Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,890
Kuanzia mwaka Jana yule Mungu wa maajabu , Mungu wa kutumainiwa na watoa vilio aliamua kupiga kambi rasmi hapa nyumbani kwetu Afrika Mashariki na hasa Kenya na Tanzania .Najua sababu ni wetu wetu kuishia makanisani kuishi kwa kumuomba na kulia kulia bila ya kuwaza ubaya dhidi ya viongozi bali tunasema Mungu waumbue siku moja .
Mambo yakaanza kwa Zitto kuleta hoja binafsi Fisadi Lowasa na Sitta na genge lao wakapinga na kumpa adhabu bwana Zitto na kumpa lawama lakini Mungu alikuwa kesha fika Tanzania akampa Zitto ujasiri na watanzania wakafunguliwa masikio wakasikia na macho yakaona wakakataa ujinga wa Lowasa, Sitta na genge la baadhi ya wabunge wa CCM wanafiki .
Wakajenga jungu wakamfukuza kijana na kula njama za kuzima hoja ya BOT ya Slaa wakaenda kwa Watanzania wakasema .Mungu akabariki na akaendelea kuwapa moyo Watanzania na nguvu .JK akapigwa na butwaa lakini ukweli ukamwingia .Tume 2 sasa yake ya madini na ya bunge juu ya Richmonduli .
Ghafla yakazuka kule Kenya ya kwao ambayo sisi tumekuwa tukiuapata lakini tunaimba tuna amani kumbe tuna njaa na uoga maana wanajeshi wetu , polisi na FFU huwa wanafurahi sana wakitumwa kawapigeni wenzenu.Kenya wakajaribu moto umewaka .Muda umeingiliana richmond report nje mambo yamewaka .Mungu amempa busara JK akasema isomwe hadharani .
Kule nyuma kila fedhuli aliyesimama na kuua sauti ya Watanzania yaani Zitto kutoka Bungeni akapatwa na mkasa kati yao wote ni mmoja alibaki salama .Kila mnafiki Mungu alimjibu hapa hapa .
Mamvi na Karamagi wakawa wamebaki wakidhani wataendelea lakini ujinga na fitina kwa watanzania na Zitto na hata upinzani sasa ukweli umewaondoa .Kwa njia ile ile waliyo muondoa Zitto na kutufanya tufe kwa umasikini huku wanaiba na kutumia mabavu leo hawako tena pale walipokuwa wanaringia na kutesea .Nasema kweli kila muosha maiti ataoshwa na sasa hawa wamesha oshwa .