Napenda maamuzi ya Raisi wa Urusi

Napenda maamuzi ya Raisi wa Urusi

Mkuu kumbuka Roman ana uraia wa uk,so sidhan kwa upande wake kama kuna tatxo
But mkuu wangu haka ka ugomvi kati ya rais wa ukrain aliyetolewa na wananchi wake,america kachangua kwa kiasi kikubwa??

Ni kweli kabisa, lakini Roman Abramovich bado ni mrusi na ana pasi mbili.

Huu ugomvi ukiangalia sana ulianzia na pale Russia iliposimama kidete kumteteta Bashad Al Asaad wa Syria na baada ya Marekani kushindwa kuipiga mabomu Syria wakawa wanatafuta njia zingine za kumtafuta Russia.

Sasa, Russia mpaka wakti huu kwa kupitia kampuni yake kubwa ya mafuta ya Gazprom kwa kusema ukweli ina utajiri mkubwa sana kutokana na kuzalisha mafuta na kuziuzia nchi nyingi tu za Ulaya na wateja wake wakubwa wakiwa Wajerumani.

Lakini wakati huohuo uchumi wa Marekani na nchi nyingi za Ulaya kwa sasa upo hoi na njia mojawapo ya kujitengeza upya kijiografia ni kutafuta baadhi ya sehemu kama hii ya Ukraine ambayo nayo ni nchi yenye mafuta.

Cha msingi ni kwamba Putin amesema leo kwamba kama watu wanafikiria vikwazo vya kiuchumi basi vitakuwa "Mutually Harmful" yaani kwa kila anaemtegemea mwenzake baina ya Russia na EU basi wote wataathirika ingawa sio Russia kwa sana.
 
tatizo watu wengi hapa wanachangia bila kuwa na uelewa wa mgogoro huu wala hawajui historia ya ukrain zimetawala story za kufikirika tu, halafu kumbukeni kuna propaganda za vyombo vya habari vya magharibi vinaegemea upande mmoja
 
Hapa ndo umejibu hoja sasa na sio kumrukia mke wangu kana kwamba yeye ndo anayekujibu
Haya twende kwenye hoja sasa,kwa nini Russia kaivamia ukrain????

Putin anasema Rais aliyeondolewa madaraka wa Ukraine aliomba msaada wa kijeshi kwa Urusi pia wapo Crimea kuwalinda watu wenye asili ya Urusi hapo.
Lakini kiukweli nia ya Urusi ni kuitenganisha Crimea kutoka Ukraine
Refer to Moldova and Georgia history
 
tatizo watu wengi hapa wanachangia bila kuwa na uelewa wa mgogoro huu wala hawajui historia ya ukrain zimetawala story za kufikirika tu, halafu kumbukeni kuna propaganda za vyombo vya habari vya magharibi vinaegemea upande mmoja

Sasa mkuu, wewe waifahamu vipi historia ya Ukraine?
 
Mkuu kipi kimemfanya Putin kuingia ukrain wakati hawajamwomba kufanya hivyo?? Kipi anahofia???

Putin amefanya sehemu yake na Bado atazidi kufanya kwa ajili ya kujilinda na kulinda maslahi yake dhidi ya wamaghalibi!

Sasa km wamaghalibi na wao wanaweza wapeleke jeshi ili tufahamu kabisa Kua ni vita dhidi ya Russia Na Wamaghalibi!
 
sababu zilizompeleka ukraine ni za kiuchumi na kiusalama

Sasa iweje aende sehemu ambayo sio yake?
Hv wewe leo hii mtu aje kwako na kutaka kumchukua mkeo majiran zako hawatakusaidia??
Putin anaweza kua yuko sahihi kabisa maana kaona kabisa marekani wakiingia pale ukrain usalama wake utakua matatani
Mbili ukrain lazima angejiunga na NATO ambapo Putin na serikali yake hataki??
Swali kwa nini alazimishe wananchi wa ukrain wafate matakwa ya Putin wakati ile ni nchi huru
 
Mkuu kipi kimemfanya Putin kuingia ukrain wakati hawajamwomba kufanya hivyo?? Kipi anahofia???

