Napenda maamuzi ya Raisi wa Urusi

Napenda maamuzi ya Raisi wa Urusi

But Russia is nothing without Putin
Kama unafuatilia habari vizuri jana mwakilisha wa Russia UN aliitisha kikao cha dharura cha baraza la Usalama la umoja wa mataifa kutoa ushahidi wa barua iliyotumwa kwa Putin kutoka kwa legitimate President wa Ukriane Viktor Yanukovchy kuomba msaada wa kijeshi ku stabilize hali ya kisiasa nchini mwake

Barua hiyo ipo kisheria zaidi ila tukirudi kimaslahi Putin hataki kuzungukwa na Pro-western nations

Anahofia siku ikilazimika vita kati ya West na Russia,Russia hatokuwa na first strike capabilities ya nuclear weapons

Na lengo la West as in NATO ni kuizunguka Russia proper with a missile defence shield.Kuiondolea uwezo wa kurudisha mapigo ikitokea vita ya makombora

Na kuna swala la Black sea fleet ya Russia iliyopo Sevastpol Crimea.Hiyo base ya Russia ndo pekee inayompa access mediterranean

Serikali mpya ya Kiev inayoendeshwa na Neo-Nazis iliyonyesha mwelekeo wa kuvunja mkataba wa Kharkov ambao unampa ruksa Russia kutumia bandari ya Sevestpol

Russia anajihami kwa kuivamia Crimea. Nchi yeyeyote ingefanya ambacho russia anafanya kma ingetupwa kwenye position hiyo

Mkuu hapa nimekupa big up,but Russia is nothing without Putin
Mark my word na ndo maana alipindua katiba ya Russia ili arudi tena kua raisi
 
mkuu
kulinda maslahi yake ni pamoja ya kuzuia Crimea isiifuate serikal mpya iliyoko Kiev.
Option waliyonayo Warusi ni kuifanya Crimea nchi, kuiongezea madaraka au kuiweka chini ya himaya yake

Na mwisho wa yote hapo Crimea kutakuwa na kura ya maoni ya kuamua kujitoa Ukraine kuwa nchi huru au irudi kuwa urusi,mimi naona ni sawa kabisa kwa urusi kufanya hayo,hawa NATO na US sio wakuwaamini nia yao wamdhoofishe urusi maana ndio wanamuona kabaki kikwazo kwao,
Maana China hana upande kinyonga yule
 
Mkuu napenda sana the way unavyojibu hoja zako tena kistaarabu tu
Mkuu wangu labda niulize tu swali moja
Ukrain ni nchi huru,kinachompeleka pale Russia hadi kuweka majeshi yake ni nini haswa??
Kwa nini anatumia mabavu kuweka rais anayemtaka yeye? Wakati wananchi hawamtaki??
Kama yeye ni super power kwa nini aogope UE na America?
Si awaache waingie ukrain zen awatufue???

Mkuu ahsante.

Ukraine ni moja ya nchi zlizokuwa USSR yaani kabla haujavunjika na kutokea Ukraine ya leo. Ina watu milioni 44 na ni nchi yenye jeshi kubwa sana barani Ulaya baada ya Russia.

Russia imepeleka majeshi yake pale Crimea kwasababu Russia na Ukraine wanachangia sehemu hio kwa kuwa na miundo mbinu ya kijeshi na kiusalama kama vile majengo maalum, viwanja vya ndege na bandari.

Huko nyuma kulikuwa na makubaliano maalum kati ya maraisi Yeltsin na Leonid Kravchuk wa Ukraine kwamba nchi hizo zinachangia Crimea hasa kwenye bahari nyeusi makubaliano yaitwayo "Black Sea Fleet".

Pia majasusi wa Russia waliona barua ambayo iliandikwa na kiongozi wa Crimea kwenda UN kudai kufunguliwa kwa ubalozi wa Marekani huko Crimea jambo ambalo liliwastua sana warusi.

Vita haiwezi kutokea ila ni kitu twaita "political ramblings in corridors of power" ambapo wababe kupigana vikumbo wakitafuta kujinafasi.

Lakini ni ukweli usopingika kwamba Russia haitakubali mchezo mchafu wa mabeberu kupenya kwenda Crimea.
 
Ni kweli kabisa, lakini Roman Abramovich bado ni mrusi na ana pasi mbili.

Huu ugomvi ukiangalia sana ulianzia na pale Russia iliposimama kidete kumteteta Bashad Al Asaad wa Syria na baada ya Marekani kushindwa kuipiga mabomu Syria wakawa wanatafuta njia zingine za kumtafuta Russia.

Sasa, Russia mpaka wakti huu kwa kupitia kampuni yake kubwa ya mafuta ya Gazprom kwa kusema ukweli ina utajiri mkubwa sana kutokana na kuzalisha mafuta na kuziuzia nchi nyingi tu za Ulaya na wateja wake wakubwa wakiwa Wajerumani.

Lakini wakati huohuo uchumi wa Marekani na nchi nyingi za Ulaya kwa sasa upo hoi na njia mojawapo ya kujitengeza upya kijiografia ni kutafuta baadhi ya sehemu kama hii ya Ukraine ambayo nayo ni nchi yenye mafuta.

Cha msingi ni kwamba Putin amesema leo kwamba kama watu wanafikiria vikwazo vya kiuchumi basi vitakuwa "Mutually Harmful" yaani kwa kila anaemtegemea mwenzake baina ya Russia na EU basi wote wataathirika ingawa sio Russia kwa sana.

Sio hayo tu, bomba la GAS litokalo Urusi kwenda kusambaza gas ulaya limepita Ukraine! Kwahiyo iwapo km wamaghalibi wataweza kuiteka Ukraine na kuwaongoza basi huenda maslahi ya Russia yakawa mashakani!
 
But Russia is nothing without Putin

Mkuu hapa nimekupa big up,but Russia is nothing without Putin
Mark my word na ndo maana alipindua katiba ya Russia ili arudi tena kua raisi

Mkuu,Putin is very smart.The fact kwamba alikuwa lieutenant colonel wa KGB na Director General wa FSB shows how much intelligent and strategic he is

Putin hakupindua katiba ya Russia.Katiba ya Russia inakataza ku serve zaidi ya two consercutive terms.Putin alichofanya ni equivalent ya move moja kweny chess inayoitwa "castling" yani queen na rook wana exchange positions

Putin na Dmitri Medvedv wali swap positions ingawa wote walikuwa wana nguvu sawa kipindi kile

Na kwa mtu kama Putin ashaanda plan of transition kama akiondoka madarakani.Usiwe na wasi Kremlin is in good hands
 
Wakuu nashukuru kwa michango yenu,na pia nashukuru kwa wale waliotoa matusi
Nashukuru mungu nina moyo wa uvumilivu kwan huwezi nitukania mke wangu kisa mambo ya Russia zidi ya Marekan na ulaya
Pili siku zote kwenye hoja lazima pawepo na mabishano na kila mwenye hoja kutiririka na kudadavua kama si kukakavua data
Tuache wenye nguvu waitwe power na sisi turudi kwenye kujadili mambo ya taifa letu
Am logging off mda wa kurudi home
Kwa wale wa mwanza tukutane viwanja bye!!!!!
 
Kama unafuatilia habari vizuri jana mwakilisha wa Russia UN aliitisha kikao cha dharura cha baraza la Usalama la umoja wa mataifa kutoa ushahidi wa barua iliyotumwa kwa Putin kutoka kwa legitimate President wa Ukriane Viktor Yanukovchy kuomba msaada wa kijeshi ku stabilize hali ya kisiasa nchini mwake

Barua hiyo ipo kisheria zaidi ila tukirudi kimaslahi Putin hataki kuzungukwa na Pro-western nations

Anahofia siku ikilazimika vita kati ya West na Russia,Russia hatokuwa na first strike capabilities ya nuclear weapons

Na lengo la West as in NATO ni kuizunguka Russia proper with a missile defence shield.Kuiondolea uwezo wa kurudisha mapigo ikitokea vita ya makombora

