Dar Ceramica yatinga Dodoma kwa kishindo

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
305
519
DODOMA Ijumaa Oktoba 6, 2023: Moja ya makampuni yanayoongoza katika vifaa vya ujenzi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, Dar Ceramica Centre, leo imefungua rasmi milango kwa wakazi wa Dodoma na mikoa jirani ili pamoja na mambo mengine kukidhi mahitaji yaliyopo sasa hivi katika miradi ya ujenzi inayoendelea katika Jiji hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo jipya lililofunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko, Bw. Raymond Nkya, alisema uamuzi wa kufungua tawi hilo ulisababishwa na maombi mengi kutoka kwa wakandarasi na watu wenye miradi ya ujenzi ya majumba na sehemu za ofisi Jijini hapo.

“Kama tunavyofahamu, Dodoma ndio Mji Mkuu wa nchi yetu ambapo ofisi zote za serikali sasa zinapatikana hapa.

Kumekuwa na miradi mingi sana ya ujenzi na wakandarasi wengi na watu binafsi wamekuwa wakiingia gharama kubwa kusafirisha mizigo kutoka matawi yetu mengine nchini kuja Dodoma na mikoa jirani lakini tumekuja na suluhisho kwani sasa mtapata bidhaa hapa Dodoma kwa ubora ule ule,” alisema.

Alisema Dar Ceramica imekuwa mstari wa mbele katika usambazaji wa tiles, vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo vya bafuni na chooni na pia vya kupendezesha nyumba kwani wanaagiza vifaa hivi kutoka kwa wazalishaji na wasambazaji bora kutoka Uropa na China. Dar Ceramica imekuwa ikitoa huduma bora kwa wateja katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati tangu mwaka 1995,” alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Nkya bidhaa za Dar Ceramica ni za viwango vya juu na zinapatikana katika matawi yote yaliyopo Dar es Salaam, Arusha, Geita, Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Mtwara, Mbeya na sasa Dodoma huku akiwaasa wakandarasi na watu binafsi wazingatie ubora katika miradi yao.

Aliendelea kusema kuwa wamepokea shuhuda mbalimbali kutoka kwa wateja wao kuhusu ubora wa bidhaa zao na hili limewafanya wazidi kuongoza katika soko kwa takriban miongo mitatu sasa.
Alitoa wito kwa serikali iendelee kutoa ushirikiano kwa biashara za ndani kama hii ya Dar Ceramica kwa kutumia bidhaa zao katika miradi inayoendelea Jijini Dodoma. “Tunajua kuna uhitaji mkubwa kwa sasa na tuko hapa kutoa suluhu,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule, aliipongeza Dar Ceramica kwa uamuzi wake wa kufungua tawi jipya katika Jiji la Dodoma kwani hatua hiyo itachangia katika kuhakikisha miradi inayoendelea inafanyika kwa ubora wa hali ya juu na pia itaongeza mapato ya Jiji hilo kwa njia ya kodi.

“Tunajivunia kama wana Dodoma kupata tawi la Dar Ceramica kwani pamoja na upatikanaji wa bidhaa kurahisishwa, ufunguzi huu ni ishara kuwa kutakuwa na ajira za moja kwa moja na ambazo sio za moja kwa moja kwa wakazi wa Dodoma,” alisema.

Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa wakazi wa Dodoma na mikoa jirani sasa hawatapata tena adha ya kusafiri mbali kutafuta bidhaa za Dar Ceramica ambazo sasa zitapatikana Dodoma tena kwa ubora ule ule huku akitoa wito kwa wakandarasi na watu binafsi wachangamkie ufunguzi huo.

“Tuko hapa leo kuunga mkono ufunguzi huu kwa sababu tumefuatilia tukaona kuwa rekodi yenu ni nzuri na tumejiridhisha kuwa nyinyi ni wawekezaji wazuri kwani tayari mko katika mikoa nane na Dodoma ni mkoa wa tisa.

Ofisi zetu ziko wazi kabisa kwa ushirikiano ili kwa pamoja tulete maendeleo katika Jiji letu la Dodoma,” alisema.
Ufunguzi huo uliwaleta pamoja viongiozi wengine wa serikali kutoka Jiji la Dodoma, wafanya biashara na wateja ambao walifika katika tawi hilo jipya.

View attachment 2774062
Wacha weee! Kuna taasisi wanachukua kwa mkopo na malipo ni mbinde. Kuna jamaa alikua anauza alminium materials wamekula mtaji wote hata PA kulala hana.
 
Back
Top Bottom