Nape,
Ni ngumu sana kwa mtu kujadili hiki unachokiita mada. Kwa uhalisia hii siyo mada ni siasa majitaka.
Pamoja na kuwa katika kundi la watazamaji nashindwa kujiuzuia kujibu hoja zako kwasababu zifuatazo;
1. Unachotaka ni mjadala uendelee kwasababu tayari umeshaona matunda yake(Mjadala usio na tija na taifa)
2. Watanzani wafahamu kwanini sisi tumebaki kuwa nchi masikini duniani
3. Hatari inayolikabili taifa huko mbeleni kama hatutachukua hatua madhubuti.
Sikutegemea kijana wa umri na wadhifa kama wako ndani ya chama tawala ungeweza kujinasibu kuanzisha mjadala(ambao si mjadala) kwa hoja dhaifu hafifu na inayodhalilisha kama hii.
Kwasisi wengine unatuacha na maswali, je wale vijana walioshauriwa wachukue uongozi kwa kuwa ni wakati wao ndio hawa kweli? Hivi kuna watu tunaowategemea kutoa dira na mwelekeo wa taifa kweli!!
Nilitegemea ungekuwa umeanzisha mada zinazogonganisha vichwa juu ya hali ya nchi yetu na mustakabali wake leo na kwa vizazi vijavyo. Kwa bahati nzuri sana kwa wapotofu na ambayo ni mbaya sana kwa dunia hii hukufanya hivyo.
Ukisoma maandishi yako huwezi kumdanganya mtu kuwa unamheshimu Dr Slaa. Hakika umemvunjia heshima ikamilifu.
Dr Slaa kama mwanadamu mwingine ana maisha yake binafsi kama alivyokuwa mzee Nanuye.
Sijui utajisikia vipi leo watu wakijadili undani wa maisha ya Nnauye hadi mauti yanamfika! Fikiri hilo kwa makini.
Mifano unayotoa hailingani na elimu au hadhi yako.
Kama mtazamaji nimeshindwa kuelewa uhusiano wa funguo za Nyumba ya upadre na kadi.
Kama utakuwa na ufahamu kuna mzozo uliokuwepo kuhusu Mwalimu Nyerere na zawadi alizopewa zile za kitaifa na binafsi. Hakuna mzozo kuhusu umiliki wa funguo za Ikulu, lile gari la kwanza la TANU n.k.
Mfano wako ni hafifu sana na ninawasi wasi na ujana kama si uwezo wako kifikra.
Umebadili hoja na kukudai Dr Slaa si Mwanachama. Umesahau ulisema analipia kadi.
Baada ya wananchi kukuonyesha jinsi usivyoijua katiba ya chama unachoongoza, utaratibu wa nchi kuhusu uongozi na vyama vya siasa sasa unakuja na habari ya kukanusha. Tunazo kumbu kumbu na zikitolewa ni aibu kwa taifa si wewe.
Umezungumzia kuhusu uongo wa kisiasa wa Dr Slaa. Ingefaa uweke wazi madai hayo kwasababu yale tunayoyasikia hakunahata moja lililokanushwa na serikali inafanyia kazi. Mathalani orodha ya mafisadi 11, serikali ya chama chako imefikisha watu mahakamani. Hebu tueleze mengine ya uongo na uzushi hasa sisi watazamaji.
Umesema kuongoza ni kuonyesha njia na kiongozi asemaye fuateni maneno yangu na si matendo huyo hatufai kwa sasa.
Nakaubaliana na maneno yako matamu sana. Lakini Nape wewe umesimama katika kutenda unayoyasema?
Mbona hujatuonyesha njia ya kukabiliana na dhambi zilizotitia ndani ya chama na serikali ya chama chako?
Mbona hatujaona matendo ya maneno uliotuahidi kuhusu vita dhaidi ya ufisadi na kuvua watu magamba?
Je, siku tisini zinaisha lini ili tujue kuwa sasa upo katika matendo zaidi ya kauli?
Je, kuhamishia kodi za taifa Uswiss ndiko kuonyesha njia?
Je, kutoa na kupokea rushwa(Kikwete kasema) kulikokithiri ndani ya chama chako tawala(Sumaye)ndiko kuonyesha njia?
Endapo Dr Slaa ni mfano wa viongozi wanaohimiza watu ''wakatibiwe katika hospitali wasizo na imani nazo'' Nape umesahau kuwa Mwenyekiti wako wa chama anachekiwa(si kutibiwa) afya Ulaya? Umesahau kuwa Marais wote na mawaziri wakuu wastaafu na waliojiuzulu kutoka chama chako wanatibiwa Ulaya kwa pesa za walipa kodi?
Je, nao wana walk the talk! Je, wanasimamia kauli kuwa Muhimbili ni pazuri sana na twende huko si ulaya, India n.k!
Spika wa bunge linaloongozwa na chama chako amefikia mahali pa kuita wahindi waje kucheki afya za wabunge, je, naye anahimiza matibabu kule asikotibiwa au ana walk the talk kwa maana yako? Anatenda anachohubiri au naye ni kama Slaa asiye walk the talk kwa maana yako
Sijui kingetokea nini kama Zitto ndiye angesema ana kadi hiyo. Ninashindwa kutabiri kwasababu sijui kingetokea nini kama Selelii, Shelukindo wangekutwa na ufisadi wa kuhujumu nchini kama ilivyo kwa Lowassa na Chenge!
Hilo sitakubaliana nawe unless unishawishi kuwa mfano huo hauna uwiano.
Mwisho kabisa, Nape nakushauri ujikite na kujifunza siasa za kileo kulingana na elimu yako, exposure na nafasi yako.
Mijadala kama hii unaoyiita mijadala inadhalilisha sana nafasi ya uongozi katika nchi yetu.
Katibu mwenezi wa chama tawala, mjumbe wa halamashauri kuu, mkutano mkuu na kamati kuu unapolete hoja za kiwango duni katika mizania hii, masikini wa TZ hana sababu ya kuwa na tumaini tena bali kilio na msiba tu.
Nape, unazidi kuipa nguvu hoja ninayoitetea kila siku kuwa uongozi ni hekima, maono na busara wala si umri , jinsia, kabila au dini. Uongozi ni kitu anachotunukiwa mtu na mola wake wala si unasaba au kurithishana kwa majina.
Ungekaa kimya ingekusaidia sana maana kila unapoandika unatutoa mashaka tuliyokuwa nayo juu yako.
Wako Raia mtiifu
Nguruvi3