Napendekeza CCM ifutwe

Wakuu wangu na wanaJF wenzangu, mnazidi tu kunipa hasira! Nadhani maumivu ninayoyasikia moyoni ni makubwa sana!
Hivi kweli hatuwezi kuamka kwa pamoja kwenda vijijini kuwaeleza wadanganyika kuwa nchi hii ilishauzwa na Chama Cha mafisadi walishagawana mapato zamani?
Ni dhuluma ya aina gani kumnyima mtu elimu, afya, miundombinu baada ya miaka yooote hii ya uhuru halafu eti unakuja leo na "T-Shirt" ama "Kanga" na vijihela "Tsh. 5000" ati iliakuone wewe wa maana huku ukicheka cheka kirahisi tu!
Watu hawa ni wahalifu, wauaji! Nadhani tunatakiwa kuwaadhibu vikali sana ifikapo Octoba 31 mwaka huu! Nadhani Mungu ameanza kutulipia kwa kuanza kushughulika nao, wengine wanadondoka dondoka tu bila sababu hadi wanaanza jitihada za kulindwa na Mashetani!
 
Tuifute CCM wenyewe kwa kuinyima kura hapo 31.10.2010
Ni kwa kupitia kura za ukombozi tuu.
 
Wakuu wangu na wanaJF wenzangu, mnazidi tu kunipa hasira! Nadhani maumivu ninayoyasikia moyoni ni makubwa sana!
Hivi kweli hatuwezi kuamka kwa pamoja kwenda vijijini kuwaeleza wadanganyika kuwa nchi hii ilishauzwa na Chama Cha mafisadi walishagawana mapato zamani?
Ni dhuluma ya aina gani kumnyima mtu elimu, afya, miundombinu baada ya miaka yooote hii ya uhuru halafu eti unakuja leo na "T-Shirt" ama "Kanga" na vijihela "Tsh. 5000" ati iliakuone wewe wa maana huku ukicheka cheka kirahisi tu!
Watu hawa ni wahalifu, wauaji! Nadhani tunatakiwa kuwaadhibu vikali sana ifikapo Octoba 31 mwaka huu! Nadhani Mungu ameanza kutulipia kwa kuanza kushughulika nao, wengine wanadondoka dondoka tu bila sababu hadi wanaanza jitihada za kulindwa na Mashetani!
Kama mna kumbukumbu nzuri, kuna wakati mabalozi wa CCM walipita kila nyumba kuandikisha kadi za CCM na kadi za kupigia kura. Nasikia sasa hivi mabalozi wameagizwa kama siyo kufundishwa kwamba wawatishie wale wananchi walioandikwa majina kwamba majina yao yapo ikulu. Atakayeinyima kura CCM atakiona cha moto. So ndugu zangu tukawaelimishe wananchi kuhusu hili. Maana wengi wao hawalijui na wanaweza kuipigia CCM si kwa kuipenda bali kwa kuogopa.
 
Back
Top Bottom