mimi bavicha wengi wangenitukana sana.

Lakini wataona jinsi mbunge wao alivyopwaya kwenye ubunge. Ni mzigo kwake inabidi mwakani wanameru wampunzishe , siasa za kuchoma bendera ni za chuki na machafuko kuleta.
 
Kuchoma bendera ni kosa kwa mujibu wa sharia gani?
 
Huyu mpuuzi ndio maana walimtafuna kampeni za Makuyuni.

Bendera za ccm zimeeka na kuchoka kama chama chao mpaka nyingine hazijulikani hata rangi yake ambapo inapelekea kuona kama ni uchafu unaostahili kuondolewa machoni pa watu na kuchomwa.
 
waliochoma bendera ni wengine na aliyeshtakiwa ni mwingine..Watanzania fikirieni kwa makini siasa ni MCHEZO MCHAFU
 
waliochoma bendera ni wengine na aliyeshtakiwa ni mwingine..Watanzania fikirieni kwa makini siasa ni MCHEZO MCHAFU
Kuchoma bendera ni kosa kwa mujibu wa sharia gani? On a serious note, nataka nifahamu.
 
Back
Top Bottom