Kama unafuatilia habari vizuri jana mwakilisha wa Russia UN aliitisha kikao cha dharura cha baraza la Usalama la umoja wa mataifa kutoa ushahidi wa barua iliyotumwa kwa Putin kutoka kwa legitimate President wa Ukriane Viktor Yanukovchy kuomba msaada wa kijeshi ku stabilize hali ya kisiasa nchini mwake

Barua hiyo ipo kisheria zaidi ila tukirudi kimaslahi Putin hataki kuzungukwa na Pro-western nations

Anahofia siku ikilazimika vita kati ya West na Russia,Russia hatokuwa na first strike capabilities ya nuclear weapons

Na lengo la West as in NATO ni kuizunguka Russia proper with a missile defence shield.Kuiondolea uwezo wa kurudisha mapigo ikitokea vita ya makombora

Na kuna swala la Black sea fleet ya Russia iliyopo Sevastpol Crimea.Hiyo base ya Russia ndo pekee inayompa access mediterranean

Serikali mpya ya Kiev inayoendeshwa na Neo-Nazis iliyonyesha mwelekeo wa kuvunja mkataba wa Kharkov ambao unampa ruksa Russia kutumia bandari ya Sevestpol

Russia anajihami kwa kuivamia Crimea. Nchi yeyeyote ingefanya ambacho russia anafanya kma ingetupwa kwenye position hiyo
 
Mkuu kipi kimemfanya Putin kuingia ukrain wakati hawajamwomba kufanya hivyo?? Kipi anahofia???

Analinda maslahi ya nchi yake hakuna kingine, kama alivyofanya Syria kuzuia assad kuondolewa,kwa sababu alijua Qatar walikuwa wanatafuta njia yakupitisha bomba za gas kwenda ulaya, na hapa urusi Analinda maslahi yake hakuna zaidi
 
Ni kweli kabisa, lakini Roman Abramovich bado ni mrusi na ana pasi mbili.

Huu ugomvi ukiangalia sana ulianzia na pale Russia iliposimama kidete kumteteta Bashad Al Asaad wa Syria na baada ya Marekani kushindwa kuipiga mabomu Syria wakawa wanatafuta njia zingine za kumtafuta Russia.

Sasa, Russia mpaka wakti huu kwa kupitia kampuni yake kubwa ya mafuta ya Gazprom kwa kusema ukweli ina utajiri mkubwa sana kutokana na kuzalisha mafuta na kuziuzia nchi nyingi tu za Ulaya na wateja wake wakubwa wakiwa Wajerumani.

Lakini wakati huohuo uchumi wa Marekani na nchi nyingi za Ulaya kwa sasa upo hoi na njia mojawapo ya kujitengeza upya kijiografia ni kutafuta baadhi ya sehemu kama hii ya Ukraine ambayo nayo ni nchi yenye mafuta.

Cha msingi ni kwamba Putin amesema leo kwamba kama watu wanafikiria vikwazo vya kiuchumi basi vitakuwa "Mutually Harmful" yaani kwa kila anaemtegemea mwenzake baina ya Russia na EU basi wote wataathirika ingawa sio Russia kwa sana.

Mkuu napenda sana the way unavyojibu hoja zako tena kistaarabu tu
Mkuu wangu labda niulize tu swali moja
Ukrain ni nchi huru,kinachompeleka pale Russia hadi kuweka majeshi yake ni nini haswa??
Kwa nini anatumia mabavu kuweka rais anayemtaka yeye? Wakati wananchi hawamtaki??
Kama yeye ni super power kwa nini aogope UE na America?
Si awaache waingie ukrain zen awatufue???
 
Putin anasema Rais aliyeondolewa madaraka wa Ukraine aliomba msaada wa kijeshi kwa Urusi pia wapo Crimea kuwalinda watu wenye asili ya Urusi hapo.
Lakini kiukweli nia ya Urusi ni kuitenganisha Crimea kutoka Ukraine
Refer to Moldova and Georgia history

Kulikua na mada hapa ililetwa Na ndugu Elungata juu ya huu mgogoro!

Kwakifu ni kwamba Russia Si kwamba anataka kuigawa Ukraine! Russia anachofanya ni kulinda maslahi yake na kusogeza mbali kitisho cha wamaghalibi dhidi ya Russia km USA walivyotaka kujenga kituo kikubwa cha kijeshi pale Poland!
 
Last edited by a moderator:
Putin amefanya sehemu yake na Bado atazidi kufanya kwa ajili ya kujilinda na kulinda maslahi yake dhidi ya wamaghalibi!

Sasa km wamaghalibi na wao wanaweza wapeleke jeshi ili tufahamu kabisa Kua ni vita dhidi ya Russia Na Wamaghalibi!

Ntuzu Putin bado anamakosa
Kwa nini uingie kwenye ardhi ya mwenzako?? Kama yeye ni mbishi na anaweza kuhimili mikiki mikiki ya EU na MAREKANI si angewasubilia wafike zen awachape??
 