Na kuna swala la Black sea fleet ya Russia iliyopo Sevastpol Crimea.Hiyo base ya Russia ndo pekee inayompa access mediterranean

Serikali mpya ya Kiev inayoendeshwa na Neo-Nazis iliyonyesha mwelekeo wa kuvunja mkataba wa Kharkov ambao unampa ruksa Russia kutumia bandari ya Sevestpol

Russia anajihami kwa kuivamia Crimea. Nchi yeyeyote ingefanya ambacho russia anafanya kma ingetupwa kwenye position hiyo

Mkuu Uko sawa kabisa!

Russia alishafanya makosa kwa Iraq, na Libya. Ndio Maana hataki kabisa huo ujinga ujitokeze Syria na Iran na Ukraine na Poland!
 
Siku mkiujua ukweli hamtapoteza muda kujadili haya hapa!
 
somo linalopatikana sasa dunian ni kwamba ukiwa upande wa russia unakua salama zaidi kuliko upande wa marekani,kwamana hiyo urusi itarajie kupata washirika wengi kuliko marekani,
 
Napenda raisi wa rassia anavyojiamini sana..sio kama maraisi wengine wanaongopa Wamarekani...maana mmarekani anapenda sana kuingilia kati mambo ya Nchi zingine,kama walivyomuwekea Mseveni kukataa Ushoga

Rassia ni wapi? Kama una maanisha russia basi huyo ni punguwani kabisa
 
Richard LILONGO Ntuzu ... wakuu nashukuru sana kwa udadavuzi wenu.

Swali langu upi msimamo wa jeshi la Ukraine, hasa ukizingatia Urusi tayari wameshatia timu ja jeshi lao.?

Vipi na Wamagharibi nao wakiingiza jeshi lao wataendelea kukaa kimya.

Au wenyewe wanaamini diplomasia ndio itakayomaliza hili swala.

Je, Diplomasia ikishindikana wapo tayari kuangalia wakigeuzwa uwanja wa mapambano?
 
Last edited by a moderator:

Ki uhalisia hamna kiongozi yeyote wa western nations ambaye yupo tayari kuende vitani kwa ajili ya ukraine,its just not worth the risk of nuclear confrontation

Ukraine hawezi kufanya lolote maana bajeti ya jeshi la Urusi ni mara 18 zaidi ya jeshi la Ukraine.Pia Ukraine anajua aki declare war against Russia Putin atapata kisingizio cha kuikali Eastern Ukraine nzima na sio Crimea pekee yake. Miji ya viwanda kama Odessa na Donestk itakuwa nchini ya Russia na uchumi wa Ukraine utakufa

Hamna vita yeyote itakoyotokea hapa.

Sasa hivi The West wanmtisha Putin na economic sanctions. Kama hizo sanctions zikiwekwa tutegemee Urusi ku cutt off gas supply kwa most of Europe na ku flood market with US TREASURY IOUs kuvuruga uchumi wa dunia

Conclusion ni kwamba West watabaki kuongea tu na hawatofanya lolote la maana kuisumbua Russia
 
Kwa habari za hivi Karibuni jeshi la Ukraine limewekwa tayari Lkn kwa kazi ya kulinda maeneo muhimu tu na hasa kwenye vinu vya nyuklia! Jeshi la Ukraine halitoweza kupigana na Urusi! Na ukumbuke Kua mpk sasaiv jeshi la Urusi lote limewekwa tayari kuwapa backup ya kutosha Askari waliomo ndani ya Ukraine kwa chochote kile kitakachotokea!

Wamaghalibi hawawezi kuingiza jeshi kwa sasa na hawatofanya hivyo! Ila wanaweza kuyasapoti makundi ya wanaharakati na kuendeleza mapinduzi ya kirai km Misri na Tunisia! Kwahiyo serikali km itawekwa na Warusi basi itakabiliana sn na vuguvugu hilo!
 
