Nashauri Mrisho Gambo agombee ubunge 2020 Arusha mjini

Nashauri Mrisho Gambo agombee ubunge 2020 Arusha mjini

Hana lolote hata upinzani uweke jiwe,litashinda tu, ajiulize yule aliegombea na Lema, pamoja na kumwaga hela tumempiga chini,
 
Gambo awe waziri mkuu? Uyu anaepigania wanawake? Mnafiki mkubwa uyu aliemchongeza mkuu wa mkoa mpaka akatenguliwa?
Kiujumla Gambo ajawai kufanikiwa sehemu yoyote kwenye maisha yake,zaidi ya kupandikiza chuki na majungu.

Hoja yangu ipo hapo eti hajawahi fanikiwa sehemu yeyote
 
Ukombozi kama ni wa kisiasa haubaki hivo hivo kama hamna juhudi za kuulea
Yaani kwakweli Lema abadilike,aache kutenda zaidi kwa mdomo aonyeshe walau vitendo.Hatusemi atoe hela mfukoni asaidie maendeleo Lakini ajaribu kuwa karibu na w/nchi na kusikiliza kero zao,ili 2020 iwe rahisi kushinda.Lakini hii kuja kukurupuka mwishoni na visingizio kibao itakuja kumcost.Msimu ulioisha alisingizia hakua na madiwani,haya tumempa madiwani wa kutosha ashindwe mwenyewe...
 
Ana watoto wawili, mke, Masters, alikuwa mkuu wa wilaya sasa mkuu wa mkoa. Ana Masters pia... Yaani hajawahi fanikiwa??? Ngoja nikalale

Kuwa na mke ni kufanikiwa? Labda kuwa na mtoto. Na huo ukuu wa waliya kapewa ili adhoofishe upinzani hapa Arusha lakini hatoweza. Tumesimama Imara.
 
Mkuu nipo hapa picnic hapa kaunta hakuna anayeunga mkono hoja yako, sana sana wanashangaa mbona anajikweza kwa kumove na msafara wa polisi akijua yeye ni mkuu wa mkoa tu
 
Mimi ni mpenzi wa CHADEMA kwa muda mrefu sasa hapa mkoani Arusha lakini kasi ya huyu kijana Mh. Mrisho Gambo ni kubwa sana na mbunge wetu Lema asipogutuka mapema atakuta mwenzake yupo mbali sana.

Tangu awe Mkuu wa Mkoa amefanya vitu vingi na sensitive sana.

Kukutana na walimu wote, kukutana na waandishi wa habari, kujadili kuhusu utalii na changamoto zake mkoani Arusha, suluhisho la mgogoro wa murieti na ujenzi wa Kituo cha Polisi Kwa Morombo ni baadhi ya mambo machache tu na yanayotia hamasa na kazidi kumjengea umaarufu na imani kwa wana arusha wote.

Yule Mh. Lema ninayemjua sijui yuko wapi kwa sasa. Juzi tu Mh. Gambo kaagiza pesa zilizookolewa kutokana na madiwani kujizidishia zitumiwe kulipia madeni ya walimu. Kama ni hivi CHADEMA itasalimika kweli?

Mrisho Gambo gombea ubunge 2020 ili wapinzani wa jifunze na kurudisha ule ushindani uliopotea kwa muda mrefu.

Arusha tunataka maendeleo sio vurugu tena.

Wasalaam,

Unajuwa kuandika uongo lakini umesahau kuwa waongo hushindwa kumaliza story zao vizuri...umejinadi kuwa wewe ni mpenzi wa chadema lakini umesahau kusema kuwa wewe ni mwanachama wa ccm. ebu soma sentence yako ya mwisho
Hivi kwanini wana ccm wanajisaulishaga kwamba nchi kama imeharibika na kuogolea kwenye dimbwi la ufukara limesababishwa na ccm?
 
Yaani kwakweli Lema abadilike,aache kutenda zaidi kwa mdomo aonyeshe walau vitendo.Hatusemi atoe hela mfukoni asaidie maendeleo Lakini ajaribu kuwa karibu na w/nchi na kusikiliza kero zao,ili 2020 iwe rahisi kushinda.Lakini hii kuja kukurupuka mwishoni na visingizio kibao itakuja kumcost.Msimu ulioisha alisingizia hakua na madiwani,haya tumempa madiwani wa kutosha ashindwe mwenyewe...
Ukweli utamuweka huru. Kudos Mkuu
 
Hana lolote hata upinzani uweke jiwe,litashinda tu, ajiulize yule aliegombea na Lema, pamoja na kumwaga hela tumempiga chini,
Wapi molabani alitoa hela sana mwisho akaupigiza.Tutachagua chadema hata kama lema atakufa leo
 
Hakuna Chama chenye hati miliki na Jimbo.

Lowassa ndio aliwaponza ccm kwa kumhujumu Mrema aliekuwa Mbunge na kummbeba Demu wake Batlda kuwa Mgombea

Wachaga wakachukia wakampa Lema kwa hasira japo alikuwa hapendwi maana hana siifa za kuwa Mbunge

Ccm bado wakajichanganya tena wakampa Monaban Maasai wakati wanajua Uchumi wa Arusha umeshikwa na Wachaga.

na hali ya mabadiliko ya kiasiasa yalivyokuwa basi Lema alikuwa hana namna lazima ashinde

ccm wakizinduka wakajipanga vizuri wakaja na Mgombea anaetokea Mgombani mweye akili na maarifa wale wanya viroba hawana namna .

Labda Lema abadilike sana japo siku hizi ameanza kubadilika kuanzia michango yake Bungeni nk.

huo ndio ukweli mchungu wewe Chariiii ya ARA
Wewe naona umelivamia jukwaa la siasa kwa taarifa yako Arusha hatuna kabisa haja na ccm na kamwe hatutaichagua ccm daima dumu.....HATUTAICHAGUA CCM KAMWE
 
Wewe naona umelivamia jukwaa la siasa kwa taarifa yako Arusha hatuna kabisa haja na ccm na kamwe hatutaichagua ccm daima dumu.....HATUTAICHAGUA CCM KAMWE
Wewe kama nani? Kura watapiga wana Arusha.
 
Back
Top Bottom