mnyikungu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2009
- 1,963
- 2,479
Tena cha ajabu basi, Putin aliongea na raisi Obama jumamosi ilopita na akamweleza msimamo wake na pia mama Angela Merkel wa Ujerumani aliongea na Putin weekend ileile na wakaelewana.
Ujerumani inaingiza asilimia 40 ya gesi na asilimia 33 ya mafuta machafu kutoka Russia na jumuia ya Ulaya inafaidika kwa kiasi Fulani kwenye maeneo mengine kama ya usalama.
Kwahio kinachoweza kutokea ni kufikia makubaliano ya kuheshimiana kati ya serikali mpya kule Kiev na ile ya Putin kule Kremlin na kila mtu alinde maskahi yake lakini sio Russia kuondoka Crimea.
Na hio itafankiwa endapo utafanyika uchaguzi mkuu ambao Russia itapenda kuuratibu kama sio kuuangalia kwa makini.
na jamaa ndo hivyo wamegoma kabisa...hata waziri wao wa mambo ya nje kalieleza wazi hilo kuwa hawataondoka huko...bora lolote litokee lakini siyo kuondoka......kuna mbunge mwingine wa urusi alisema russia ilianzia ukraine hivyo hawako tiyari kuipoteza ukraine kwa namna yoyote ile