Nasema tumechoka na mfumo DUME

Nasema tumechoka na mfumo DUME

Miss X

Member
Joined
Dec 18, 2010
Posts
97
Reaction score
137
Sijui nianze vipi, lakini kwa ufupi kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu sisi wanawake wa tanzania nasema kwa niaba ya wengi tumechoka na mfumo dume.

Kila mahali unaenda unakuta midume imejitutumuaaaaaa, mara miruzi fyuuuuuuuu, mara anti samahani oooooooh ~!@#@$%#@^#&$* tumechoka.Haya tuanze na majumbani mwetu, kila kitu kipaumbele anapewa mwanaume. Shule yeye, urithi yeye, nyumba yeye.

Tukija makazini hivyo hivyo, tunafanywa kama vitu, hupati kazi mpaka utangulize kitu.Jamani tumechoka.Tukija katika uchumi, tunadhalishwa sana na hatuthaminiwi juzi shangazi yangu karudi nyumani kakuta mjomba kauza mazao yote aliyolima.

Tumejaribu tumeshaweza kuwa na benki yetu, maana nyingine zimekuwa zikitunyanyapaa na hazijui mahitaji yetu. Kutokana na malaamiko yaliyomo vyuoni na sisi tunataka chuo chetu kikuuu tusinyanyaswe kijinsia na mijibaba mikware yenye kutoka udenda ionapo mwanamwali.

Bado kwenye nafasi za uongozi wa nchi hii tumesahauliwa tunadharauliwa sana. Yaani isingalikuwa wabunge wa viti maalimu, wabunge wanawake wangekuwa wa kuhesabu. Mwaka huu na sisi tunataka raisi mwamamke.

Historia ambayo imepindishwa pindishwa kuhusu uhuru wa nchi hii. Wanawake hawatajwi kabisaaaaa. Nauliza: Hivi ni wanaume peke yao ndio waliopigania uhuru wa nchi hii. Ni budi sasa iandikwe upya. Sisi tulishiriki kwa hali na mali zaidi, tena zaidi kupigania uhuru wa nchi hii, tulikuwa wahamasishaji wakubwa mikoani kuanzia Usangi mpaka Uyole. Mtwara mpaka Ngara. Kama si wanawake wa nchi hii usingepatikana. Toka uhuru tumekuwa tukipewa ahadi hewa, mnatutumia tu kushida huku mkituachia kanga, tishert , elfu kumikumi na sahani za wali miharagwe, lakini hamtekelezi madai yetu. Mwaka huu nasema hatukubali tena kutumiwa. PATACHIMBIKA


Kwa kumalizia ni haki katika nchi hii, sisi kinamama wa nchi hii mifumo ya mahakama imejaa mfumo dume tunaonewa mahakamani hatupati haki. Mahakimu wengi wanaume, wazee wamahakama wengi wanaume, majaji weeeeeeengi wanaume. Tena nauliza toka uhuru mpaka sasa mbona kumekuwa na wasomi wengi wanawake?, mbona hakuna jaji mkuu mwanamke. Ni wakati sasa na sisi wanawake tupate mahakama zetu. Mashauri yote ya yanayousisha wanawake yapelekwe kwenye mahakama zetu, natena nasema na sisi ni raia wa nchi hii.

ONYO :

  1. WANAUME ACHENI WANAWAKE TUDAI HAKI ZETU.
  2. WANAUME ACHENI BUNGE NA SEREKALI WAFANYE KAZI ZAO PINDI WATAKAPOAMUA KUTEKELEZA MADAI YETU.NASEMA ACHENI KABISA
  3. MADAI YETU NI YAMSINGI OLE WAKE ATAKAYEYAPUUZIA NA KUKEBEHI
​TUNAJUA TUNATAKA NINI KATIKA NCHI HII NA SISI NI WALIPA KODI PIA.

Tukiwezeshwa tunawezaaaaa
 
Mmepewa uwaziri wa ardhi na nyumba mmeacha kazi mnaenda kukwapua mabilioni ya escrow! Hamna shukrani nyie mijike!
 
Sijui nianze vipi, lakini kwa ufupi kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu sisi wanawake wa tanzania nasema kwa niaba ya wengi tumechoka na mfumo dume.
Kila mahali unaenda unakuta midume imejitutumuaaaaaa, mara miruzi mara weweeeeeeeee tumechoka aaaaaaaaah.
Haya tuanze na majumbani mwetu, kila kitu kipaumbele anapewa mwanaume. Shule yeye, urithi yeye, nyumba yeye.
Tukija makazini hivyo hivyo, tunafanywa kama vitu, hupati kazi mpaka utangulize kitu. jamani tumechoka.
Tukija katika uchumi, tunadhalisha sana lakini hatuthaminiwi juzi shangazi yangu karudi nyumani kakuta mjomba kauza mazao yote aliyolima.

Tumejaribu tumeshaweza kuwa na benki yetu, maana nyungine zimekuwa zikitunyanyapa hazijui mahitaji yetu. Kutokana na malaamiko yaliyomo vyuoni tunataka chuo chetu kikuuu tusinyanyaswe kijinsia na mijibaba mikware yenye kutoka udenda ionapo mwanamwali.

