Nasikia kelele masikioni na kichwani

Nasikia kelele masikioni na kichwani

Pole sana ndugu, Leo ndio nimejua kama kuna tatizo kama hili.
Matatizo ya kiAfiya yapo mengi... Kujitokeza hadharani Kama hivi ni ujabari na kujiamini...
Kuliko kuficha!! Allah atampa takhfifu na uzima AMEEN
 
Salaams wana JF,

Ninasumbuliwa na kelele zinazovuma ndani ya masikio yangu na kichwani kwa ujumla. Usiku sauti inakuwa kubwa zaidi...
Ugonjwa unaitwa tinitus, unasababishwa na sikio kuwa exposed kwenye lous sound, kwa muda mrefu. Huwa inaisha yenyewe baada ya muda.

Usijaribu kabisa kuweka earphones kwa kipindi chote unachosubiri kupona, wala kwenda kwenye club za mziki ama kufungulia redio kwa sauti kubwa. In short stay away from any kind of loud noises

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wangu kanipasulia baloon sikio la kushoto, now masikio yote hayasikii nahisi kudata! Aliniita kama anataka Kuninong'oneza kitu kumbe ana lake jambo
 
pole sanaa. MRI inahusika hapo, wahi hospital kujua tatizo ni nini kabla hali haijawa mbaya mkuu.
 
Ugonjwa unaitwa tinitus, unasababishwa na sikio kuwa exposed kwenye lous sound, kwa muda mrefu. Huwa inaisha yenyewe baada ya muda. Usijaribu kabisa kuweka earphones kwa kipindi chote unachosubiri kupona, wala kwenda kwenye club za mziki ama kufungulia redio kwa sauti kubwa. In short stay away from any kind of loud noises

Sent using Jamii Forums mobile app
yaah hata Mimi kwa njia hii ndiyo nilipona kaka maana Mimi napenda sana earphone but now nimepunguza


silence
 
habari ndugu naona tatizo nililo nalo ni kama la kwako ila mimi ni sikio la kulia linatoa milio usiku naona uzi wako ni wa muda vipi ummeshapona au bado lina kusumbua na kama umepona ulitumia dawa gani?
vp mkuu umepata dawa utusaidie na sisi??
 
Duuu jamani hili tatizo pia linanisumbua sana sikio langu la kushoto,linapiga kelele nimekwenda hadi Ekenywa Hospital kwa Dr,Bingwa akanitoa nta lkn bado linasumbua,sasa karibia miezi 6 naomba mwenye kujua dawa jamani tusaidiane
 
Duuu jamani hili tatizo pia linanisumbua sana sikio langu la kushoto,linapiga kelele nimekwenda hadi Ekenywa Hospital kwa Dr,Bingwa akanitoa nta lkn bado linasumbua,sasa karibia miezi 6 naomba mwenye kujua dawa jamani tusaidiane
ulimaliza dozi maana Nina mda na Mimi sijaendelea na matibabu hapo
 
Samtaimu kuna tuvirusi tunashambulia koo lakini unasikia tatizo lipo kwenye sikio. So mda mwingine ni koo sema sikio linasikia/linahisi sana. Na mda mwingine kweli linakuwa limepokea maambukizi kutokea kooni! Ukienda kwa daktari wa koo masikio na pua atasaidia.

Mwenyewe mwenyewe unaweza kuamua kuongeza dozi ya matunda na mbogamboga ili kupona haraka, machungwa, ndizi etc na afya mwa ujumla ili kupambana na huto tuvirusi au tubakteria. Kama ni tubakteria utahitaji na antibiotic pia.
 
Mkuu pole

It could be Tinnitus (hizo kelele unazozisikia humo ndani)
Tinninus haina dawa kama ni mild inaweza kupotea yenyewe, ila kama ni moderate na severe haipotei

Ila nenda ENT mapema ukaangalie tatizo nini

Jaribu kukaa sehemu iliyotulia pasipokuwa na kelele nyingi usivae earphone pia
Sikiliza muziki kwa low volume. Maana tinnitus na kelele vitu viwili tofauti
 
Back
Top Bottom