Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,925
- 6,574
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Nasra Mohammed amekemea baadhi ya Wanaharakati uchwara kutoka nchi za jirani kuingia jijini humo kuingilia masuala ya nchi ya Tanzania.
Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni kuwepo baadhi ya wanaharakati ambao waliwasili jijini Dar es Salaam wakiwa na matamko ambayo yanaenda kinyume na taratibu za Tanzania.
Ndg. Nasra akizungumza na maelfu ya vijana katika Uzinduzi wa Kijani First Time Voters uliofanyika Jijini Dodoma na mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewataka waache mara moja kuingilia tamaduni na utu wa Tanzania.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Wakae mbali na michakato ya Kitanzania, tuheshimiane na tuthirishane vitu ambavyo vinaenda kubomoa amani ya Taifa letu, Dar es Salaam kipaumbele chetu ni Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Ndg. Nasra
Katika hatua nyingine amewapongeza vijana hao ambao itakuwa ni mara ya kwanza kupiga kura mwaka huu wakiwa zaidi ya milioni 5 Tanzania na tayari wamejiandikisha kuhakikisha wanatunza kadi zao za mpiga kura na kuweka imani yao kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi.