Nashauri wanaochafua nchi wafilisiwe mali zao

Nashauri wanaochafua nchi wafilisiwe mali zao

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,966
Reaction score
5,558
Hapo vip!

Hii hali ya kuichafua nchi imekuwa biashara kwa wanasiasa na wanaharakati fulani fulani.

Kuichafua Nchi ni kitendo cha uhaini na watu hao wanafaa waweke Kwenye list ya maadui wa taifa letu.

Kuichafua nchi inapelekea nchi kujengewa mashaka na wawekezaji ambao walikuwa na nia ya kuja kuekeze kwenye taifa letu..maana yake ni kupotea kwa fursa za ajira ambazo zilikuwa zitolewe kwa Watanzania.

Nchi kukosa ushirikiano wa maendeleo, na misaada kutoka katika mataifa mengine. Haya madhara yote yanamkuta mwananchi na sio mtawala.

Ni wazi hizi sarakasi za akina Lema na watu wanaofanana na yeye zinatokana na aibu ya kukataliwa na wananchi na kwakufanya hivyo wanapata misaada ya kifedha katika mataifa husika waliowapatia hifadhi na watoto wao wanasomeshwa bure.

Nashauri serikali yetu sikivu kwasababu hii tabia inamea na inakuwa kwa kasi. Na watu wenyewe wanaochafua nchi wamechuma sana ndani ya nchi wanaoichafua basi serikali ichunguze mali walizonazo huku kisha wafilisiwe ili wanaposababisha maisha magumu kwa wananchi kwa kuisema na kutangaza nchi vibaya naye asiwe salama kiuchumi.

Sijawahi kusikia wala kuona mataifa ya Ulaya na America wananchi wake wakichafua nchi zao. Mfano mzuri China na Russia hamna Mzungu anayekimbia nchi yake na kujidai mkimbizi.
 
Kuchafua Nchi kivipi? Kuchafua Nchi kama kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani? Kuna kuchafua Nchi kama kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu? Unawaza uteuzi mpaka umejitoa fahamu zote? CCM ndiyo mnaichafua Nchi kwa matendo yao ya hovyo hovyo yasiyo na tija kwa Taifa
 
Kuwaza kuwapora watu mali zao kwa visingizio vya kuichafua Nchi hilo ndilo litaichafua Nchi maradufu, huu upumbavu wako wa kusuka mbinu za kuwachukulia watu mali kwa visingizio haramu vya kishamba na kishetani ndiyo kuichafua Nchi, matendo haramu ya CCM ndiyo yanaichafua Nchi
 
Naomba pia utoe ushauri kuhusu watu wasiojulikana na wale wote wanaotoa vitisho vya kiusalama kwa wengine, pia unatoa ushauri gani kuhusu vyombo vya dola ambavyo vinashiriki kuhujumu zoezi la uchaguzi huku vikijua fika ni kinyume na katiba na sheria za nchi, mwisho kabisa unatoa ushauri gani kuhusu viongozi wa serikali ambao wanakiuka na kuikanyaga katiba ya nchi yetu hadharani huku wakitoa maneno ya kejeli na ya kipumbavu kuhalalisha uvunjwaji huo wa katiba ya nchi yetu. Naomba kufahamu ushauri wako kuhusu hayo machache kamanda.
 
Hawachafui nchi. Wanasema ukweli uliopo. Hivi Lisu kusema kuwa alipigwa risasi 16 kwenye maeneo ya serikali yanayolindwa na mpaka leo hakuna hata mtuhumiwa anachafua nchi? Au anasema ukweli?

Jamani ee ukweli utabaki ukweli tu huwezi kubadili hata ukifunga watu midomo.
 
Wanaochagua nchi ni wale wanaojaribu uchaguzi kwa kuiba kura, kuua wapimzani na kuwakumbusha kesi za info zisizo na dhamana
 
Tofautisha kati na nchi na serikali kwanza,

Hao wanaokimbia nchi wanakimbia matendo maovu na machafu ya serikali ya awamu ya tano

Kwahio wanachokisema hao ni uchafu unaofanywa na serikali hii,kwahio serikali imejichafua yenyewe kwa kuua raia wake,kuteka, kuwabambika kesi,kuwafilisi nk

Kwahio serikali hii ikiondolewa ikaja inayotenda haki na kujali utu hayo hutayasikia na nchi itaheshimika
 
Back
Top Bottom