Cd4ever92
Member
- Mar 8, 2013
- 11
- 2
Habari wakuu. Mimi ni kijana, nina kazi nzuri tu inayoniingizia kipato cha kutosha.. Nina mpnz wangu ambae tulianza mahusiano nae mwezi March mwaka huu. Nilipanga yeye ndo aje kuwa mke wangu siku moja. Ila toka niwe nae sijawahi kuhisi raha ya mapenzi . Nliwah kugundua ana mahusiano mengne na watu wengine na pia kumfumania mara mbili na wanaume tofauti ila mara zote nimekuwa nikimsamehe akiomba msamaha.. Kilichonisukuma niandike uzi huu ni kitendo cha yeye kutoa ujauzito wangu wa miezi 3(japo sina hakika sana kama ulikuwa wangu) na tulikuwa tumeelewana kuulea. Nataman sana niachane nae ila kila nikijaribu kufanya hivyo najikuta naumia zaidi. Naomba ushauri nifanyeje kwan naogopa kuendelea nae kwa kuogopa makubwa zaidi