Nasema sijui tena sijui! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasema sijui tena sijui!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by everybody, Feb 23, 2011.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Fuatilia haya majadiliano na mheshimiwa ..., Duh!

  Swali: Mheshimiwa Rais je unawajua wamiliki wa kampuni ya Dowans?


  Jibu:
  Nasema mimi sijui, ni kina nani sijui,
  Wanatoka wapi sijui, walifikaje sijui,
  Kama nawafahamu sijui, kama wananijua sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Swali: Mheshimiwa Rais, lakini waliingia nchini na kupata Mkataba wa Richmond na kuleta majenereta katika kutekeleza mpango wako wa kupunguza tatizo la umeme nchini kweli huwajui?

  Jibu:
  Nasema mimi sijui!, kwanini walikuja sijui,
  Uhusiano wao siujui, Kama nao Richmond sijui,
  Waliingia kwa lipi sijui, na walirithishana vipi sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Swali: Lakini ulisema kuwa Richmond ni kampuni Hewa kama Kamati ya Mwakyembe ilivyoonesha na kudai, na ukatoa pongezi! Unawaeleza vipi Watanzania kuwa Taifa liko tayari kuheshimu mkataba wa kampuni ya kitapeli?

  Jibu:
  Nasema tena sijui!Kama kampuni hewa sijui,
  Kama ni matapeli sijui, Kama walibebwa sijui,
  Wahusika kina nani sijui, Mwakyembe alijuaje sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Tulikoanzia sijui, tumefika vipi sijui,
  Nahusika vipi sijui, nimuulize nani sijui,
  Niwaridhishe vipi sijui, nianzie wapi sijui!
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini Rostam Aziz ametajwa kuhusika kuanzia mwanzo wa sakata hili na yeye mwenye amekiri kuhusika na hili kwanini usimuulize ili ujue?

  Jibu:

  Nitamuanza vipi sijui, Rostam huyu sijui,
  Kama mwingine sijui, anahusika vipi sijui
  Nimuamini nani sijui, kama ni kweli sijui!
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Swali: Lakini, inawezekana vipi usijue wakati una vyombo vingi vya usalama ambavyo vingeweza kukupata taarifa mbalimbali za kiinteligensia kama walivyoweza kuzipata kule Arusha na kuvunja maandamano ya Chadema? Kwanini hujapatiwa taarifa za kiinteligensia kuhusu Dowans?

  Jibu:

  Intelligensia mimi sijui, nani anipe sijui,
  Kwanini wanipe sijui, nifanye nayo nini sijui,
  Wasiponipa sijui, kama nadaganywa sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Nani awaagize sijui, kama nini mimi sijui,
  Au makamu sijui, Waziri Mkuu sijui,
  Wajitolee tu sijui, au ni Bunge mimi sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Swali: Sasa msimamo wako wewe binafsi kama Rais ni upi, Dowans walipwe au wasilipwe?

  Jibu:

  Msimamo gani sijui! Kama ninao sijui,
  Nilikuwa nao sijui, nitakuwa nao sijui,
  Kama walipwe sijui, na wasilipwe sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Wizara ilipe sijui, Au Tanesco sijui,
  Au huko hazina sijui, au hapa Ikulu sijui,
  Bunge litenge fedha sijui, au Mahakama sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Swali: Sasa mheshimiwa inaonekana hujui mambo mengi tu; kuna mambo mengine yoyote unayoyajua?

  Jibu:
  Kwanini masikini sijui, Kagoda ni nani sijui,
  Meremeta nani sijui, Dipu Grini nani sijui,
  Mbona elimu duni sijui, wanagomea nini sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Sijui mimi sijui, mengine mengi sijui,
  Ya kilimo siyajui, ya Sayansi siyajui,
  Mambo ya maji sijui, umeme ndiyo sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Kama napendwa sijui, kama nachukiwa sijui,
  Nafurahiwa sijui, au nakejeliwa sijui,
  Kama ninachekewa sijui, au nakebehiwa sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!

  Swali: Mheshimiwa swali la mwisho; asante sana kwa kutupa nafasi hii na kwa hakika umetuelewesha na tumeelewa kuwa hujui mambo mengi sana. Labda uwaambie Watanzania, je wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

  Jibu:

  Sijui mimi sijui, ninarudia sijui,
  Kama miye sijijui, mtajuaje sijui
  Kama najua sijui, kama sijui sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha kweli ila nimecheka mpaka machozi!Kweli rais tunae...!
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  mwanakijiji alisha ileta
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  You are amazing....one of the most useful threads i have ever read at JF....
   
 5. R

  Rugemeleza Verified User

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndiyo matokeo ya kupachikiwa viongozi wa kuchongwa na watoto wa Saigoni. Mtu hana sifa za uongozi na hawezi kuongoza lakini anawekwa pale kututopesha katika lindi la umasikini. Hatumtaki nasema hatumtaki ewe Mwenyezi Mungu tunaomba utusikilize na kutuondolea maafa na maangamizi haya tuliyojitakia.
   
 6. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mods tunaomba muiunganishe hii thread na ile iliyoletwa na Mwanakijiji
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Kila mnapo-reproduce kazi za mwanakijiji, ni vizuri kutoa credit zinazostahili.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hili shairi sijui nani kalikuta leo ofisini maana limezunguka sijui mara ngapi? Thanks kwa wale wanalizungusha ila sijui kama ni vizuri au vibaya maana limefika sehemu nyingine hadi naogopa. Well.. maji yameshamwagika.
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Nadhani wanalitoa kwa Wanabidii hapa
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  ooh I got it.. thats why.. lakini almost what two weeks later? LOL
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  kama huna cha kukoment unakausha. mods wenyewe wanajua kazi yao
   
 12. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Siwezi kausha kwa kuwa nilikuwa na cha kukoment...nacho nilikipata baada ya kugundua kuwa content ya hii thread ni duplication ya ile iliyoletwa na Mzee Mwanakijiji.

  Wana JF tunatakiwa kuleta mambo mapya on time na siyo kuwa na mawazo mgando kama ya kwako.
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  si unajua tena. unaenda shule hujui hata kutamka one, two, three, four, five, six, seven, eight, nine, ten.

  mwalimu akisha kufundisha kila aliyeinyaka utaskia wanaimba one, two, 'free' four, five, ....

  hatimaye kila mtoto atajua.

  wengine ndo kwanza wameona leo. na hii ni muhimu sana. kadiri siku zinavyosonga watu wengi watakuwa wanajua kuwa nchi yetu inaongozwa na Mr. Sijui.
   
 14. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Tanzania kubwa ndugu yangu. usishangae shairi la mwanakijiji linajulikana na nyie wenye akses ya mtandao tu. lakini hili linatakiwa kuzagaa na kusomwa nchi nzima na kusomwa na kila mwanamageuzi na wahafidhina wote.

  bado hili kabrasha la mwanakijiji halijazunguka kama unavyodhani.

  tena naomba mods wawasiliane na mwanakijiji wabadilishe heading. waondoe ile ya kidhungu, waweke ya kiswahili yenye mvuto zaidi.
   
 15. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Niliposema duplication nina maana ya kuwa wazo au habari hiyo hiyo inaletwa JF zaidi ya mara moja.Ikiwa lengo ni shairi kuwafikia watu wengi zaidi: basi shairi hili lapaswa kusambazwa kwenye mitandao mingine yenye kutembelewa na watu wengi zaidi kama blogs mbalimbali za wabongo,websites za waTz,facebook,wanabidii..nk. Wengine mwaweza tuma kwenye magazeti ya wanaharakati kama makala.

  Ikumbukwe kuwa si watu wengi sana wanaoifahamu JF ,kwa hiyo kuposti kitu hicho hicho zaidi ya mara moja humu JF hakutasaidia coverage ya watu wengi zaidi bali ukitaka coverage access do as I suggested.
   
 16. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee mwanakijiji, sikujua origin yake i could have aknowledged you, sorry for that. Ila nimekutana nayo nikaona niiwasilishe JF. Sikujua kama ulishaipost before. Ila siyo mbaya kukumbushia maana mjadala wa Dowans umeanza upyaaaa bada ya huyu anayejiita owner wa Dowans kutua Dar. Anyway, i aknowledge your creativity.
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Yoooooooooooooooooooooooote hajui ila kucheza kiduku ni nambari wani.HASARA KWELI KWELI.
   
 18. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Ni kazi nzuri mwanakijiji.nakupa credit.hata mimi napenda sana kujadili maudhui yake na watu.kama nakukwaza sijui,kama skukwazi mi sijui.
   
Loading...