Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Ndugu zangu,
Usiku wa leo nimekosa kabisa usingizi kwa kuufikiri mstakabali wa nchi yangu chini ya chama filisi cha CCM. Msongo huu wa mawazo ulinifikisha mahali pa kujiridhisha kwamba chama hiki yafaa kifutwe nchini. Nina sababu moja au mbili kuu za kuwaza hivyo kama ifutavyo:
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilisajiriwa kama ni chama cha wakulima na wafanyakazi na katika bendera ya CCM kuna alama za jembe na nyundo kama uwakilishi wa wakulima na wafanyakazi. Lakini hivi sasa CCM imekiuka mkataba wake wa usajili kwa kuwatosa wakulima na wafanyakazi na kuamua kuwa chama cha kifamilia, cha wafanyabiashara, matajiri wakubwa, mafisadi, majangiri, wahujumu uchumi na majambazi. Wapo watakaoubishia mtazamo huu. Lakini napenda kuwapa vielelezo vifuatavyo:

- Muundo wa chama: Ni nani walioshika nafasi za juu za chama, nani ni wachangiaji wakubwa wa chama, ni kwa kiasi gani familia ya Kikwete na Makamba imeweka mizizi ndani ya chama? Baba mwenyekiti, mama mjumbe wa kamati kuu, mtoto mjumbe wa halmashauri kuu ya UVCC, mtoto ni mwenyekiti wa vijana chipukizi: Baba ni katibu mkuu wa chama, mtoto mshauri wa raisi na mgombea ubunge: Baba rais mstaafu, mtoto waziri. Hii ni mifano michache tu wapo wengi ndani ya CCM ambao utasikia historia zao zinaanzia kwa wazazi wao.
- Uendeshaji wa chama: Ni akina nani wenye sauti ya mwisho ndani ya CCM? Naamini hakuna atakayenibishia juu ya hili. Wahindi na wafanyabiashara wakubwa ndio wanaoiongoza CCM na nchi kwa ujumla. Hao ndo wanaopanga nani awe nani na wapi? Hao ndo ambao Rais alisema wakikamatwa kwa wizi wa fedha za EPA, na kupelekwa mahakamani nchi itayumba. Hao ndo mabosi na waajiri wa Kikwete na CCM kwa ujumla wake. Si wakulima na wafanyakazi tena. Kwa kuwa wakulima na wafanyakazi hawana tena nafasi ya kuhoji wala kudai haki yao kutoka katika chama kinachojiita ni cha kwao.
- Nafasi za uongozi: Ukifuatilia kwa umakini utagundua kwamba uongozi katika nafasi ya ubunge na udiwani, kwa kiasi kikubwa zimechukuliwa na watu maarufu, wenye pesa za kutosha kununua kura, huku wakulima na wafanyakazi wa kawaida wa serikali wenye kipato cha kawaida na wasio na uwezo wa kununua kura wakiambulia patupu. Sehemu kubwa ya wagombea kupitia CCM ni matajiri waliojijenga kiuchumi na wafanyabiashara wakubwa, wakulima na wafanyakazi hawana chao.
- Mwenyekiti wa CCM aliwakataa wafanyakazi kweupe alipowahutubia wazee wa Dar es salaam. Kwanza nauona huu kama ulimbukeni: wanaodai maslahi bora ni wafanyakazi, lakini wanaohutubiwa ni wazee wastaafu, kuna uhusiano gani hapo? Lakini kikubwa ni kwamba huyu mwenyekiti alisema wazi kwamba serikali yake haina uwezo wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi (ambao kiujumla ndio wanaochangia kuinua hali ya kilimo kutokana na kugawana kipato chao na wa kwao huko vijijini ambao ni wakulima). Wakati akikataa kuwatekelezea wafanyakazi mahitaji yao, alikuwa anajua kabisa kwamba ana msululu wa makampuni ambayo ameyasamehe kodi kwa miaka kadhaa ili yachume ambapo hayakupanda. Alikuwa anajua kabisa kwamba kuna meli ya Kinana inabeba magogo na pembe za ndovu kijangiri, alikuwa anajua kabisa kwamba kuna Rostam aziz ambaye amekalia mabilioni ya watz. Kwa hiyo aliwakataa wafanyakazi akawalinda wafanyabiashara, wageni, mafisadi, majangiri na majambazi wa uchumi wetu.
- Naamini pia kwamba CCM si chama cha wakulima na wafanyakazi kwa kuwa serikali ya CCM ndiyo ilishiriki katika kuviua viwanda vyote vilivyokuwa vinasindika mazao yetu ya kilmo, ndiyo iliyoua kiwanda cha mbolea, ndiyo hiyo iliyoingia mikataba mibovu ya kuimaliza nchi. Wakati CCM ikiingia mikataba ya TANGOLD, Meremeta, Deep Green, IPTL, RICHMOND na mingineyo ya hivyo, iliwashirikishaje wakulima na wafanyakazi? Wakati CCM inaidhinisha wizi wa mabilioni ya fedha EPA kuyapeleka kwa wafanyabiashara wakubwa nchini ilikumbuka kwamba kuna zaidi ya asilimia 60 ya watanzania wasiokuwa na ajira wala mitaji? Na iliwashirikishaje hawa wote ambao ndio wanachama wa CCM?