Nasema Rais Magufuli hawezi kutoka madarakani

Nasema Rais Magufuli hawezi kutoka madarakani

Iko hivi si kwamba madikteta wanapenda sana kuongoza wanaogopa watarudije Kwa jamii waliyoiumiza hali hawana ulinzi hivo Salama yao ni kung'ang'ania Madaraka au kuweka atakaemlinda still nayo sio Salama. Mfano Kabila bado ni Kijana ataingia mwingine asiyeside Na tsekedi atamnyoosha Kabila kumlipizia kisasi hata kama ni miaka 30 ijayo akiwa Mzee atavuna.Hata maliyamungu ajiandae tu hata kama ni miaka 30 ijayo watamlipizia kisasi maana atakuwa nje ya mfumo ushawatema.Hawana Madaraka hawana ulinzi
 
Mkuu, pia Museven alipojiona kijana alibana umri wa kugombea urais uwe chini ya miaka 75 ili wazee wasim-challenge ila yeye kwa sasa ana miaka 77 amebadili katiba eti umri wa kugombea urais usiwe na ukomo. Yani hawa madikteta wanaweka sheria na matamko kwa wakati walio nao na wanabadilisha hayo kutokana na muda na muda ilimradi waitendee haki nafsi yao.

Kinachomuokoa m7 na still anadunda ni kacheza Na mambo 2 kutogusa maslai ya mabeberu Na kutosomesha namba watu wake,shida ya students mjuaji ye anasomesha wote si beberu si wanyonge.Ukigusa maslai ya mabeberu lzm watakuondoa Ukigusa maslai ya wananchi wako lzm watakuondoa
 
dogo - kauli ya karibuni, sitaondoka bila kuongeza mishahara
7) maendeleo hayana vyama - wanotaka kuja CCM wanakaribishwa ili tujenge nchi
8) safari nimeteua wakurugenzi wa halmashauri makada wa CCM ili wakasimamie vizuri ilani ya CCM - leo wanasema eti wakurugenzi wa halmashauri siyo makada ila ni wanachama tu wa CCM
9) ambaye atakosa chakula hakuna chakula cha msaada, watanazania nawapenda sana - unaowapenda utawanyima chakula kukiwa na janga?; n.k. n.k.

Je, tunaweza kuendelea kumwamini
Du! Watu mna kumbukumbu!!!! Ama kweli watu mna takwimu na nukuu
 
Iko hivi si kwamba madikteta wanapenda sana kuongoza wanaogopa watarudije Kwa jamii waliyoiumiza hali hawana ulinzi hivo Salama yao ni kung'ang'ania Madaraka au kuweka atakaemlinda still nayo sio Salama. Mfano Kabila bado ni Kijana ataingia mwingine asiyeside Na tsekedi atamnyoosha Kabila kumlipizia kisasi hata kama ni miaka 30 ijayo akiwa Mzee atavuna.Hata maliyamungu ajiandae tu hata kama ni miaka 30 ijayo watamlipizia kisasi maana atakuwa nje ya mfumo ushawatema.Hawana Madaraka hawana ulinzi
Umenena vema!.
 
Ukishaona tu kiongozi haheshimu box la kura basi jua huyo kutoka madarakani ni kwa machafuko.
Du! Leo kuna vitu adimu humu! Hii inaweza tokea, maana sioni dalili zozote za huyu mutu kutoka
 
Wanajamvi kulingana na utendaji kazi wa Mhe Magu na huruka zake mimi nasema hawezi kutoka madarakani kwa hiari yake!.

Nasema hivyo kwa sababu watu wenye utendaji wa aina yake haijawahi kutokea wakaachia madaraka, na hii ni kwasababu;

1.Wanaamini kuwa wao ni wanauwezo mkubwa kuliko viongozi wenzao, wananchi wengine, n k, na kila uamzi waufanyao ndio mzuri kwa mstakabali wa Taifa.

2.Wanaamini kuwa wana maadui wengi wa ndani na nje.

3. Wanaamini kuwa kila kitu wanakijua na wanakiweza, na kutaka kifanyike kulingana na mtazamo wao na sivinginevyo.

4.Dunia ya ushirikishaji na maamzi ya pamoja kwao ni mwiko.

5. Ni mwendo wa maagizo tu kulingana na waonavyo wao.

6.Hawapendi kukosolewa wanapenda kusifiwa tu. Ukikosoa unageuka kuwa adui wake na Taifa.

7. Wanaamini lazima ndoto na fikra zao zitimie wakiwa bado wapo madarakani.

8. Hahahahahaaa, hawaamini kuwa kuna nguvu ya asili na inaweza kutokea wakati wowote na kufanya chochote bila kizuizi, n.k.

Viongozi wenye karba kama hiyo ni kama;
-John P. Magufuli
-Paul Kagame
-Yoweri Mseven
-Ally Bushir
-Gadaff, n.k.

