Napinga kuajiri kwa vigezo vya GPA.

Napinga kuajiri kwa vigezo vya GPA.

Jabman

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2016
Posts
1,005
Reaction score
1,339
Kama ilivyotangazwa kuwa wenye shahada wataajiriwa wenye GPAkuanzia 3.8 na kuendelea, ukweli napinga kwa sababu zifuatzo.
1.Grading inatofautiana chuo na chuo. MF: Vyuo vingine 75ni A wakati vingine ni B+.
2. Kuna vyuo wanafunzi wakifeli lecturer anawajibishwa hivyo lecturer hufanya fair ili alinde mkate wake wakati vyuo vinginel
kufaulisha sana lecturer anahojiwa
3. Hakuna syllabi zinazoelekeza. Kila chuo kinafundisha kitu kinachopenda kulingana na uwepo wa wakufunzi.
4. Kila chuo kinatunga mtihani wake kulingana na kilichofundisha.
5. Anayefundisha ndiye hutunga mtihani ndiye husahihisha na ndiye hutoa matokeo. Kama ulimkosea kidogo basis mwanafunzi umeliwa.

Kama serikali inataka kutumia kigezo hiki basi watkaoajiriwa in wachache hata walioajiriwa waondolewe wasio na 3.8. Naamini mawaziri wengi wataachia nafasi.
Naishauri serikali
1. Iweke viwango sawa vya ufaulu yaani grading.
2. I centralize mtihani. Yaani wahitimu wafanye mtihani mmoja wa taifa kwa vyuo vyote.
 
Kuna wengine wamewekeza kwenye kukariri madesa na mbinu za kujibu mitihani lakini ukimleta kwenye cognitive na analytical skills ni mtupu kabisa.Hili swala liangaliwe upya.
 
Lete reference sio kuweka maneno yako tu.... lete evidence tuchangie. La sivyo hatuna sababu ya kutoka povu wakati hatufahamu uliyoyaweka kama yana usahihi. Tutaamini vp? Tuletee ushahidi...period
 
Katibu utumishi
Ulimsikia wapi? Hebu weka ushahidi hapa! Hizo zilikuwa kelele za uvccm eti wanawananga BAVICHA utafikri wenyewe GPA zao nzuri! Kama iko hivyo basi serikali ianze uhakiki tena kuwaondoa walioajiriwa bila kutimiza kigezo hicho!
 
Kama ilivyotangazwa kuwa wenye shahada wataajiriwa wenye GPAkuanzia 3.8 na kuendelea, ukweli napinga kwa sababu zifuatzo.
1.Grading inatofautiana chuo na chuo. MF: Vyuo vingine 75ni A wakati vingine ni B+.
2. Kuna vyuo wanafunzi wakifeli lecturer anawajibishwa hivyo lecturer hufanya fair ili alinde mkate wake wakati vyuo vinginel
kufaulisha sana lecturer anahojiwa
3. Hakuna syllabi zinazoelekeza. Kila chuo kinafundisha kitu kinachopenda kulingana na uwepo wa wakufunzi.
4. Kila chuo kinatunga mtihani wake kulingana na kilichofundisha.
5. Anayefundisha ndiye hutunga mtihani ndiye husahihisha na ndiye hutoa matokeo. Kama ulimkosea kidogo basis mwanafunzi umeliwa.

Kama serikali inataka kutumia kigezo hiki basi watkaoajiriwa in wachache hata walioajiriwa waondolewe wasio na 3.8. Naamini mawaziri wengi wataachia nafasi.
Naishauri serikali
1. Iweke viwango sawa vya ufaulu yaani grading.
2. I centralize mtihani. Yaani wahitimu wafanye mtihani mmoja wa taifa kwa vyuo vyote.
Kwanza siamini kama hiyo taarifa ina ukweli wowote. Hata ingekuwa ni kweli, mimi pia napingana na matumizi ya kigezo cha GPA. Hata hivyo naona sababu ulizozitaja hazina mantiki hata kidogo. Nadhani ungepitia upya system za vyuo vikuu ili uelewe vizuri!
 
Zamani sana mimi niliajiliwa na UDSM kama TA kwa sababu nilimaliza na GPA kubwa sana darasani kwangu. Hiyo ilinikosesha mambo mengine kwani ilinilazimisha kuwa mwalimu wakati nilikuwa nataka kuwa mtaaalamu wa kufanya mambo niliyosomea kweli kweli, na ilibadilisha sana mwelekeo wangu kwani hadi leo bado ni mwalimu.

Hata hivyo vipimo vya GPA huwa ni katika level inayojulikana, kwa mfano UDSM wakati huo ilikuwa inatumia GPA kwa wahitimu wake tu, haikutumia GPA kwa wahitimu kutoka vyuo vingine kwa vile TA alikuwa ni lazima awe ni graduate wa UDSM mwenye Bachelors degree tu, vinginevyo Assistant Lecturer lazima awe na Masters degree ambayo ilikuwa haipimwi kwa GPA bali kutokana na interview ya candidate mwenyewe. Hata hapa ninapofundisha leo, tunapata wanafunzi wanaohama kutoka vyuo vingine na huwa tunachukua grade zao walizotoka nazo huko lakini hatuzitumii katika kukokotoa GPA kwa vile hiyo ni relative sana.

Waajiri wote huwa hawatumii GPA ila kama wanataka kupima wanafunzi wawili kutoka chuo kimoja waliosoma kozi moja ndipo wanapotumia GPA kama kigezo kimojawapo, lakini siyo final. Mwajiri anatakiwa aangalie ni nini mwombaji atasadia kampuni yake, si alichofanya shuleni.
 
Kwanza siamini kama hiyo taarifa ina ukweli wowote. Hata ingekuwa ni kweli, mimi pia napingana na matumizi ya kigezo cha GPA. Hata hivyo naona sababu ulizozitaja hazina mantiki hata kidogo. Nadhani ungepitia upya system za vyuo vikuu ili uelewe vizuri!
GPA siyo kipimo sahihi. Ni kipimo cha hovyo kabisa. Reason: Mazingira ya kupatikana hizo GPA ni tata na tofauti. Kila chuo kina grading yake. Mtoa GPA ana madaraka makubwa yasiyohakikiwa. 1.Anatunga mtihani.2.Anasahihisha mtihani.3.Anagawa marks. Hii ni hatari sana.NB: Vyuo vingine vinagawa GPA za juu kama njugu, bila kuzingatia quality.Utaratibu wa kuajili kwa GPA upo hasa kwa Lecturers na Assnt.Lecturers. Utaratibu huu unawatupa nje watu wengi ambao ni competent hata kama wana GPA ya chini.TCU lazima wafanye utafiti na kuja na mpango mwingine. Wasijifungie ofisini tu. Mtu mwenye PhD hahitaji kupimwa na GPA ya undergraduate. Kama hivyo basi kipimo iwe ni mtihani wa Form 4 au 6 ambao ulisahihishwa kwa haki na kwa usawa.
 
Huu ubaguzi unaopandikizwa awamu hii lazima ututokee puani. Zile mbwembwe Tanzania kisiwa cha amani zitafutika tu. Watoto wenu wanasoma Feza Schools, full computer, full laboratory, wanalala Osterbay halafu mnataka kulinganisha ufaulu wa GPA na sie watoto wetu wanaosoma TAWA Secondary ya kata ambapo google tunakuja kuijua chuo kikuu. Jamanijamani, Mungu anawaona.
 
Kama ilivyotangazwa kuwa wenye shahada wataajiriwa wenye GPAkuanzia 3.8 na kuendelea, ukweli napinga kwa sababu zifuatzo.
1.Grading inatofautiana chuo na chuo. MF: Vyuo vingine 75ni A wakati vingine ni B+.
2. Kuna vyuo wanafunzi wakifeli lecturer anawajibishwa hivyo lecturer hufanya fair ili alinde mkate wake wakati vyuo vinginel
kufaulisha sana lecturer anahojiwa
3. Hakuna syllabi zinazoelekeza. Kila chuo kinafundisha kitu kinachopenda kulingana na uwepo wa wakufunzi.
4. Kila chuo kinatunga mtihani wake kulingana na kilichofundisha.
5. Anayefundisha ndiye hutunga mtihani ndiye husahihisha na ndiye hutoa matokeo. Kama ulimkosea kidogo basis mwanafunzi umeliwa.

Kama serikali inataka kutumia kigezo hiki basi watkaoajiriwa in wachache hata walioajiriwa waondolewe wasio na 3.8. Naamini mawaziri wengi wataachia nafasi.
Naishauri serikali
1. Iweke viwango sawa vya ufaulu yaani grading.
2. I centralize mtihani. Yaani wahitimu wafanye mtihani mmoja wa taifa kwa vyuo vyote.
Sasa umeanzisha uzi mwingine wewe si ndo moma2k?
 
Back
Top Bottom