Last edited by a moderator:
Ki uhalisia hamna kiongozi yeyote wa western nations ambaye yupo tayari kuende vitani kwa ajili ya ukraine,its just not worth the risk of nuclear confrontation

Ukraine hawezi kufanya lolote maana bajeti ya jeshi la Urusi ni mara 18 zaidi ya jeshi la Ukraine.Pia Ukraine anajua aki declare war against Russia Putin atapata kisingizio cha kuikali Eastern Ukraine nzima na sio Crimea pekee yake. Miji ya viwanda kama Odessa na Donestk itakuwa nchini ya Russia na uchumi wa Ukraine utakufa

Hamna vita yeyote itakoyotokea hapa.

Sasa hivi The West wanmtisha Putin na economic sanctions. Kama hizo sanctions zikiwekwa tutegemee Urusi ku cutt off gas supply kwa most of Europe na ku flood market with US TREASURY IOUs kuvuruga uchumi wa dunia

Conclusion ni kwamba West watabaki kuongea tu na hawatofanya lolote la maana kuisumbua Russia

Hili ni eneo lenye migogoro ya kikabila kwa mamia ya miaka mpaka sasa. Ilitegemewa kwamba Warusi hawataruhusu Cremea iwaponyoke kwasababu ingekua siyo kuipoteza Ukraine tu bali kuwaruhusu mahasimu wakee mpakani mwa Urusi!

Kuanguka kwa utawala wa pro Russia kule Kiev kumechelewa kwasababu Wamagharibi hawana uongozi madhubuti inapofika mambo makubwa kama haya. Na utawala wa Obama na Waamerika wengi wanauona mgogoro huo hauwahusu sana na ni mambo ya Ulaya!
 
Hapa ni mtifuano wa wakubwa wa Dunia na anaeumia hasa ni Watu wa Ukraine,hii Dunia imejaa unafiki sana nimemsikiliza John KERRY bila aibu wala haya anasema Russia anafanya mambo kizamani eti katika karne hii ya 21 kuvamia nchi ingne Kijeshi ni olda fashion!!!! anasahau hawa hawa Wamarekani wameua Ghadafi Juzi 2011, hivi sasa wanasaidia waasi Syria, wanasaidia waasi South Sudan, Wameua saddam kule iraq na afghan hivi ni karne ya ngapi ile?!!!

Tatizo US anajifanya jeuri na kakutana na kichaa Putin anashangaa,hivi Russia anakopa US?!! LINI na wapi??!!! eti umtishie nyau kama wanazotishia huku Afrika za misaada ya kishenzi??!! pale hawatavuka wamekutana na mbabe mwenzao watakaoumia na wale Maukraine ...
 
Richard LILONGO Ntuzu ... wakuu nashukuru sana kwa udadavuzi wenu.

Swali langu upi msimamo wa jeshi la Ukraine, hasa ukizingatia Urusi tayari wameshatia timu ja jeshi lao.?

Vipi na Wamagharibi nao wakiingiza jeshi lao wataendelea kukaa kimya.

Au wenyewe wanaamini diplomasia ndio itakayomaliza hili swala.

Je, Diplomasia ikishindikana wapo tayari kuangalia wakigeuzwa uwanja wa mapambano?

Nikija ktk maswali yako mawili ya Mwisho!

Msimamo Wa Putin Western counties wanaufahamu vzr kabisa kwamba ktk dipromasia kamwe hawatoweza kumlainisha Putin ktk msimamo wake juu ya maslahi ya Urusi Na usalama Wa Urusi kwa ujumla! Kwahiyo ktk Hilo western wanapiga kelele tu!

Dipromasia ata km itashindikana western hawatoweza kuingia kwenye Mapambano ya vita na Urusi! Njia ambazo wanataweza kutumia ni kuiwekea vikwazo Urusi! Na ktk Hilo nchi za ulaya zitaingia ktk matatizo makubwa hasa kwa nishati ya gas na mafuta!

Kwahiyo unaweza ukaona vikwazo havitokua dhana mujarabu ya kuiidhohofisha Urusi!

Tutegemee kuona western ktk hili swala Kua wapole!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom