Napenda maamuzi ya Raisi wa Urusi

Napenda maamuzi ya Raisi wa Urusi

Fakharu

Member
Joined
Nov 9, 2013
Posts
60
Reaction score
2
Napenda raisi wa rassia anavyojiamini sana..sio kama maraisi wengine wanaongopa Wamarekani...maana mmarekani anapenda sana kuingilia kati mambo ya Nchi zingine,kama walivyomuwekea Mseveni kukataa Ushoga
 
Unapenda maamuzi au unapenda kujiamini?

Kama kujiamini hata ma fashisti kina Mussolini na ma NAZI kina Hitler walijiamini.
 
wanaongopa ......???
Rassia..........??????
Mseveni..,.....??????
hebu rekebisha hapo kwanza
 
Hata Russia wanapenda kuingilia mambo ya nchi zingine, njoo na hoja nyingine jombaa
 
internet-memes-the-most-interesting-pm-in-the-world.jpg
 
Super Vladimir Putin!!! Kila Rais anayelipenda taifa lake ni vyema amsome huyu Rais!!! Na hakika Amerika hapa wanagwaya kabisa!!! Vita ya Amerika na Urusi ambayo ilibomoka kule U.S.S.R bado haijaisha hadi leo. Na kwa furaha ya Urusi Putin alirudi tena madarakani hasa katika kipingi hiki ambacho marekani inataka kuendelea kushikilia kidedea cha kuwa Rais wa Dunia!!! Kwa mantiki hii vita ya Syria, Uganda na kwingineko ni vita kwa interests za America versus Russia!!!
 
Napenda maamuzi pia kujiamini maana vyote hivyo vinatengemeana
 
Super Vladimir Putin!!! Kila Rais anayelipenda taifa lake ni vyema amsome huyu Rais!!! Na hakika Amerika hapa wanagwaya kabisa!!! Vita ya Amerika na Urusi ambayo ilibomoka kule U.S.S.R bado haijaisha hadi leo. Na kwa furaha ya Urusi Putin alirudi tena madarakani hasa katika kipingi hiki ambacho marekani inataka kuendelea kushikilia kidedea cha kuwa Rais wa Dunia!!! Kwa mantiki hii vita ya Syria, Uganda na kwingineko ni vita kwa interests za America versus Russia!!!

Sorry naomba unieleze japo kwa ufupi issue ya Ukraine na Russia ni nini hasa...
 
Mimi nafikiri Russia analinda maslahi yake pake Crimea na kila mtu anafahamu hilo. Crimea ni sehemu ya Warusi tokea mika ya 1600s na hio ndio historia.

Vladmir Putin ni jasusi na alikuwa mkuu wa KGB enzi za Boris Yetsin huku akiandaliwa kuwa kiongozi wa Russia tunayoiona leo.

Sidhani kama Putin atakuwa tayari kuona Russia inaipoteza Ukraine kwenda kwa nchi za magharibi huku wakigawa baadhi ya sehemu kama ilivotokea USSR ilipovunjika.

Lakini hii ya mahesabu ya Putin kutoa Conference na waandishi wa habari kabla John Kerry hajatua mjini Kiev ni msisitizo kwamba Russia sasa inalinda interests zake na hawana wasiwasi na interest za wengine.

Tumsubiri John Kerry atasemaje baadae leo.
 
Sorry naomba unieleze japo kwa ufupi issue ya Ukraine na Russia ni nini hasa...

pale RUSSIA anachofanya ni kujihami dhidi ya nchi za magaribi....Russia lazima iidhibiti ukraine kwa ajiri ya maslahi yake kiuchumi na kiusala...ukrane ndo nchi ambayo bomba la gesi la russia limepita kulelekea nchi za ulaya kama germany na nyingine..kwa hiyo ni lazima selikali yoyote ya ukraine iwe na maelewano mazuri na russia la sivyo russia hatafanya biashara...lakini pia russia inaona usalama wake upo hatarini kwasababu ukraine inataka kujiunga na NATO....kama ikifanikiwa kujiunga itakuwa ni hatari kubwa kwa russia....WARUSSIA wanalijua hili ndo maana wanatumiaga pesa na nguvu kuzicontrol tawala za ukraine....halafu pia russia ana vituo vya kijeshi ndani ya ukraine kikiwemo kile kikubwa kilichopo black sea ambako kuna kituo kikubwa cha kijeshi kiitwacho black see fleet chenye miaka zaidi ya 230 hivi...kwa hiyo wao wanaposema kuwa wanawalinda raia wenye asili ya russia si kweli ukweli ni kuwa wanajilinda wao na maslahi yao
 
Sorry naomba unieleze japo kwa ufupi issue ya Ukraine na Russia ni nini hasa...

