Napenda kufahamu uhusiano uliopo kati ya Mnyamwezi na Mtusi ndani ya Tabora

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
Kwa sasa nipo mjini tabora ambapo kabila kubwa la hapa ni mnyamwezi ila ndani ya mnyamwezi kuna watu wanaoitwa watusi .

Lakini pia inasemekana asili ya mnyamwezi ametokea ndani ya mtusi yaani mtusi ndio amemtoa mnyamwezi .

Kwa wale wenyeji wa tabora na wazawa wa tabora napenda kufahamu uhusiano kati ya mnyamwezi na mtusii .

Na je ni kweli chimbuko la mnyamwezi limetokea ndani ya jamiii ya mtusi haya wale ndugu zangu wa sikonge,urambo, uyui,kaliuwaa,mabama,usoke,nzega,usinge isevyaa karibuni sana mtupe elimu

Uhusiano wa mnyamwezi na mtusi.
 
Kiongozi mbona inasemekana mnyamwezi asili yake ni mtusiiii
Mnyamwezi ni kabila kubwa sana ila watu huwa hawajui na ndio mkoa wa tabora ulikuwa mkubwa sana na hata baada ya,kupunguzwa bado ni mkubwa mpanda kigoma sumbawanga katavi inyonga zote zilikuwa,ni tabora lakini inasemekana hata msukuma ni chimbuko la mnyamwezi ila wawo wamelimeza kabila la kinyamwezi kutokana na shughuri zao za ufugaji hasa wanapotafuta malisho lazima wazaane sana hivyo basi ndani ya mnyamwezi kuna mkimbu mkonongo, mweli, dakama ,mgulu ,msukuma,msumbwa,mtusi
 
Hao ni badushi. Kuna aina mbili ya watusi waliopo mkoa wa Tabora. Wale waliokuja kabla ya ukoloni na wale waliokuja miaka ya 60 hadi 70 wanaitwa badushi. Hakuna uhusiano wowote japo wameoleana kwa kiasi kidogo
 
Sifahamu historia ya haya makabila mawili, ila kwa simple logic naona hii kitu haiwezekani!

Wanyamwezi ni kabila, watusi ni kabila. Kusema mnyamwezi ni mtusi ni sawa na kusema mkurya ni mchaga!

Nafikiri kilichotokea ni muingiliano wa kawaida kabisa wa kimakabila huko zamani hasa katika biashara au katika kutafuta maisha.

Inawezekana kabisa watusi wachache walihamia unyamwezini katika kutafuta maisha, wakaamua kua wakazi wa kudumu mwisho wa siku wakajichanganya na kuzaliana na wanyamwezi!

Hii sio kwa wanyamwezi pekee, watusi wamejichanganya sana hata usukumani, ukuryani na kwa makabila mengine mengi ya kanda ya ziwa.

Wapo watusi wakurya kama mkuu Gentamycene, waliotokana na kuchangamana kwa aina hiyo. Sasa huwezi kusema wakurya ni watusi, au watusi ni wakurya.

i think it's a cross breeding case!

I stand to be corrected!
 
umegonga palepale kwa Gentycine
 
umegonga palepale kwa Gentycine

Namkubali sana huyu tribe mate wangu!

Ukimuangalia kwa akili ya kawaida utaona ni mpuuzi flani tu, ila ukiangalia kwa makini utajua sio mtu wa kawaida.

Acha nisepe kabla hajafika!

Mnyamwezi ni kabila kubwa sana ila watu huwa hawajui na ndio mkoa wa tabora ulikuwa mkubwa sana na hata baada ya,kupunguzwa bado ni mkubwa mpanda kigoma sumbawanga katavi inyonga zote zilikuwa,ni tabora lakini inasemekana hata msukuma ni chimbuko la mnyamwezi ila wawo wamelimeza kabila la kinyamwezi kutokana na shughuri zao za ufugaji hasa wanapotafuta malisho lazima wazaane sana hivyo basi ndani ya mnyamwezi kuna mkimbu mkonongo, mweli, dakama ,mgulu ,msukuma,msumbwa,mtusi

Point of correction: Mimi Ni Mnyamwezi wa Ussoke. na nimelelewa kienyeji kabisa kwa maana ya kukaa na babu yangu askari kea. kifupi Mnyamwezi ni Taifa na sio kabila. Zamani taifa hili lilitwa Unyamwezi , au Bara Unyamwezi , ndani ya Unyamwezi kuna , Wayubhi, Wagalaganza, wanyanyembe, wayobha, wakimbu, wawele, wakonongo, wasubwa( hawa imigrants kutoka Rwanda) na wasenye ( wa Usinge) wagalla wa uyumbu, warambo wa Urambo. Wanyaweli ni waha na watusi wahamiaji waliopokelewa Unyamwezini toka miaka ya nyuma sana , hasa hawa watusi wamefika tabora kwa awamu mbili ya mwisho kabisa ni mwaka 1959 walikuja na mifugo yao wakipitia Kagera. hawa sisi hatuwaiti wanyamwezi japo wameoa na kuolewa na wanyamwezi na kutuambukiza muzimu ya Maswezi kiasili maswezi si mizumu ya kinyamwezi ila mix ya Utusi na unyamwezi kwa wanyamwezi asili kama mimi tunalijua hili
 
Duuuh kudadeki kumbe eeee ndioo maana nyie watu wa kanda ya Ziwa akili zenu na Matendo yenu zinaendana na wale Jamaa... Leo sasa ndioo nimejua kama mnaoleana na mnaishi nao na wanaoa kwenu tokea enzi za ukoloni kumbe nyie wakiii......! Samahani ila nawapenda lazima nifunge safari toka Dar nije nami niwaolee maana napenda Maumbo yenu
 
Watusi( bhadushi kwa kisukuma na kinyamwezi) ni wahamiaji toka Rwanda, wanyamwezi ni wabantu wenyeji wa tabora, Watusi wameoana na wasukuma na wanyamwezi pia, lakini sio kabila moja.
 
Hao ni badushi. Kuna aina mbili ya watusi waliopo mkoa wa Tabora. Wale waliokuja kabla ya ukoloni na wale waliokuja miaka ya 60 hadi 70 wanaitwa badushi. Hakuna uhusiano wowote japo wameoleana kwa kiasi kidogo
Ukoo vizuliii kiongoziii
 
Back
Top Bottom