Nashauri Serikali kuwaita raia waliosaidia uokozi wa ajali ya ndege na kuwashukuru kwa kazi ya kizalendo na kishujaa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu kwanza Natanguliza pole zangu za dhati Toka ndani ya moyo Wangu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajari ya ndege ya Jana, Najuwa maumivu, machungu, majonzi, huzuni, simanzi waliyonayo mpaka Sasa, Najuwa wanalia mpaka Sasa, Najuwa wanabubujikwa machozi mpaka muda huu, najuwa chakula hakiliki mpaka muda huu, Najuwa miili yao haina nguvu mpaka muda huu, familia zao zimejaa machozi, watoto wao wamegeuka ndani ya muda mfupi na kubaki Yatima, wengine wamebaki wajane, wengine wamepoteza matumaini, lakini MWENYEZI MUNGU Ni Mkubwa hatawaacha peke yao, Naamini atawapa faraja nguvu na kuwatia Moyo katika kipindi hiki kigumu wanachopitia,

Watanzania wote tumeumia, watanzania wote tumesikitika , watanzania wote Tunalia. Taifa lote linalia na Taifa lote linaomboleza kwa kuwapoteza watanzania wenzetu waliopoteza maisha Katika uso wa Taifa na uso wa ulimwengu. Hakika Ni maumivu makubwa Sana kwa waliokuwa wanajuwa Kuna wapendwa wao waliokuwa ndani ya Ndege Ile, Hakika Mwenyezi Mungu awaangazie Mwanga wa Milele Marehemu wote.

Ndugu zangu pamoja na ajali Hiyo Kuna watanzania wenzetu waliojitoa na walioonekana mbele ya macho ya watanzania na macho ya ulimwengu wakijitokeza kwa ushujaa mkubwa, kwa moyo wa uzalendo, kwa moyo wa kishujaa kuwaokoa na kufanya shughuli za uokoaji kwa ndugu zetu. Hawa ni Raia wa kawaida wasiolipwa mishahara Wala kuwa na ofisi. Hawa Ni raia wa kipato Cha chini, Hawa Ni raia wa mitaani, Hawa Ni wazalendo wasiioonekana na kutambuliwa. Hawa Ni raia ambao ukikutana nao unaweza kuwadharau. Hawa Ni raia ambao unaweza kukuta Kuna siku waliomba kazi ya Jeshi lakini wakakosa nafasi kwamba hawana sifa,

Lakini ni Hawa leo wameonekana mbele yetu wakifanya shughuli ya kizalendo, wametupunguzia madhira na majonzi ambayo tungeyapata Kama Taifa Kama wangekwenda na kukaa kuanza kushangaa ili wahusika wafike kuokoa, lakini hawakusubiri Hilo, hawakusubiri Amri ya kuingia majini, hawakusubiri maelekezo, walihamasishana na kupeana moyo wa kishujaa kuingia majini bila kuhofia uhai wao, walijitoa na kujitolea kuwaokoa watanzania wenzetu.

Hakika wameionyesha Dunia namna Mtanzania alivyo jasiri, mzalendo na shupavu katika kujali uhai wa mwanadamu, wameionyesha Dunia yote kuwa Mtanzania atabaki kuwa Mtanzania, wameionyesha Dunia namna watanzania tulivyo na umoja na mshikamano wa kitaifa

Sasa hapa ndio napotoa Ushauri wangu kwa serikali yangu inayoongozwa na mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kuweza kuwaita watu Hawa ili kuwapongeza na kutoa Neno la shukurani kwao mbele ya vyombo vya habari na kuwaahidi Kuendelea kushirikiana nao na kuwasaidia watakapohitaji msaada wa serikali, kuwaahiidi kuwafungulia milango ya ofisi pale watakapofika kupeleka kero zao, hii itaonyesha moyo wa kuwajari na kuwathamini.

