Nashauri Manispaa ya Moshi itangazwe kuwa jiji 2022. Mashamba makubwa yaruhusiwe ndani ya mipango miji

z12f

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
638
467
Nashauri Manispaa ya Moshi itangazwe kuwa jiji in 2022.

1) Mji upanuliwe kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha, this is very important. Kamwe mji usipanuliwe Kaskazini mwa barabara ya Moshi-Arusha.

2) Sehemu ya kata za wilaya ya Hai na Moshi Vijijini, zinazopakana na Manispaa ya Moshi na zilizoko kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha, zihamishiwe kwenye Manispaa ya Moshi.

3) Katika eneo litakalohamishwa, contribution ya Moshi vijijini iwe kubwa kuliko contribution ya Hai, kwasababu Wilaya ya Moshi Vijijini ni kubwa (kieneo) kuliko Wilaya ya Hai.

4) Mipango miji ya Manispaa isiwabague watu wa kipato cha chini.

5) Mipango miji ya Manispaa isiwabague wazawa wenyeji.

6) Mipango miji ya Manispaa iruhusu mashamba makubwa na viwanja vikubwa sana kuendelea kuwepo ndani ya Manispaa.

7) Mipango miji ya Manispaa isilazimishe majengo marefu ndani ya Manispaa.

8) Mipango miji ya Manispaa isifute hati za kimila ndani ya Manispaa.

9) Kuwe na maeneo ya viwanja vya low density. Ambayo yata mimic Oysterbay na Masaki.

10) Maeneo ya makaburi ya waafrika yazungushiwe ukuta mfupi (wa futi 2). Na kuwe na gaps pana kwenye pande mbali mbali zitakazoruhusu magari mapana na watu wengi kuingia na kutoka kwa rahisi sana.

11) Serikali kuu ipeleke fungu kubwa la pesa litakalo boresha miundombinu ya Jiji hilo la Moshi.

12) Eneo la Mji wa Himo lipanuliwe (kwa upande wa kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha-Holili, unaopakana na barabara ya kwenda Dar es Salaam) na Miji wa Himo upewe hadhi ya Manispaa ya mji. Kanuni za mipango miji ya Himo zifanane na hizo hapo juu nilizoshauri kuhusu mipango miji ya Manispaa ya Moshi.

13) Kiwanja kidogo cha ndege cha Moshi mjini kihamishiwe Uchira (Kusini mwa Barabara ya Moshi-Arusha). Na kiwe na runway ya lami ya 3.3 kms.

14) Mipango miji mingine yeyote ya maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro ifuate kanuni za mipango miji nilizoshauri hapo juu. E.g. Mipango miji ya makao makuu ya wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro. Pia barabara za makao makuu ya wilaya zisile sana viwanja na mashamba ya watu.

NB: Mikoa mingine ya Tanzania (ambayo sio makao makuu ya nchi kama Dodoma na Dar es Salaam) inaweza kuiga kanuni hizi za mipango miji.

Asante sana.
 
Moshi mjini wachoyo kwa ardhi yao hawauzi kwa wageni waiendeleze pia wao wenyewe hawaiendelezi kuweka vitega uchumi vya maana mji uamke

Mji umechakaa utafikiri choo cha city mijengo mingi ya zamani design za kizamani utafikiri uko ujiji kigoma hakuna new estates development kubadili sura ya mji

Moshi kuipa hadhi ya jiji hapana hawajafikia hicho kiwango mji choka mbaya mno
 
Nami naiga kwa Mtwara kama ifuatavyo.

Kwa mujibu wa Mtwara Grand Masterplan itakua na Mji wa Mtwara na vitongoji vyote vinavyopatikana katika barabara tatu kuu zinazoingia Mtwara mjini ambazo ni:

1. Barabara kuu ya Mtwara-Mingoyo/Lindi-Kibiti to DSM. Hapa kwa mujibu wa hii itahusisha eneo lote la kuanzia vijiji vyote kabla ya Dangote, Dangote yenyewe, Msijute kuja hadi Mikindani(Wastani wa Kilometa 32)

2. Barabara kuu ya Mtwara-Nanyamba-Tandahimba-Newala-Masasi. Hapa itaanzia Nanguruwe, kuja hadi Mbawala Mailikumi hadi Naliendele(Umbali wa Kilometa 32 pia)

3. Barabara ya Mtwara-Mangamba-Mtawanya-Ziwani- Kilambo Boarder/ Msimbati(Ruvula Beach).

Hii itahusisha Mangamba, Mtawanya na Ziwani wastani ni kilometa 20
Hii ndiyo Masterplan ambayo niliwahi kuiona inaweza kuwa kuna baadhi ya vitu haviko 100% kama ilivyo lakini nilivyoisoma hiyo ilikua na mpangilio anagalau kama huo. Hii iliwekwa online, nafikiri google unaweza kusearch na ukaipata

 
Mkoa mzima wa Kilimanjaro ni mdogo sana yaani ardhi ni ya thamani sana kwa Wachagga, na wao ni wengi na kitendo cha kuuza ardhi kinaletaga mgogoro si tu kwa familia bali hata kwa jamii nzima.
 
mkoa mzima wa kilimanjaro ni mdogo sana yani ardhi ni ya thamani sana kwa wachagga, na wao ni wengi na kitendo cha kuuza ardhi kinaletaga mgogoro si tu kwa familia bali hata kwa jamii nzima.
Miji inayokua kwa kasi sasa hiivi ni le ambayo sio michoyo kuuza ardhi kwa wageni yenye mchanganyiko wa makabila mbalimbai

Moshi mjini wanataka jiji lenye mashamba makubwa!!!! la ardhi isiyoendelezwa!!!

