Jiji la Dar es Salaam ndio nguzo kuu kwenye kufanikiwa, vijana kimbilieni huko

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Hapa nazungumzia nyanja za mafanikio kwa sisi wasakatonge, nimezaliwa Moshi-kilimanjaro nimezunguka pande Nyingi za Tanzania Lakini dar-es salaam ndio Kila kitu kwa mtu ambae ana chachu ya mafanikio.

MWANZA
Ukienda Mwanza na hakika asilimia 100% utashindwa kujua uanzie wapi umalize wapi, labda uchague kua machinga na shida ya kua machinga ni bidhaa kutoka, unaweza kupigwa doro kuanzia asubuhi mpaka jioni mpaka utamani kurudi Kijijini kitu ambayo uwezi kuikuta dar Maeneo kama buhongwa, igoma ndio wamejaa machinga na wengi wao ni mwendo wa doro, useme ufungue labda frame kupata katikati ya Jiji ni ngumu huwezi kupata kama una mtaji mdogo. (Usisahau wasukuma wanauza kwa madawa)..kwahiyo na conclude kwa kusema Mwanza sio sehemu nzuri kwa anaeanza kutafuta maisha. Labda ufanye kuzunguka minadani kupeleka bidhaa pande za Magu na kwimba.

MOROGORO.
Ni sehemu nzuri ya kuishi sio kutafuta Hela itakuchukua miaka mingi kuanza Kuona mafanikio, Huu mji ni kama njia ya kwenda dar watu hakuna kabisa, wafanyabiashara wa jumla kutoka pembezoni mfano ifakara, kilombero wakifata mzigo ni moja kwa moja dar, kwa sababu ya ukaribu kijana usijichanganye kwenda Morogoro kuanza kutoka chini.

ARUSHA
Huku na penyewe mambo ni Yale Yale tu kwa msakatonge labda Uwe machinga kwa kumwaga chini "sendozi" za kina dada jioni mitaa ya mianzini Hapo au stand (jiandae kukimbizwa na migambo), frame uwezi kupata mjini Ukiwa na mtaji mdogo.

Kwanini nasema dar es salaam ndio Kila kitu? Fanya wepesi uje mjini, dar es salaam chochote unauza ukipata location nzuri, Kuna watu waliofanikiwa kwa umachinga wakiwa manzese,ilala mbagala,mbezi,chanika, mbande,kigamboni n.k unaweza usifanye mishe zako kariakoo na Bado ukatoboa, ni kwa sababu muingiliano ni mkubwa.

....nilikua nanunua viatu vya wadada kariakoo namwaga pale manzese nauza kuanzia asubuhi mpaka usiku saa 4, guess nitakua nimekusanya shingapi? Mtaji nilioaanza nao ni kama laki 7 Lakini progress unaiona na mtaji unakua, je huko Kigoma, Mpanda, Bariadi unaweza kumwaga viatu barabarani na usiuze hata kimoja.

Nilifanya harakati za viatu hapo karume nachukua viatu ndani kwa jumla namwaga nje, ndani ya mwezi nikawa na pointer wengi sana Pamoja na wafanyabiashara wa jumla kutoka mikoani huko naanza kuuza saa 11 usiku kufika saa 2 asubuhi jamaa zangu wa gairo nawahesabia mzigo wote tunapatana nachukua changu, hivi nitajie mkoa gani hii inafanyika? Labda Hapo Soko la mtumba memorial Moshi tena kwa kiwango kidogo.

Nimefanya harakati Nyingi sana hapo na Kila harakati niliofanya ilinilipa, mpaka nikaondoka Jiji ilo. Mikoani Huku mzunguko hamna, pesa ni ngumu, ukifungua harakati wachawi ni wengi sana, Sasa kijana unakaa Kigoma, Mpanda Katavi, Babati, Njombe, Shinyanga na unaridhika kabisa?

Sasa hivi Niko vijijini huku na mtaji Sasa Lakini Cha kufanya sikioni naona kama nitazika pesa.

Tokeni huko nendeni kwenye Jiji lenye pesa nyingi.
 
Kungekua hakuna mzunguko wa biashara hao watu wa mikoani ungewaona huko kuja kuchukua bidhaa?

Akili yako na juhudi zako za kupambana ndio zitakazofanya utoboe kwenye haya maisha
Umesema ukweli mkuu, lakini ujue hao wanaokuja dar kuchukua mzigo ni ma-tycoon wa ilo eneo husika tofauti na dar hata Ukiwa na million 5 ni kama huna Hela tu.
 
Maisha popote penye riziki mkuu, mi Kuna sehemu npo mwaka wa 2 huu yaani nahisi kama nilichelewa kupajua yaani siwezi kwenda popote hata uniambie wapi

Hapa nimejipa likizo ijumaa narudi huko, na hakuna hata network ya internet huko, lazima ndo pananiweka mjini na napakubali kinoma
 
Maisha popote penye riziki mkuu, mi Kuna sehemu npo mwaka wa 2 huu yaani nahisi kama nilichelewa kupajua yaani siwezi kwenda popote hata uniambie wapi

Hapa nimejipa likizo ijumaa narudi huko, na hakuna hata network ya internet huko, lazima ndo pananiweka mjini na napakubali kinoma
Hapana jina au unaogopa kurogwa?
 
Back
Top Bottom