Hii itawapa ujasiri hata wale wa maeneo mengine, Ikumbukwe kuna watu wanaolipwa ambao walitakiwa wawe wamefika katika eneo la tukio haraka Sana walipo pata taarifa kutoka kwa rubani juu ya hatari iliyokuwa mbele yao,lakini Hawa raia wazalendo hawakupewa Taarifa lakini wakawa wa kwanza kufika eneo la uokozi na kutumia maarifa yao kuifanya kazi ya uokozi,

Serikali yangu Ni sikivu Sana na naamini itafanyia kazi ushauri huu japo ushauri Ni ushauri ambao huwa siyo lazima uchukuliwe, Naomba Radhi kwa nitakaye kuwa nimemkosea kutokana na bandiko langu hili kulitoa wakati huu wa majonzi, Naheshimu mamlaka na popote nilipoikosea Naiomba Radhi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Uokozi kani umefanyika pale, watu wanapiga simu kwamba oxygen inawaishia na maji yanazidi kujaa - hadi tunawapoteza.

Uokozi wa kamba? 2022 una mobilize watu kutumia kamba kuvuta ndege toka majini - acheni hizo, watu wameamua kunyamaza tu msiwachokoze.
 
Wananchi wameonyesha namna watanzania tulivyo wazalendo

Kwenye matatizo ndio wananchi Ni Wazalendo, lakini siku ile Pemba jeshi la JWTZ na Polisi walivamia Pemba kuua wanannchi kisa wanasapoti. Namshukuru Mungu sijawahi kuwa mwanachama wa CCM tangu kuzaliwa ni full laana.
 
Serikali imeona kilichotokea na itafanya uchunguzi kubaini mahali ambapo wahusika hawakutekeleza wajibu wao vizuri wa kiuokoaji

Serikali gani, hii ya Tanzania iliyoshindwa hata kuleta hitimisho la Moto soko la kariakoo. Serikali inachojua ni kuleta kesi za ugaidi kwa CHADEMA, ndio wanachokiweza basi. Serikali ya kijinga Sana.
 
Wazo zuri ila tunapowapongeza,tusisahau kuwaadhibu waliofanya uzembe(Vyombo husika)
Wala usijari ndio maana ya kufanyika uchunguzi kubaini chanzo Cha ajari na Kama Kuna uzembe ulifanyika katika uokoaji kutoka kwa wahusika
 
Serikali gani, hii ya Tanzania iliyoshindwa hata kuleta hitimisho la Moto soko la kariakoo. Serikali inachojua ni kuleta kesi za ugaidi kwa CHADEMA, ndio wanachokiweza basi. Serikali ya kijinga Sana.
Suala Hilo hakifai kuanza kuongoza uchama maana Ni suala la kitaifa
 
Kwenye matatizo ndio wananchi Ni Wazalendo, lakini siku ile Pemba jeshi la JWTZ na Polisi walivamia Pemba kuua wanannchi kisa wanasapoti. Namshukuru Mungu sijawahi kuwa mwanachama wa CCM tangu kuzaliwa ni full laana.
Tuondoe uchama katika suala hili maana tumepoteza ndugu zetu, tujadiliane kwa Nia ya kusaidia kutoa mawazo yatakayosaidia na kutuepusha na Yale yaliyotokea jana
 
Ndugu zangu kwanza Natanguliza pole zangu za dhati Toka ndani ya moyo Wangu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajari ya ndege ya Jana, Najuwa maumivu, machungu, majonzi, huzuni, simanzi waliyonayo mpaka Sasa, Najuwa wanalia mpaka Sasa, Najuwa wanabubujikwa machozi mpaka muda huu, najuwa chakula hakiliki mpaka muda huu, Najuwa miili yao haina nguvu mpaka muda huu, familia zao zimejaa machozi, watoto wao wamegeuka ndani ya muda mfupi na kubaki Yatima, wengine wamebaki wajane, wengine wamepoteza matumaini, lakini MWENYEZI MUNGU Ni Mkubwa hatawaacha peke yao, Naamini atawapa faraja nguvu na kuwatia Moyo katika kipindi hiki kigumu wanachopitia,

Watanzania wote tumeumia, watanzania wote tumesikitika , watanzania wote Tunalia. Taifa lote linalia na Taifa lote linaomboleza kwa kuwapoteza watanzania wenzetu waliopoteza maisha Katika uso wa Taifa na uso wa ulimwengu. Hakika Ni maumivu makubwa Sana kwa waliokuwa wanajuwa Kuna wapendwa wao waliokuwa ndani ya Ndege Ile, Hakika Mwenyezi Mungu awaangazie Mwanga wa Milele Marehemu wote.

Ndugu zangu pamoja na ajali Hiyo Kuna watanzania wenzetu waliojitoa na walioonekana mbele ya macho ya watanzania na macho ya ulimwengu wakijitokeza kwa ushujaa mkubwa, kwa moyo wa uzalendo, kwa moyo wa kishujaa kuwaokoa na kufanya shughuli za uokoaji kwa ndugu zetu. Hawa ni Raia wa kawaida wasiolipwa mishahara Wala kuwa na ofisi. Hawa Ni raia wa kipato Cha chini, Hawa Ni raia wa mitaani, Hawa Ni wazalendo wasiioonekana na kutambuliwa. Hawa Ni raia ambao ukikutana nao unaweza kuwadharau. Hawa Ni raia ambao unaweza kukuta Kuna siku waliomba kazi ya Jeshi lakini wakakosa nafasi kwamba hawana sifa,

Lakini ni Hawa leo wameonekana mbele yetu wakifanya shughuli ya kizalendo, wametupunguzia madhira na majonzi ambayo tungeyapata Kama Taifa Kama wangekwenda na kukaa kuanza kushangaa ili wahusika wafike kuokoa, lakini hawakusubiri Hilo, hawakusubiri Amri ya kuingia majini, hawakusubiri maelekezo, walihamasishana na kupeana moyo wa kishujaa kuingia majini bila kuhofia uhai wao, walijitoa na kujitolea kuwaokoa watanzania wenzetu.

Hakika wameionyesha Dunia namna Mtanzania alivyo jasiri, mzalendo na shupavu katika kujali uhai wa mwanadamu, wameionyesha Dunia yote kuwa Mtanzania atabaki kuwa Mtanzania, wameionyesha Dunia namna watanzania tulivyo na umoja na mshikamano wa kitaifa

Sasa hapa ndio napotoa Ushauri wangu kwa serikali yangu inayoongozwa na mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kuweza kuwaita watu Hawa ili kuwapongeza na kutoa Neno la shukurani kwao mbele ya vyombo vya habari na kuwaahidi Kuendelea kushirikiana nao na kuwasaidia watakapohitaji msaada wa serikali, kuwaahiidi kuwafungulia milango ya ofisi pale watakapofika kupeleka kero zao, hii itaonyesha moyo wa kuwajari na kuwathamini.

Hii itawapa ujasiri hata wale wa maeneo mengine, Ikumbukwe kuna watu wanaolipwa ambao walitakiwa wawe wamefika katika eneo la tukio haraka Sana walipo pata taarifa kutoka kwa rubani juu ya hatari iliyokuwa mbele yao,lakini Hawa raia wazalendo hawakupewa Taarifa lakini wakawa wa kwanza kufika eneo la uokozi na kutumia maarifa yao kuifanya kazi ya uokozi,

Serikali yangu Ni sikivu Sana na naamini itafanyia kazi ushauri huu japo ushauri Ni ushauri ambao huwa siyo lazima uchukuliwe, Naomba Radhi kwa nitakaye kuwa nimemkosea kutokana na bandiko langu hili kulitoa wakati huu wa majonzi, Naheshimu mamlaka na popote nilipoikosea Naiomba Radhi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Ikifanyika hii watajaa kijani tu hapo.
 
Back
Top Bottom