Napitia katika changamoto kubwa

Napitia katika changamoto kubwa

Asipokuelewa hapa basi, hasa hiyo namba 4 na 6.

Maandiko yanasema " Mungu hujibu kwa wakati wake (sio wako).

Waswahili wanasema "Ukiona kiza totoro ujue ndo kumekaribia kukucha".

Hakika umemshauri vyema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumuombee Mungu apate macho na akili ya kutafakari comments za wakuu hapa na kuzifanyia kazi.vinginevyo atakuja kuomba ushauri akiwa analia
 
Vumilia dada, upo.sahihi kabisa, Mungu hujibu.kwa wakati wake muafaka, endelea na maombi na kujitunza, utakapozaa jua umejiharibia bahati ya mume maana kuoa mwanamke.mwenye mtoto wa kidume mwingine wanaume wengi tunalikwepa hilo maana nikuondoa amani ndani ya nyumba. We sali timiza.wajibu wako ktk kukuomba Mungu, naye Baba wetu wa mbinguni atakuletea mtu. Usiishi kwa kusikia maneno ya watu maana ukizaa hujaolewa hao hao wataanza kusema kazalishwa bila hata ndoa, maneno ya watu ni sumu dada, watu wamejaa unafiki. Msikikize Mungu wako na sio wanadamu. Mbona kazi nzuri kakupa, tena yenye mshahara mzuri ambayo hukutegemea, iweje imani yako ishuke katika hili la pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dada angu pole Kwa kinachokusumbua. Jambo hili limekuwa common Sana Kwa wanawake ambao wenye fikra kama zako . Wengi huona umri unaenda na huchoka kuvumilia na kinachotokea ni kujirahisi Kwa mtu yeyote ambae hata hamjui. tatizo ndpo linapoanzia kila kitu hubadilika na kujikuta hata mwenendo wa maisha hubadilika pia. Malaz huchukua nafas yake, mbaya Sana kukata tamaa cha kufanya hapo usikate tamaa, na maamuzi yeyote unapotaka kuyachukua fikiria faida na hasara. Kinachokutesa wewe saiv ni hofu ya kuwa na umri mkubwa bila ya kuwa na mme,bila ya kuwa na mtoto .jaribu kuishinda hyo hofu. Ucijar kuwa na umri mkubwa pasipo kuwa na mtoto/watoto.amini kuwa mda bado na jione kama ndo Kwanza una miaka 22. Uciruhusu hofu hyo ikatawala nafsi yako itakufanya ikosee mwishoni wakat karbu unashinda

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante ndugu yangu. Maana nikikaa mwenyewe najiona kama niko mkosefu. Angalau niliona nisemee huku ili la moyoni linitoke niweze kufanya kazi vizuri. Kunachangamoto unapita nazo mpaka unaona dunia umeibeba.
 
Habari za jumapili wana jamii.
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa. Napitia katika changamoto kubwa sana.
Hapo mwanzo kipindi ninasoma niliona si vyema kujiingiza katika mahusiano ya kufanya mapenzi kwani niliona yatanivuruga na ningejikuta napitia katika mahusiano mengi kitu ambacho sijawahi kukipanga maishani.
Nikamaliza chuo vizuri namshukuru Mungu.katika kutafuta ilikuwa ngumu kidogo nilitafuta mpaka nikakata tamaa nikaomba Mungu mpaka nikaona inatosha. Katikati ya kukata tamaa nikamuomba Mungu basi anipe kitu kimoja kwanza mme au kazi. Ila la kazi ndio nililoliwekea msisitizo kwani kwa kipindi hicho familia yangu ilikuwa inapitia changamoto nyingi kwa hiyo nikaona kazi itanisaidia kupunguza changamoto ama la basi niolewe ili nipunguze mzigo kwa familia yangu.
Siku isiyotarajiwa nikaitwa interview na nikapata kazi nzuri ambayo sikuwahi hata kufikiria wala kuiwaza.
Nikashukuru Mungu na kuanza maisha mapya ya kazi na kusaidia familia yangu. Nikajikita kwenye kumuomba Mungu anijalie mme mwema atakayenifaa na kuongoza familia tutakayoipata katika misingi ya imani ta dini ya kikristo. Sikubagua kabila wala atakuwa mkirsto wa aina gani maadamu awe anaabudu jumapili maana mimi nilikuwa tiari kuhama katoliki ili tulee familia yetu tukiwa na muongozo wa dini moja.

