Narudi CCM

Narudi CCM

S
jamani mpaka sasa sijaona tofauti ya cdm zaidi ya ujinga tu na sera zisizo na tija najuta kuwapa kura yangu narudi ccm kuanzia leo

sasa mkuu kama hujaona tofauti ya cdm na ccm...ila umeona ujinga na sera zisizo na tija ..........sasa ccm unafata nini kama hivi vyama havina tofauti..........au umetumwa....cdm hutihitaji wa2 kama nyinyi.....
 
pole sana kumtia moyo kumwambia aondoke! maana huyu namfananisha na m2 anayetaka kunywa sumu than anatangazia ndugu nakunywa sumu ! ujue hanywi anabeep ! acha kutubeep . daima mwanajeshi harud nyuma akirud, ameikomboa nchi yake. wewe umekumbuka utumwa unarud kwa bwana zako! nenda kapige ngoma wenzio huku wenzio wakila kamwisho mwisho!
 
Nimechukua uamuzi wa kurejea chama tawala chama kubwa chama tawala CCM.

Lengo langu ni kupata ubunge hata wa kuteuliwa na jk au rais atakayekuwepo wakati huo.

OMBI
naomba mnisaidie mbinu za kutumia ili niupate huo ubunge mpaka uwaziri.
MWIGURU alitumia kashfa na matusi dhidi ya upinzani akapata!

JUMA NKAMIA alitumia matusi dhidi ya upinzani kama vile "siongei na mbwa"

Je,nitumie mbinu gani nimfurahishe rais aniteue?
 
Ladha ya sumu hutambuliwa kwa kuonja na si kuona
 
kwani wewe una mzazi kule kama ungekuwa naye ungepata chance kiulaini kama unakunywa maji mkuu all the best
 
sijajua ww jinsia yako, kama ni mvulana Shikilia ukuta ujae utapata tu...kama ww mwanamke wasiliana na mwigulu aku-igunga utapewa ubunge
 
Fanya hivi, nenda tawi lolote vunga umerudi CCM, (lazima watakupokea tu maana sasa wamefulia si kama enzi za Nyerere ambapo watu walisomea miezi kadhaa na kupewa mitihani ili wapokelewe!), hakikisha mavazi yako yote unamechisha yaani kuanzia soksi kijani, viatu kijani, tai kijani, shati hata kitambaa cha kufutia jasho kiwe kijani (potelea mbali ukionekana kama mwanasesere; the end will justify the means maana utawakuta wengi tu kama wewe, tumbo CCM, roho upinzani!)
Njiani tembea ukiimbaimba "CCM nambari wani na jenga tabia ya kuusifu ujinga woote wa CCM.
Mwisho jifunze ujangili wa kuua tembo, faru, nyati na kuuza "unga" maana ndiyo pasipoti ya iukaa meza moja hata na rais.
Ukishafika hatua hiyo hata ukigombea ukakataliwa "Rahisi" atakutunuku hata u-DC au u- RC. Ukiwa na bahati utaukwaa ule wa kuteuliwa. Upo Mkuu?
 
Nitajaribu ila neno "mwanasesere"limenitisha! Mpaka nivae kijani tena!kazi kweli.
 
mkuu kwani ulipokuwa unahama ccm ulituomba ushauri?
 
OMBI
naomba mnisaidie mbinu za kutumia ili niupate huo ubunge mpaka uwaziri.
MWIGURU alitumia kashfa na matusi dhidi ya upinzani akapata!

JUMA NKAMIA alitumia matusi dhidi ya upinzani kama vile "siongei na mbwa"

Je,nitumie mbinu gani nimfurahishe rais aniteue?

Hata walimu wa shule za yebo yebo hawaulizi maswali baada ya kutoa majibu
 
Nisifiche hisia zangu na enyi wapinzani mtanimehe kwani tokea Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani nimekuwa nikijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kutafuta tu mabaya au madhaifu yake hasa ya kiuongozi na kiutawala lakini nasikitika tena kwa uchungu mkubwa sana kusema kuwa sijaona baya lolote sana sana naona tu Rais Dkt. Magufuli anayafanya yale ambayo nahisi hata Mtu ambaye nilikuwa naandamana nae huku tukizungusha mikono kama matairi ya magari asingeweza hata kuthubutu kuyafanya.

Hivyo basi nimeamua rasmi kuwa kuanzia leo hii natangaza rasmi kuachana na huku upinzani nilipo na narudi CCM kwani naona kama vile pengine nilirogwa kipindi kile na mimi nikaongozana na waliotushawishi kwenda upinzani.

Mwisho kabisa nitoe tu rai yangu kuwa kwakuwa Rais JPM kupitia ilani ya chama chake cha CCM sasa wanayafanya yale ambayo sisi upinzani tulikuwa tukiyasisitiza naomba tu hivi vyama vyote vya upinzani tuvivunje tu na wote mfuate nyayo zangu na turudi kuungana na CCM ili kusiwe kabisa na upinzani kwani ninachokiona sasa huku upinzani nilipokuwa badala ya kuendeleza siasa sasa tunaendeleza tu majungu, uwongo, fitna na propaganda ambazo naona hazina tija.

Samahani kwa wale wazungusha mikono wenzangu kwa huu uamuzi wangu na mnivumilie tu ila narudi kwenye chama kilichopata kibali cha Mwenyezi Mungu cha CCM na kinachoongozwa vyema na Mchunga Kondoo mwenye upako wa kiroho na imani kamili Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Asanteni.

Wenu mzungusha mikono maarufu
Dar es Salaam
Tanzania.
Pia akili yako ni ndogo kuona tofauti!
 
Tangu lini ulikuwa chadema wewe popoma au unafikiri hatujui ile id nyingine ya kipopoma unayotumia kuingilia humu.
 
Kuna kamsemo ka kizungu huwa wanasema "if you can't fight them join them....!! Hapa ujanja ni kuwa mahala pa uhakika kukomaa na Upinzani ni kupoteza mda na future wajanja wote ni kufanya shughuli binafisi ukisubilia kila kitu ifanye Serikali utaramba chuma cha Reli......!! Zinduka kijana acha Unyumbu na Ujuha siku hazigandi.......
 
# wajanja wote ni kufanya shughuli binafisi ukisubilia kila kitu ifanye Serikali utaramba chuma cha Reli......!!#

Hongera kwa kulitambua hilo mpendwa
 
Kuna kamsemo ka kizungu huwa wanasema "if you can't fight them join them....!! Hapa ujanja ni kuwa mahala pa uhakika kukomaa na Upinzani ni kupoteza mda na future wajanja wote ni kufanya shughuli binafisi ukisubilia kila kitu ifanye Serikali utaramba chuma cha Reli......!! Zinduka kijana acha Unyumbu na Ujuha siku hazigandi.......
Maneno yako yamejaa ubinafsi, wahi CCM unaweza kuambulia uDED si umesikia kuna waliogoma kuripoti!
 
Back
Top Bottom