Nichumu Nibebike
JF-Expert Member
- Aug 28, 2016
- 8,658
- 15,814
Miaka ya 2012 niliwahi kwenda kulipia bili ya maji pale Kimara mwisho. Ile niko kituoni nangojea daladala akawepo binti mmoja mrembo matata! Mateja wapiga debe wanamtolea macho na wameacha kupiga debe! Mi mwenyewe nikakosa cha kuongea nabaki namchek tu dogo. Ikaja dala dala tukapanda naye. Mie nilikuwa nashukia Ubungo ila ikanilazimu nipitilize mpaka Magomeni. Alivyoshuka sijui alishuka wapi hata sikumuona tena nikabaki najilaumu kwa kuzembea.