Sikuwahi kudhani nitafikia huku maana mpaka sasa imekuwa ngumu kama ni Mungu hachelewi ama hawahi basi kwangu mimi kwa sasa imekuwa ni shida kubwa. Nimefunga novena nimesali sana mpaka naona nimeanza kuathilika nahili swala. Mwaka jana tarehe moja nikaona basi kama mme wangu hayupo nipate tu mwanamme nitakae zaa nae lakini awe mkirsto maana siko tiari kumtenga baba na mtoto wake hata kama hamhudumii, nikiamini kuwa uwezo wa kulea mwenyewe ninao hata kama watoto watakuwa zaidi ya mmoja niko tiari kupambana na maisha. Nikaona kwa sababu nitakuwa pekeangu nikaanza kuwekeza ili watoto wangu wanikute nimejiandaa. Na penyewe Mungu akaona wakati wangu bado.
Mwaka huu mwezi wa pili akatokea mme wa mtu kitu ambacho sijawahi hata fikiria kuwa kunasiku nitaangukia huko, Mwanzoni nilitaka tuzungumze mapema kabla hatujazoena sana matakwa yangu lakini akawa mtu wa kuona nampangia sheria mapema na kudai hizo mipango ninazotaka kupanga nae tukiwa hatujafika mbali ni mipango gani. Nikaona isiwe tabu.
Ikafika siku ya kukutana nikamwambia mimi sijawahi kabisa hakuamini na nikamwambia kama anajiamini aendelee ila ajue atakuwa na deni la kulipa, akatafakari akaona viatu ni vikubwa akaondoka.

Chenga zikaongezeka nikajiuliza ni nini shida, tukapanga tukutane ili tuone hatima ni nini kati yetu. Akaja na kudai yeye hayuko tiari kutoa bikira ya mtu asiye na mpango nae. nikamuelewa na nikaona yuko sahihi.Nikamuuliza wewe ulivyoanza ulitegemea mimi ni mti sina hisia za kufanya mapenzi akadai alijua anajihusisha na mapenzi ya kila mtu ana mtu wake hivyo wanakutana kulizishana tu. Akaniambia nahitaji nini hasa kwake nikamwambia kama ulishaona hisia zangu unadhani nahitaji nini? Niliona nisianze kutaja shida niliyonayo kwanza nimsikilize yeye ndio na mimi niseme ya kwangu. Yeye akadai aliona ni mahusiano ya kula na kuondoka. Akaniambia kama niko tiari ataweka sheria za kutuongoza za maandishi ili baadae tusijekupeana shida. Nikamwambia sheria zako utazoniwekea nitazifuata vilivyo japo najijua ninawivu lakini wewe ni mme wa mtu tiari nitavumilia. Akaja na sheria na mipango mingi sana asee.sheria nyingi nilivyotafakari nikaona nyingi zinamlenga mtoto ambaye mimi ndio ninayemhitaji zaidi. na yeye akaona labda ni mmoja tu wakati mimi nishajipangia wakunitosha kabisa. Kwa maelezo yake nikaona hayuko tiari kuwa na mtoto nje ya familia na nikitokea kumpata basi nitoe mimba ama atamchukua. Nilichoka viungo vyote. Akaniuliza unalolote nikamwambia nizungumze nini wakati sheria zimekuwa ngumu.

Haki ya Mungu yaani natamani siku zirudi nyuma nizunguke na wanaume kama wafanyavyo wengine. Hukukujitunza kwangu kunanifanya nilie kila siku na kuomba Mungu usiku kucha kisa nilimtunzia mtu bikira. Jamii inayonizunguka itanitia wazimu maana swali la unaolewa lini limenichosha kabisa. Basi kama siolewi hata mtoto tu ni shida kumpata.

Kwasasa ninashida na mtoto kuliko maelezo na niendako nadhani nitawehuka. Msaada wenu tafadhalini sana.

NB. Hapo mwanzo nilifunga novena kwa muda wa mwaka mmoja na kuomba na kukabidhi mwili wangu uwe kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye ndio atakayekuwa mme au baba wa watoto wangu. Ndio maana inaniwia vigumu kuingia mahusiano mbalimbali.
Ukikosa vyoote hata wa kukupa mtoto, ukifikia hatua ya nani akutoe bikra yako... Tafadhali nishirikishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hivi naona kama umri unaenda sana hivyo nahofia kukosa mtoto kabisa. Tatizo kubwa nililonalo ninapenda sana watoto na kwa sasa namhitaji kuliko ninavyoweza zungumza.
Et usubiri hadi 40 ndo uende leba ha ha haaa ushauri wangu sio lazima upate unaemtaka ingekua hivyo maisha yangekua mepesi kwa kila mtu

NAKUSHAURI

tafuta mwanaume asie jiweza umuweke ndani muishi wote akuzalishe tu
 
Usipanic life begins at 40 ukiacha desperation wako atakuja ila sasa hivi ikikurupuka utaumia atajitokea mhuni akulize. God's time is the best loh , hafu zawadi ya maisha ni muhimu kuliko huyo mume unayemlilia ukiona case za wanawake kuhangaika kuwatuliza waume kuanzia kanisani had kwa waganga ungetulia tu upate sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu yupo 32 unasema aendelee kutulia? Mungu hatoi wenza ila hukupa akili ya kumpata mwenza unaemtaka sasa Anza kutembelea sehemu zenye vijana unaowataka kama vyuoni, kwenye makambi ya ibada, kwenye viwanja vya soka, disco, semina za neno la Mungu nk.. Kisha jirahisishe Jifunze kutongoza mwanaume, jiongezee mvuto kisha tambua unachotaka hasa kisha kitafute kwa mbinu zote, hiyo bikra ikishakutoka ndo akili yako itafanya kazi zaidi. Ukiwa na hiyo bikra Kuna sehemu ya ubongo haifanyi kazi vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaishi kwa ajili ya watu??usiombe kulea watoto mwenyewe dear..unaona ni rahisi kwa kuwa bado hujawapata.

1.unataka watoto wako waje kuishi bila baba yao kisa wti umri unaenda??tafakari.

2.unataka wasome katika mazingira magumu?

3.unaonekana unataka kuwafurahisha watu.ishi maisha yako.

4.inaonekana unafanya maombi yako kwa malalamiko.ni kama unamlaumu Mungu kwanini akupi unalolihitaji.kama unafanya hivyo acha mara moja.

5.Unataka kuolewa au kupata watoto kwa sababu marafiki uliomaliza nao chuo au unaofanya nao kazi wana watoto au wameolewa.nakusisitiza ishi maisha yako wewe hayo unayoyalazimisha yawe wakati muda wake bado,,utakuja kulia jua likiwa linawaka na usiamini.

6.usithubutu kuzaa na mume wa mtu mpendwa.kabisa usithubutu utakuja kulia machozi ya damu.bora uzae na mwanaume ambae hajaanza kuwa na familia,familia yako ndo iwe ya kwanza.

Mume wa mtu utazaa nae lkni ikifika jioni huyoooo kwa mke wake anakuacha bado unamuhitaji.atakuwa anakuona kwa kificho kwa sababu anaipenda familia yake ya kwenye ndoa.

Muda wako utafika tu usiishi kwa kufuata maishi ya watu kuwa wewe.punguza haraka.ulishawahi kujiuliza kwanini ulimuomba Mungu akupe mume na kazi lakini akaamua kukupa kazi na sio mume na vyote uliviomba kwake?????shukuru kwa kila nyakati unayopitia hutoamini majibu yatakayotoka hapo.

Naomba niishie hapa.uwe na wikend njema mpedwa.[/QUOTE
Nawe pia my dear uwe na weekend njema. Angalau nikisoma kama hivi napata moyo wa kuendelea kumuamini Mungu kwamba siku yangu yaja.
 
Mtu yupo 32 unasema aendelee kutulia? Mungu hatoi wenza ila hukupa akili ya kumpata mwenza unaemtaka sasa Anza kutembelea sehemu zenye vijana unaowataka kama vyuoni, kwenye makambi ya ibada, kwenye viwanja vya soka, disco, semina za neno la Mungu nk.. Kisha jirahisishe Jifunze kutongoza mwanaume, jiongezee mvuto kisha tambua unachotaka hasa kisha kitafute kwa mbinu zote, hiyo bikra ikishakutoka ndo akili yako itafanya kazi zaidi. Ukiwa na hiyo bikra Kuna sehemu ya ubongo haifanyi kazi vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujue hyo 32 alivopanic atazoa had visivozoeleka kuna Dada namfahamu kashahangaika kote huko kila mahali hapati, sasa ndo asifurahie maisha, ifikr mahali Watanzania hasa wanawake wenzangu lazima maisha yaendelee, walioko huko ndani kwenye wa naishi kwenye mateso mume hatafutwi huja mwenyewe baada ya kuona vtu vitakavompendeza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N
kitu ambacho Mwenyezi Mungu hawezi kukifanya kwa binadamu ni kumnyima haki yake....siku yako ipo zidisha maombi tu

shida zikizidi sana neema inakaribia, kuna watu wanashida zaidi ya wewe still wanaamini siku yao ipo...mfano mimi

stay strong madam, kila la kheri...nitakuombea kwa siku ya leo
Nashukuru ndugu. Niombee mpendwa maana huwa inafikia mpaka akosa cha kuomba wakati wa kusali.
 
Back
Top Bottom