Nashindwa kumuelewa huyu mwanaume

Nashindwa kumuelewa huyu mwanaume

Wanawake bwana mna akili ndogo sana,
Kweli K ni K
 
Inategemea ila wengi ukiwasumbua wakikupata hamu yao kula na kusepa.

Kaa na unayempenda, kwa wewe kujiuliza inamaanisha kuwa unamfikiria.

Kaa na uliyenae kama unafuraha.
 
Habari zenu wapendwa,

Nina mahusiano na mwanaume wangu kwa muda mrefu sana ila kuna mwanaume mmoja alinitokea akawa ananipenda sana lakini sijawahi kumkubalia zaidi uwa tunawasiliana tu, ananisaidia vishida shida tena bila kumuomba, ni mkarimu mpole na hana maneno mengi.

Cha ajabu ambacho nashindwa kuelewa kwa huyu mwanaume amenitaka kwa muda mrefu sana sasa ila nimekuwa namwambia nina mahusiano na siwezi kuwa naye lakini hakati tamaa jamani kuna muda namjibu vibaya sana lakini kakomaa tu na mimi, ananitumia pesa kila baadaa ya muda ananiambia zitanisaidia shida ndogo ndogo.

Mimi nashindwa kumuelewa huyu mwanaume ndo atakuwa ananipenda sana au atakua ana shida zake tu anazozijua yeye.

Nipeni ushauri mwenzenu.


Huo ni mtihani na muamuzi ni wewe mwenyewe.....jaribu kumpa papuchi uone machungu ya wanaume wanaopenda kuchezea wasichana. Uko katika mahusiano mazuri na jamaa yako wa sasa (I guess), usichezee shilingi chooni utakuja juta.
 
Sisi wanaume sio watu wa mchezo mchezo huwa tunafuatilia papuchi hata kwa miaka mitano..!
Na hizo pesa anazokupa unasema ni ndogo ndogo, yeye sasa anaona ni vijipesa viduchu sana, akilinganisha na anachokitafuta kwako.
Zaidi zaidi unavyozidi kumzungusha ndio jinsi anavyopata mshawasha wa hiyo papuchi, yaani anakamia game kisawa sawa.

Ila ukila na wewe ukubali kuliwa, kama vipi mtunuku tu hiyo papuchi huyo mshikaji.
Ila usi-guarantee sana kuwa anakupenda.
As long as hujasema una tatizo na mpenzi wako endelea tu kuwa nae, ila hayo mambo ya pembeni usiyachukulie serious sana usije kutuletea uzi wa kilio humu.

sina mbavu kwako kiongozi umenichekesha sana., sasa umeanza kuweka siri zetu hadharani eti si wanaume si watu wa mchezo tunadowea paupuchi ata miaka 5.....
 
Unamkatalia ombi lake tu pekee lakini heller na vijizawadi hukatai eh!😀 Mungu anakuona..
 
mwanamke anakataa maneno...ila pesa anakula kimya kimya! teh teh..

kama kweli wewe ni mzalendo kwa mumeo, rudisha pesa zooote ulizokula...

Kisha toa taarifa kwa Mr wako...
 
Kama yuko serious mwambie aende kwenu kujitambulisha na kufuata procedures mfunge Ndoa.

Uchunguzi ni muhimu kabla hujafanya maamuzi yoyote
 
Jamaa kazimika kweli kweli hlf sasa ushajua anakupenda sn ndo maana unamtesa.
 
huyo jamaa mwingine una mahusiano nae muda gani?
kuna dalili ya ndoa? mfano utambulisho,mahari etc
na je yeye ni mtoaji?
Kwani wewe ni mtoaji?????. Isije ikawa ni upande mmoja ndio unaumia. Hiv kilakitu mnadai pesa tu. Kunavitu ni zaidi ya pesa/ utoaji.
 
Nilicho jifunza toka kwako.


1. Unampenda jamaa ndo maana unapokea vyake/pesa.

2. Umekuja kuomba ushauri kwasababu nafsi inakusuta.

3. Unaumia kuona mshikaji ulie nae atajisiakiaje/ atakuonaje akigundua unacheat.


Mwisho uamuzi ni wako. Kusuka au kunyoa. Cha mwaume hakiliwi bure. Iko siku huyo ulie nae ata kuudhi na utahitaji mtu wa kukufariji. Hapo ndipo shetani ataingia. Being desperate is very dangerous if kunakidume ashawahi kupa ufadhili lazima atakula tu. Jiulize kwanini ni rahisi kutongoza mwanamke ambaye wametoka kuachana na boyfriend wake
 
kosa ni kupokea pesa za jamaa, inamfanya ahisi bado kuna nafasi kama humpendi achana nae kabisa usimpotezee muda
 
Back
Top Bottom