Bado kwenye nafasi za uongozi za nchi hii tumesahauliwa tunadharauliwa sana. Historia ambayo imepindishwa kuhusu uhuru wa nchi hiii ni budi sasa iandikwe upya, sisi tulishiriki kwa hali na mali zaidi tena zaidi kupigania uhuru wa nchi hii, tulikuwa wahamasishaji wakubwa mikoani kuanzia usangi mpaka uyole. Mtwara mpaka Ngara. Kama si wanawake wa nchi hii usingepatikana.


Kwa kumalizia ni haki katika nchi hii, sisi kinamama wa nchi hii mifumo ya mahakama imejaa mfumo dume tunaonewa mahakamani hatupati haki, ni wakati sasa na sisi wanawake tupate mahakama zetu. Mashauri yote ya kinamama na yanausisha wanawake yapelekwe kwenye mahama hizo, natena nasema na sisi ni rahia wa nchi hii.

unataka mfumo jike?
 
usipigane na ukuta utaumia mwenyewe, kasome vizuri vitabu vya dini natumaini utaelewa kwa nini ke ni second class human beings
 
Mfume dume ni jinsi ulivyoset mind yako! But kiuhalisia hakunaga hii kitu...! Huwezi kukuta baba anaforce kumpleka boy kilaza shule anaacha jinias girl home hakuna hii mambo! Nyie tatizo mgawanyo wa kazi nao mnaona mfume dume mfano kazo za kijeshi mara nyingi zinawavutia wanaumw kuliko wanawake na kwa mwenye akiri km yako utasikia jeshini kuna mfume dume! Mbona namba ya manesi na masecretary wa kike ni kubwa na sisi hatulalamiki!

Mnapewa upendeleo kwenye viti maalum wabunge kana kwamba kuna sehemu katiba au sheria imeweka kipingamizi kuwazuia. Makazini kujipendejeza na kupenda kuonewa huruma ndiyo kuna waponza mkiomba kazi na boys nyie mnatka muonekane so special kwa maboss wasiwake watakuja mburula kiasi gani hamtaki uwanja sawa wa kushindana.

Kitu kingine mnajiweja nyuma mno mara hooh...! Wanawake tukiwezeshwa tunaweza nani awawezeshe bila fadhira dawa yenu kuliwa tuuuuh...!

Mwisho mnapenda mno vya dezo familia tusipo kula hamna chakula aliyekosea baba! Ata nyie mademu zetu mnakera unakuta unapesa afu unabeep nipige kwa mwendo wa kubeep utapata wapi fursa ya kunigombeza kwa heka yangu niliyotolea jasho nisikukatie simu! Kiufupi kulalamika hakuwasaidii km hamjui kelele za mfume dume ni diri kwa wenzenu wajanja wanaendesha Ngo,s na wanakula pesa nyie mnabakia kulalama fanya kazi na jitambue utatoka how womens they hv a a good positions in the government but they dont care mayowe yenu!
 
hii hoja yako ulitakiwa huilete miak ya 90, sasa hivi mnapewa fursa nyingi sana mnashndwa zitumia. Just imagine kwenye sector ya elimu mnavyo bebwa.
Kumbuka si kila sehemi inahitaji huruma, kuna sehemu zingine zinataka mtu anae qualify, so acheni kulalamika na pigeni kazi, wanaosoma wasome
 
hii hoja yako ulitakiwa huilete miak ya 90, sasa hivi mnapewa fursa nyingi sana mnashndwa zitumia. Just imagine kwenye sector ya elimu mnavyo bebwa.
Kumbuka si kila sehemi inahitaji huruma, kuna sehemu zingine zinataka mtu anae qualify, so acheni kulalamika na pigeni kazi, wanaosoma wasome

wanataka wabebwe ndo wazione fursa, mimi sipendi kuona mwanamke analalama kila kitu, hebu na sisi tuonyeshe uwezo,natolea tu mfano mdogo, ukija humu jf ukiingia majukwaa kama sayansi na tech, siasa, biashara, wanawake ni wachache, ila ukiingia kule kwenye mapenzi wamejaaa hakianani hakuna post inayowapita
 
unataka mfumo jike?

dada, ngoja nizungumze upande wa elimu, kuna shule za wasichana tupu, za serikali na za watu binafsi, lakini kinachoshangaza hizo shule nyingi ndo za mwisho kitaaluma, kwanza uendeshaji mbove, kwa kifupi mimi napingana na mada yako

kama sisi wanawake tunataka kuinuka ni lazima tujikubali sisi kama sisi, tupeane support wanawake kwa wanawake, tusisubiri aje mwanaume ndo atupe support, cha kushanga huko maofisini wanawake tunaongoza kwa kuchukiana na majungu, yani mwanamke anaona ni bora aongozwe na mwanaume kuliko kuongozwa na mwanamke mwenzie, hebu tubadilike jamani tuache porojo na lawama kila kukicha
 
wanataka wabebwe ndo wazione fursa, mimi sipendi kuona mwanamke analalama kila kitu, hebu na sisi tuonyeshe uwezo,natolea tu mfano mdogo, ukija humu jf ukiingia majukwaa kama sayansi na tech, siasa, biashara, wanawake ni wachache, ila ukiingia kule kwenye mapenzi wamejaaa hakianani hakuna post inayowapita

umesema vema kabsa, badilikeni ama sivyo mtalia kila siku
 
Back
Top Bottom