Nashauri hili Kuhusu kufunguliwa kwa shule na vyuo

Nashauri hili Kuhusu kufunguliwa kwa shule na vyuo

Nashauri, serikali ione haja kufanya tathmini ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona na itoe mwongozo mapema ili wazazi/walezi wajiandae mapema ki fedha na kisaikolojia kuhusu watoto wait kuludi shule hapo April,17,2020


Shule za watoto wa kishua wazazi wamepunguziwa ada kama wataendelea kufundishwa nyumbani naongelea IST na Braeburn
 
Nashauri, serikali ione haja kufanya tathmini ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona na itoe mwongozo mapema ili wazazi/walezi wajiandae mapema ki fedha na kisaikolojia kuhusu watoto wait kuludi shule hapo April,17,2020

Shule na vyuo viendelee kufungwa. Vichukue muda huu wa kufungwa sababu ya Corona virus kama likizo yao kubwa ya mwaka. Ikifika mwezi wa sita mwanzoni, na iwapo tutakuwa tumesalimika, basi shule na vyuo vifunguliwe na hakutakuwa na likizo kubwa ya mwaka. Mfano, vyuo vikuu huwa vinafungwa mwezi 6 - 9 kwa likizo kubwa. Mwaka mpya wa masomo huanza mwishoni mwa mwezi wa 10. Sasa , sababu ya coronavirus, tumefunga mwezi wa 3. Tuendelee kufunga mpaka mwezi wa 6.

Tukifungua mwezi wa 6 tuendelee mpaka mwezi wa 9. Ni miezi 3. Mwaka mpya wa masomo huanza mwezi wa 10. Hivyo, Ni kuunganisha. Hakutakuwa na mapumziko yeyote. Kwa mtindo huu, wahadhiri wanaostahili likizo za mwaka kisheria, wachukue sasa. Vyuo vikifunguliwa ni KAZI TU.

Hatua hii ichukuliwe kwasababu peak ya coronavirus Tanzania ni mwezi wa 5. Imeingia nchini mwezi wa 3. Kuruhusu nyuo kufunguliwa mwezi wa 4 wakati peak haijafika ni mchezo wa utani.
 
Hapo nafikr n kutumia simple calculation,likizo ya mwezi wa 6 na mwezi wa 12 zisiwepo wakae tu sahv angalau mpaka mwezi wa tano au sita mwanzoni baada ya hapo corona atakuwa Amerudi kwao China,watoto warejee mashulen wale kitabu mwanzo mwisho
 
Nawaonea huruma kidato cha sita, waliotarajia kuhitimu mwezi May 2020.... sijui itakuwaje..!!
 
share,
Good! Pia maandalizi ya kukabili mlipuko kwenye watu wengi unatia shaka.
 
WHO walitabiri maambukizi ya corona kuongezeka Africa ndani ya wiki mbili kuanzia wiki hii huku TZ ikitabiliwa kutakuwepo wagonjwa kuanzia 1000 mpaka 100,000!!

Nadhani serikali ingeweka weka angalizo kwa utabiri huo then ifanye tathmini early May kama kutakuwa hakuna kuongezeka kwa maambukizi the shule na chuo zifunguliwe wiki ya pili ya May na maisha ya kawaida yaendelee ila Tafadhali ziendelee kuzingatiwa. Ikiwemo kunawa mikono, kuvaa mask [emoji40] na kuepuka mikusanyiko isihokuwa na tija.

Karibia kila raia anavaa mask china, japan, Hong Kong na hii imesaidia sana kudhibiti kusambaa kwa corona 🦠 na wanaendelea na kazi kama kawaida. Serikali pia inaweza kuruhusu mtu mwenye uwezo avae mask muda wowote atavyojisikia ndani ya miezi 3.
 
Back
Top Bottom