Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,707
- 1,729
Naona kajivua gamba sasa humu JF.Kama kweli imetolewa na wewe ni Nape nakubaliana na kichwa cha habari kuwa si mzima na hakuna wa kukutibu. Upumbavu ni majaliwa
Naona kajivua gamba sasa humu JF.Kama kweli imetolewa na wewe ni Nape nakubaliana na kichwa cha habari kuwa si mzima na hakuna wa kukutibu. Upumbavu ni majaliwa
DR. SLAA NA KADI YA CCM, NA UNAFIKI WA WATETEZI *WAKE
Nikiri wazi kuwa pamoja na kuwa mimi ndie niliyeanzisha mjadala huu, namheshimu sana Dr. Slaa kama mtu mzima sana kwangu na ndo maana huwa namuita babu,lakini bila kumumunya maneno ana mchango katika demokrasia ya nchi yetu bila kujali ni chanya au ni hasi.
Wapo wanaodai hoja hii haina mashiko eti kwasababu hawaoni kama itabadili maisha ya watu masikini. Hawana makosa kusema haya kwasababu ndipo uwezo wao wa kufikiri walipoamua uishie. Lakini hebu fumbueni macho mtazame ukweli huu, moja ya tatizo kubwa la binadamu wengi na hasa viongozi ni kuwa wazuri sana wa kusema wasiyoyaamini wala kuyaishi ndo maana nchi nyingi masikini, rasilimali zake hazifaidishi walio wengi bali wachache sana,huku wakidai tufunge mkanda wakati wao wanaongeza ukubwa wa suti kwani zinawabana zilizopo.
Babu anatofauti gani na wanaohimiza watu kujikinga na ukimwi wakati wao hata kinga hawaijui? Wanahutubia mkutano wa kupinga rushwa mpaka mapovu yanawatoka wakishuka wao ndo wanaulizia rushwa tena kwa ukali mkubwa? Anatofauti gani na msimamizi wa hospitali anayehimiza watu wakatibiwe kwenye hospitali hiyo na huku yeye mwenyewe hana imani na tiba za pale matokeo yake hata homa tu anakwenda ng'ambo kuitibu? Huyu ndo mnataka awe kiongozi mkuu wa nchi yetu? Anasema asiyoyaamini na kuishi asiyoyasema??!!
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki CCM.
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa
Msumari huo,nape yupo vizuri cha msingi ni kujibu hoja je ingekiwa zitto ingekuwa vipi ? Na je kauli ya padr mzinifu kwamba kuwa na kadi ya ccm ni laana nayo mnasemaje ? Na je kuwaadaa wenzakevwarudishe kadi za ccm wakati yeye bado anaitunza siyo unafiki ?
Nape,
Kama ujinga unalewesha basi na wewe umeshalewa siku nyingi.
dunce ni ni nini?Sijaona hoja ya kujadili hapo.matusi,kejeli,ukosefu wa adabu kwa wakubwa,upuuzi mtupu.nape wewe ni dunce tena sana tu.
kweli nape wewe sio mzima. Sasa utafanyaje?
Ukisoma post hiyo siyo ya graduate wa masters mie nakataa kwa sababu zifuatazo:
Una lugha ya matusi,
Una lugha ya dharau,
Una chembe chembe za ubaguzi wa kiumri, na kidini,
Unajiona wewe ndio bora kuliko wengine.
Ningekuwa mimi ndo TCU ningekuvua digrii zako za kuchakachua
pia Lipumba na Nape ni muhimu wafanye.Naona kuandaliwe mjadala mkali, Slaa vs Nape kabla ya mwisho wa mwaka.
.......yaliyomfikisha kwenye kumuasi Mungu na kanisa achilia mbali familia yake yaani mke na watoto....
Watetezi wake hebu muulizeni Dr. Slaa alipoasi upadri nyumba ile ya utawa aliyokuwa akiishi kama padri aliondoka na funguo za ile nyumba au vifaa vingine vya upadri kwa madai kuwa ni kumbukumbu kuwa alikuwa padri wakati flani katika maisha yake? Tusikurupuke kumtetea tukadhani tunamsaidia ,kumsaidia kwa kweli ni kumwambia ukweli kuwa hapa babu umeteleza.....
yep mkuu, wakamdanganya na mzee wa watu aropoke masuala ya familia ya nyerere kule arumeru--- duh aibu tupu unapokuwa na kampeni manager low namna ile -- hamshindi uchaguzi hat mmoja.Matusi ya hawa jamaa ndo kilichomnyima SIOI kura arumeru mashariki, wapo juu kwa matusi hawa jamaa, kama Mwigulu, Mkapa, na wengine. Hivi kumbe maadili ya chama tawala yanaruhusu matusi? Nilikuwa sijui. Tunajua ni mkakati mlioupanga. Hivi nchi inaongozwa kwa mipasho? Da tutafika kweli. Ushauri wangu Kwa CHADEMA wasijibu chochote, atatulia tu, lakini pia tukumbuke ndo ajira yake, atakula wapi sasa, Hivi Katibu wa itikadi na uenezi, Haya matusi ndo itikadi? Na mipasho ndo uenezi? Poor Tanzania!!!! tunakwenda wapi?
Suala la imani, ndoa, mapenzi, ......... What the f.ck is this?
Hivi yule kijana wa mwenyekiti wako ni mtoto wa First Lady kweli? Mbona hauhoji hilo? Na kama ni umri Mangula ni Kijana? Serengeti boy eee? na kama ni upadre we unajua kanisa alilokuwa analihudumu wanasemaje? You are just like as...le:deadhorse: