PreGE2025 Nasra: Dar es salaam sio lango la wanaharakati uchwara

PreGE2025 Nasra: Dar es salaam sio lango la wanaharakati uchwara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,923
Reaction score
6,565
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Nasra Mohammed amekemea baadhi ya Wanaharakati uchwara kutoka nchi za jirani kuingia jijini humo kuingilia masuala ya nchi ya Tanzania.

Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni kuwepo baadhi ya wanaharakati ambao waliwasili jijini Dar es Salaam wakiwa na matamko ambayo yanaenda kinyume na taratibu za Tanzania.

Ndg. Nasra akizungumza na maelfu ya vijana katika Uzinduzi wa Kijani First Time Voters uliofanyika Jijini Dodoma na mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewataka waache mara moja kuingilia tamaduni na utu wa Tanzania.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Wakae mbali na michakato ya Kitanzania, tuheshimiane na tuthirishane vitu ambavyo vinaenda kubomoa amani ya Taifa letu, Dar es Salaam kipaumbele chetu ni Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Ndg. Nasra

Katika hatua nyingine amewapongeza vijana hao ambao itakuwa ni mara ya kwanza kupiga kura mwaka huu wakiwa zaidi ya milioni 5 Tanzania na tayari wamejiandikisha kuhakikisha wanatunza kadi zao za mpiga kura na kuweka imani yao kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Nam na watapigwa tu

Wana bahati sana walikutana na watu wapole.

Leo ingekua funzo ukanda huu.
 
UVCCM ndo upuuzi gani, watu wanauwawa unaongelea dar es salaam. What is dar? mji wenyewe mchafu mchafu umejaa mapepo majalala. Hatuhitaji mavyama tunataka watu wasitekwe na kuuwawa.
 
Badala ya kutueleza soka yuko wapi analeta ngojera.Binafsi natamani washambuliaji wawe wengi,wengine watokee pembeni,kulia,kushoto na mawinga machachali ndo akili za kibinadamu zitawarudi
 
Nchi imejaa empty brains huyu Nasra ni mfano halisi
 
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Nasra Mohammed amekemea baadhi ya Wanaharakati uchwara kutoka nchi za jirani kuingia jijini humo kuingilia masuala ya nchi ya Tanzania.

Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni kuwepo baadhi ya wanaharakati ambao waliwasili jijini Dar es Salaam wakiwa na matamko ambayo yanaenda kinyume na taratibu za Tanzania.

Ndg. Nasra akizungumza na maelfu ya vijana katika Uzinduzi wa Kijani First Time Voters uliofanyika Jijini Dodoma na mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewataka waache mara moja kuingilia tamaduni na utu wa Tanzania.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Wakae mbali na michakato ya Kitanzania, tuheshimiane na tuthirishane vitu ambavyo vinaenda kubomoa amani ya Taifa letu, Dar es Salaam kipaumbele chetu ni Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Ndg. Nasra

Katika hatua nyingine amewapongeza vijana hao ambao itakuwa ni mara ya kwanza kupiga kura mwaka huu wakiwa zaidi ya milioni 5 Tanzania na tayari wamejiandikisha kuhakikisha wanatunza kadi zao za mpiga kura na kuweka imani yao kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Anafikiri yupo salama na hawezi kufanyiwa kama waliyomfanyia yule dada wa Uganda kwa sababu yeye amevaa guo la kijani.
 
Ukishaanza kucheza na damu za watu tu siku za utawala wako huwa zinahesabika.

Huyu ni mmoja wa aliyepigwa upofu asions kinachoenda kutokea. Sio sheria, it's nature
 
CCM Machineries ndio zinaanza kuingia kazini
 
1. Ikiwa Watanzania tuliwasaidia watu wa ANC ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Makaburu kule nchini Afrika Kusini.
2. Ikiwa Watanzania pia tuliwasaidia watu wa ZANU ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wazungu (Waingereza) kule nchini Zimbabwe.
3. Aidha, ikiwa Watanzania vile vile pia tuliwasaidia watu wa FRELIMO ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wareno kule nchini Msumbiji.

Je, ni kwa nini basi majirani zetu wa Kenya au Uganda nao wasiwe na Haki ya kuwasaidia Wananchi wa Tanzania ili waweze kuondokana na Utawala dhalimu na usiitenda Haki wa CCM hapa nchini sawa sawa kabisa na vile ambavyo waTanzania walifanya kwa majirani zao wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji?

Remember:
"Injustice somewhere is a threat of justice everywhere."
By Martin Luther King Jr.

HAKI haina mipaka, wala Haki haijali mipaka ya nchi.
 
Dawa inaingia BADO!!
KAZI ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom