Nashauri salamu ya "Shikamoo" ifutwe

Bosi wangu ilikuwa nikimsalimia shikamoo anaitikia safi, nikaja kugundua hapendi hiyo salamu na toka siku hiyo kama ni asubuhi namwambia shikamoo

Ukagundua hapendi hiyo salamu halafu we ndo ukakomaa, lengo ikiwa nini hasa..?
 
Nikajua una salamu mbadala, kumbe utaahira tu. Sasa good morning ndio kitu gani? Yaani unasema shikamoo ni utumwa ila good morning ndio nzuri, kichwani una akili au makamasi?

Vijana wa siku hizi, badala watumie akili kufikiri wanatumia inye ndembe ndembe.
 
Duuuuh kama ni kweli basi nadhani BAKITA wa deal nayo hii kitu
 
Naunga mkono hoja, hii salamu imekaa kiwhack sana.

Kwanza lazima umtathmini mtu halafu ndio umsalimie, sometimes unaweza msalimia mdogo au sometimes unaweza msalimia mtu mzima salamu isiyo sahihi.
 
Shikamoo nafikiri ni neno lililotokana na waarabu. Tulifute tu. Na tuendelee kujuliana hali kwa mambo ya nyakati. kilugha kipo perfect ktk kusalimiana. Utasikia mwaomba, ulembwike, mghonile,....
 
Hakuna kabila linalosalimia kushika miguu wenzao bali ni kuulizana habari za asubuhi, mchana na jioni basi.

Tufanye direct translation kutoka lugha zetu za asili kwenda kiswahili. Utumwa umeisha ila sisi bado tunauendekeza.
 
Shikamoo nafikiri ni neno lililotokana na waarabu. Tulifute tu. Na tuendelee kujuliana hali kwa mambo ya nyakati. kilugha kipo perfect ktk kusalimiana. Utasikia mwaomba, ulembwike, mghonile,....
Wakoloni wote wameikuta Shikamoo! Wakaipenda maan yake wakaitumia kama kutukuzwa wao sasa.
 
Wewe sio lost id tu, bali ni lost akili pia!
 
Kajifunze kuchamba kwanza.
Unajua maana ya utamaduni?
Shroud.
 
source mkuu please usijekuwa unasema ya kwenye vijiwe vya bangi.
 
Shikamoo nafikiri ni neno lililotokana na waarabu. Tulifute tu. Na tuendelee kujuliana hali kwa mambo ya nyakati. kilugha kipo perfect ktk kusalimiana. Utasikia mwaomba, ulembwike, mghonile,....
Wanyaturu wao salamu zao ni matukio atakayokukuta unafanya ndio salaam.

Mfano akikute unakula, atakuambia unakula?
 
Binafsi siipendi kabisa hii salamu. Ukitazama hata lugha za makabila yetu ziko well organized kwa upande wa salamu kwa kuzingatia wakati(muda), ajabu ni hii shikamoo katika Kiswahili! Ina maana gani hasa? Je, ni kiashiria cha heshima au ni salamu kandamizi isiyo na maana yoyote ya msingi kijamii? Je, hatuwezi kurekebisha na kubadili mfumo wa salamu zetu ukategemea zaidi wakati na bado dhana nzima ya nidhamu ikibaki palepale?
 
Ewe mzee mwenye hekima tusaidie tafsiri ya neno 'Shikamoo'
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…