Ukabila utaua Moshi mji sababu wazee hawauzi maeneo yao wala nyumba zao zivunjwe wawekezaji wapya wafanye yao!!

matokeo vijana wa kichaga wengi wamejenga na kuwekeza sana mikoa mingine Moshi mjini wametelekezea wazee wabaki nao na ardhi yao ndio maana haukui wala kuwa na sura mpya ya maana.

Moshi mbeleni waweza shushwa hata hadhi kutoka manispaa na kuwa mji wakiendelea na hiyo tabia sababu mji ni kama hauna generational success plan ya kuufanya uende juu
 
Waachieni Wachaga Moshi yao kama ilivyo. Isije kuwa kama Dar ambako wazawa wenyeji wameshindwa kukaa. Wazaramo na Warufiji ambao walikuwa Dar kabla ya nchi kupata Uhuru wameuza nyumba zao wameondoka. Jiji limejaa wageni.
 
Wivu tu unakusumbua
Magofu ya mji wa Moshi mjini ndio niyaonee wivu? angalia miji wasiokuwa wachoyo wa Ardhi ilishakuwa majiji siku nyingi angalia majirani wa Moshi mjini mfano Tanga lilishakuwa jiiji miaka mingi ukienda Arusha Mjini lilishakuwa jiji miaka mingi na ajabu wamejaa wafanyabiashara wa kichaga.

Kule wamejazana na kuliendeleza sababu ubahili wa Ardhi haupo na wenyeji wako tayari kuchanganyika na wageni wenye nacho wawekeze .Matokeo yake fursa kwa wenyeji zinakuwa nyingi. Moshi fursa kwa wenyeji chache mno kutwa wanakimbilia mikoa mingine sababu wenyeji hawana uwekezaji wa maana wa kuamsha ajira nyingi na fursa vitu vilivyojazana ni sehemu za kuuza pombe tu na nyama choma!!!

Wamkaa tu kukumbatia hopeless land ambayo imeachiwa vizee vikongwe ambavyo havina hata cha maana wanachozalisha cha kuamsha ajira na fursa nyingi.

Huwa nikisafiri unaingia moshi mjini unakutana na mishamba mikubwa hopeless mjini unajiuliza hivi hawa watu kichwani zimo kweli kimji kimebanana kasehemu kadogo imezungukwa na mishamba mingi mipori pori tu ukishatoka himo kwenda moshi mjini mfano haina hata tija ya uzalishaji wa maana wa hata kusema kumsaidia mtu aondokane na hata umaskini wake tu.
 
Upinzani umtuchelewesha sana. Subirini kidogo tumalize mambo ya chato. Mbunge wenu mliyemchagua atamaliza kipindi chake atakua anaweza kuchimba hata choo kwenye taasisi yeyote. Huku akidai jiji.
 
12) Eneo la Mji wa Himo lipanuliwe (kwa upande wa kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha-Holili, unaopakana na barabara ya kwenda Dar es Salaam) na Miji wa Himo upewe hadhi ya Manispaa ya mji.
Hii imepita tayari aliahidi Kimei na Magufuli kumuunga mkono. Himo itakuwa ya kisasa zaidi na itapendeza
 
Hii imepita tayari aliahidi Kimei na Magufuli kumuunga mkono. Himo itakuwa ya kisasa zaidi na itapendeza
Himo yaweza kuwa jiji kabla ya Moshi mjini cha msingi wa address issue ya ardhi kuna Mishamba mingi wakae waulizane wako tayari kuruhusu uwekezaji mkubwa kwa kuruhusu ardhi yao kutumika kiuwekezaji mkubwa au wataendelea kuikumbatia kama masai mwenye ngombe 2000 asietaka kuuza hata wawili anunue bati aezeke kibanda chake?

Issue ya ardhi moshi kwa sasa inazalisha maskini sio kitu cha maana tena Moshi

Umaskini mashambani moshi ni mkubwa mno wasiishi kwa mazoea wabadilike Ardhi is no longer a gold mine imebaki tu kama prestige kama ambavyo masai mwenye ngombe 2000 anavyojisikia presitdge kwa kitu kisichobadili maisha yake. Moshi na wamasai sasa hawana tofauti wote wanataka tu prestige kwa vitu visivyosaidia maisha.
 
Siwezi nikakukatalia, wala sikubaliani na wewe kwa asilimia zote, Lukuvi alisema nini kwa wenye viwanja ambavyo havijaendelezwa? Kama serikali ikiamua kupima mashamba yote nan mwenye ubavu wa kukataa? Issue ni urasimu tu wala sio wakaazi wa Moshi hakuna asietaka maendeleo
 
Back
Top Bottom