From the horses' mouth below:

"Eastern Ukraine and the Crimea have closer ties to Russia, while Western Ukraine is more friendly with Europe. Many Eastern Ukrainians still speak Russian, and the 2010 presidential elections divided the country with Eastern Ukraine voting heavily in favor of pro-Russia Prime Minister Viktor Yanukovych. On Saturday, the Kremlin issued a statement that Russian President Vladimir Putin told U.S. President Barack Obama that Russia approved military action in Ukraine because it "reserves the right to defend its interests and the Russian-speaking people who live there."
Heaven on Earth, kuna a lot of secret movements (politically, economically, socially and security wise) ambazo Russia anatumia kwa Eastern Ulkraine na Crimea!!! Kwa mantiki hii hata chaguzi za Ulkraine Russia ina support ili kumpata Pro-Russia. Ni siri kubwa sana ngoja niyamaze nisije tumiwa polonium 210.
 
Mimi nafikiri Russia analinda maslahi yake pake Crimea na kila mtu anafahamu hilo. Crimea ni sehemu ya Warusi tokea mika ya 1600s na hio ndio historia.

Vladmir Putin ni jasusi na alikuwa mkuu wa KGB enzi za Boris Yetsin huku akiandaliwa kuwa kiongozi wa Russia tunayoiona leo.

Sidhani kama Putin atakuwa tayari kuona Russia inaipoteza Ukraine kwenda kwa nchi za magharibi huku wakigawa baadhi ya sehemu kama ilivotokea USSR ilipovunjika.

Lakini hii ya mahesabu ya Putin kutoa Conference na waandishi wa habari kabla John Kerry hajatua mjini Kiev ni msisitizo kwamba Russia sasa inalinda interests zake na hawana wasiwasi na interest za wengine.

Tumsubiri John Kerry atasemaje baadae leo.

Putin ni rais makini kuliko Obama na kundi lake; walitegemea ataruhusu Ukraine kuchafuke kama Syria ili magaidi wahamie mpakani kwake, never hawezi kuruhusu hilo. Kilichokuwa kinafuata pale ni raia wote wa mashariki wanaoongea kirusi kuwa flushed out na katika piga nikupige hiyo lazima ingekuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe; kwanini putin akaribishe adui na magaidi mlangoni kwake na wakimbizi kibaaao wakiwemo magaidi humohumo? Big up president of the universe
 
Mkuu you heat the nail!!! Nakuhakikishia hata warusi kumrudisha Putin si bure!! Jamaa ni kiboko, na kwa machafuko ya dunia kwa sasa kama si Putin basi ungekuta na Urusi hali ni tete. Jamaa unaambiwa kila mara yuko cool anatumia kichwa chake sawasawa, Si mtu wa YES MAN na marekani pale wanagwaya. Wakati wote yuko nchini mwake anapanga mipango na kutulia kutafakari utekelezaji na mafanikio. Putin ni tofauti kabisa na hawa mavasco da gama wetu kila siku kiguu na njia. Mara eti secretary wa mambo ya njee na bla bla!! Kwa Puti hakuna hilo na utamsikia amesafiri mara chache sana. Penye interest zake anapafahamu na ana act taratibu kabisa!!! Wamarekani na dunia hawakutegemea kabisa kuwa urusi ilishika hatamu immediately, tena kwa uandalizi makini kabisa na hata majeshi ya Ulkraine hawathubutu kufua dafu pale. Tatizo Marekani na washirika wake wanataka waone kuwa bila wao hakuna kinachowezekana, sasa Putin anawaambia yeye anaweza bila wao.
 
Putin ni rais makini kuliko Obama na kundi lake; walitegemea ataruhusu Ukraine kuchafuke kama Syria ili magaidi wahamie mpakani kwake, never hawezi kuruhusu hilo. Kilichokuwa kinafuata pale ni raia wote wa mashariki wanaoongea kirusi kuwa flushed out na katika piga nikupige hiyo lazima ingekuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe; kwanini putin akaribishe adui na magaidi mlangoni kwake na wakimbizi kibaaao wakiwemo magaidi humohumo? Big up president of the universe

Tena cha ajabu basi, Putin aliongea na raisi Obama jumamosi ilopita na akamweleza msimamo wake na pia mama Angela Merkel wa Ujerumani aliongea na Putin weekend ileile na wakaelewana.

Ujerumani inaingiza asilimia 40 ya gesi na asilimia 33 ya mafuta machafu kutoka Russia na jumuia ya Ulaya inafaidika kwa kiasi Fulani kwenye maeneo mengine kama ya usalama.

Kwahio kinachoweza kutokea ni kufikia makubaliano ya kuheshimiana kati ya serikali mpya kule Kiev na ile ya Putin kule Kremlin na kila mtu alinde maskahi yake lakini sio Russia kuondoka Crimea.

Na hio itafankiwa endapo utafanyika uchaguzi mkuu ambao Russia itapenda kuuratibu kama sio kuuangalia kwa makini.
 
Back
Top Bottom