Sasa iweje aende sehemu ambayo sio yake?
Hv wewe leo hii mtu aje kwako na kutaka kumchukua mkeo majiran zako hawatakusaidia??
Putin anaweza kua yuko sahihi kabisa maana kaona kabisa marekani wakiingia pale ukrain usalama wake utakua matatani
Mbili ukrain lazima angejiunga na NATO ambapo Putin na serikali yake hataki??
Swali kwa nini alazimishe wananchi wa ukrain wafate matakwa ya Putin wakati ile ni nchi huru

ukiongea kuhusu wananchi basi unakuwa hujafuatilia....sehemu ambayo majeshi ya russia yapo inaitwa cremea...hapo cremea wakazi wake wengi ni wale wenye asili ya russia na wanaongea kirussia....hata vyombo vya habari wanavyosikiliza ni vya russia...hata yale maandamano yalikuwa ya pande mbili kati ya wanaotaka kuwa upande wa russia na ambao wanataka kuwa umoja wa ulaya.....ni kweli ile ni nchi huru lakini jua katika kulinda maslahi yako huwezi kujali kama ni nchi huru au la!.....kumbuka marekani imezivamia nchi huru ngapi? kavamia afghanistan na iraq hii yote kwa ajiri ya kulinda maslahi yake tu....kwanini leo urussi inapotaka kulinda maslahi yake jumuiya ya kimataifa inaihukumu tofauti? mbona hawakuwahi kuipigia kelele marekani...mbona hawakuwahi kuipigia kelele ufaransa ilipowasaidia waasi libya?....wanaitaka sana ukrane kwa maslahi yao ndo maana urusi hayuko tiyari kuliona hilo likitendeka
 
Na Mimi Nina maswali machache kwako? Kwanini USA ilimtoa Sadamu Hussein madaraka ingali Wairaq walikua wanamtaka?

Kwanini Gadafi alitolewa madarakani na USA wakati Asilimia ndogo tu ya Walibya ndo walikua hawamtaki?

Unayafahamu maslahi ya Urusi yaliyokua Libya? Au yako Syria? Au Ukraine? Au Iran? Au Iraq?

Russia Lazima ijilinde na kulinda maslahi yake!

Imeshajifunza mengi kutoka kwa unafiki Wa western kule Iraq, Libya, na kwenye baadhi ya nchi ambazo zilikua chini ya umoja Wa kisovieti!

Ndio Maana kwa Syria na Iran na Ukraine, Tunaona Putin anakua Wa kwanza kutumia nguvu Na kulinda maslahi!

Mkuu napenda sana the way unavyojibu hoja zako tena kistaarabu tu
Mkuu wangu labda niulize tu swali moja
Ukrain ni nchi huru,kinachompeleka pale Russia hadi kuweka majeshi yake ni nini haswa??
Kwa nini anatumia mabavu kuweka rais anayemtaka yeye? Wakati wananchi hawamtaki??
Kama yeye ni super power kwa nini aogope UE na America?
Si awaache waingie ukrain zen awatufue???
 
Ntuzu Putin bado anamakosa
Kwa nini uingie kwenye ardhi ya mwenzako?? Kama yeye ni mbishi na anaweza kuhimili mikiki mikiki ya EU na MAREKANI si angewasubilia wafike zen awachape??
awe na makosa asiwe na makosa...yeye anachotaka ni kuona maslahi yake yako salama muda wote
 
Kulikua na mada hapa ililetwa Na ndugu Elungata juu ya huu mgogoro!

Kwakifu ni kwamba Russia Si kwamba anataka kuigawa Ukraine! Russia anachofanya ni kulinda maslahi yake na kusogeza mbali kitisho cha wamaghalibi dhidi ya Russia km USA walivyotaka kujenga kituo kikubwa cha kijeshi pale Poland!

mkuu
kulinda maslahi yake ni pamoja ya kuzuia Crimea isiifuate serikal mpya iliyoko Kiev.
Option waliyonayo Warusi ni kuifanya Crimea nchi, kuiongezea madaraka au kuiweka chini ya himaya yake
 
Last edited by a moderator:
Ntuzu Putin bado anamakosa
Kwa nini uingie kwenye ardhi ya mwenzako?? Kama yeye ni mbishi na anaweza kuhimili mikiki mikiki ya EU na MAREKANI si angewasubilia wafike zen awachape??

Ktk mbinu za kijeshi, mwenzako akikuwahi kupeleka jeshi na dhana za kivita msatari Wa mbele Wa Mapambano anakua na nguvu na advantage ya kushinda vita!

Russia angeweza kuwasubiri waingie na angeweza kiwachapa, Lkn kaamua kuingia Yeye kwanza aone nani atawachapa? Na pia ameweka jeshi tayari kwa vita kuwasaidia Wa Askari ambao wako ndani ya Ukraine! Sasa Hapo Unafikiri hao western watafanya nini ?

Mrusi hana makosa kabisa yuko sawa! Kwani Siri iliyoko nyuma ya USA na Europe ni kuidhohofisha Russia kiuchumi na kijeshi ili waje wawe wanawaongoza!
 
Back
Top Bottom