IGWE
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 9,463
- 7,385
...good.Nichukue nafasi hii kuwashukuru nyote katika changamoto yangu ngumu sana nayopitia.
Wako baadhi wamenifata inbox na kunisaidia kwa chochote kile walichonacho nawashukuru sana.
Wako pia ambao wamenitia moyo na kunishauri mawazo mazuri nao pia nawashukuru.
Naami wako ambao hata kama hatukuwasiliana nao lkn baada ya kuliona hili huko waliko kwa namna moja ama nyingine wakaguswa na kuniombea kheri nao pia nawashukuru sana.
Wako ambao tumebahatika kuonana nao ana kwa ana na kufahamiana pia nawashukuru.
Kwa pamoja Mungu awabariki sana.
Sikuwa na pesa ya kumpeleka hata mke wangu hospital lakin kupitia walionichangia siku ya jana nilimpeleka na alipata vipimo na matibabu na sasa anaendelea vzr, kwa hilo nawashukuruni sana.
Ingawa bado naendelea kupambana na mengine ya kutoka kwenda kutafuta vibarua ili sasa kupata chochote kwaajili ya familia kula, huku afya ya mke wangu ikiwa inaendelea vzr, naamin haya yote kwa uweza wa Mungu ntayavuka.
Wako watu wamekuwa wakinishauri kuweka no ya Simu hapa hapa kwa yeyote mwenye ushauri, kibarua huko aliko au hata chochote anachowiwa kusaidia ili iwe rahisi. Nimeona ni wazo zuri na mm naiweka hapa hiyo no ambayo tunaweza kuwasiliana. Ambayo ni: 0742843490. Inapatikana na tutawasiliana moja kwa moja.
...amani ya Mungu idumu kwako,idumu na kwa wengine/kwetu pia.