Kweli Mhe Magu wetu mwenye karba hizo anaweza kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe?, mimi nasema hawezi kuachia madaraka kwa hiari!.
JPM anaweza kuishi uraiani bila uraisi kweli? 'public relation' yake ni very poor sana ndani ya chama chake na nje yachama, kwa matajiri na wanyonge kwa wasomi na wasio wasomi sera zake zimegusa kila aina yawatu.....kuna watu wamepoteza muelekeo wa maisha kimzaha mzaha wengine wamekufa kwa stress za maisha biashara za watu zimefunga bila sababu.....unadhani hao watu wote watamsamehe? kunyantuka kwake inaweza ikawa 'turning point' ya siasa za Tz.....lazima katiba itaguswa kinga ya maraisi iondolewe
 
Ni kweli hata mimi naamini hawezi kutoka. Ulinzi alio nao sasa hivi unadhihiri hilo. Mwanzao alikuwa hata barabara hafungi akitoka, sasa hivi ni balaa. ndo atoke awe bila madaraka thubutu. Tuone tungoje. time will tell
Ktk katiba ya chama changu ccm atabaki lakini ktk Nchi wananchi wakiamua anaondoka kumbuka hata Mkapa alipitia upepo wa kisiasa kama huu kwa hiyo naye ataondoka .
 
Kwanza lazima hawa wanaofananisha hizi Nchi na Nchi yetu lazima waangalie katiba ya Nchi inasemaje sio ya chama kwani ya chama anaweza kufanya atakavyo sio ya Nchi
Sasa mbona iko wazi kuwa watatoka tu madarakani siku moja. Kwa namna yeyote watatoka na mara nyingi sio mwisho mzuri. Umetoa mifano nadhani tunajua mwisho wa Gaddafi na Al Bashir wa Sudan ulikuaje. Hao Museveni na Kagame tunajua fukuto la nchini kwao. Hebu usimletee uchuro wa kwetu. Usitake kumsababishia matatizo. Akimaliza muda wake atakaa pembeni
 
Ndugu yangu naheshimu mawazo yako, ila pia jaribu kufuatilia kwa kupitia historia kidogo ya viongozi mbali mbali Dunia wenye karba ya Mhe wetu utajua ninacho maanisha!.

Lakini pia uzoefu unaonyesha muda mwingine mhusika anaweza akawa anatengeneza mazingira hata yeye bila kujua, nahatima yake mazingira na huruka zake zikamlazimisha kufia madarakani au kufurushwa madarakani!.
Huo ni mtazamo wangu na naomba kwa Mungu iwe hivyo kama katiba yetu inavyoeleza. Pia najipa moyo kuwa kihistoria rais mwanayansi hana mambo ya kupindishapindisha. Rais wetu ni mwanasayansi. Naamini ataondoka muda ukifika. Hofu yangu ni pale atakapokuja rais mwanasiasa au mwanajeshi!
 
[emoji1787][emoji1787] haya banah, ila sayansi yenyewe inakubaliana kuwa elements ni kiashiria cha jambo/kitu fulani ambacho kipo around the corner!.
 
JPM anaweza kuishi uraiani bila uraisi kweli? 'public relation' yake ni very poor sana ndani ya chama chake na nje yachama, kwa matajiri na wanyonge kwa wasomi na wasio wasomi sera zake zimegusa kila aina yawatu.....kuna watu wamepoteza muelekeo wa maisha kimzaha mzaha wengine wamekufa kwa stress za maisha biashara za watu zimefunga bila sababu.....unadhani hao watu wote watamsamehe? kunyantuka kwake inaweza ikawa 'turning point' ya siasa za Tz.....lazima katiba itaguswa kinga ya maraisi iondolewe

Hakuna kitu kinaitwa kinga ni busara tu za atakaekuwepo kupitia Sheria hio hio still MTU anaweza akalimia meno vizuri tu.Matumizi mabaya ya Madaraka, kutokufuata katiba, matumizi mabaya ya fedha za umma,uhujumu uchumi, upotevu wa watu,nk labda asitokee kichaa tu.
 
Katiba ya nchi ni miaka mitano mitano,mshauri basi mwakani aachie,kwasababu hata yeye alishasema kazi hiyo ni ngumu,basi mwakani ni wakati mzuri kuachia
aache then achukue nani? maana kule upinzani hawana mtu hadi atoke CCM na kwa mapokea ya CCM lazima amalize mihula miwili
 
Rais Magufuli anajitambua sana hawezi kufanya hivyo. Rais hana chake binafsi anachojipangia, bali anatekeleza ilani ya chama na serikali kama alivyojinadi wakati wa kampeni. Pia anasimamia misingi ya katiba kwa uwaminifu kabisa. Usijali, muda ukifika ataondoka kwa mujibu wa katiba.
Kwa mawazo yangu, kiongozi habakii madarakani baada ya muda kwa matakwa yake, bali kwa matakwa ya kikundi kinachonufaika na uwepo wake hapo madarakani. Raisi kama raisi peke yake hana huo ubavu.
 
Back
Top Bottom