Nape si mzima!!

Nape si mzima!!

Nape hii single imepoteza mvuto tafuta single nyingine ya kutokea
 
Msumari huo,nape yupo vizuri cha msingi ni kujibu hoja je ingekiwa zitto ingekuwa vipi ? Na je kauli ya padr mzinifu kwamba kuwa na kadi ya ccm ni laana nayo mnasemaje ? Na je kuwaadaa wenzakevwarudishe kadi za ccm wakati yeye bado anaitunza siyo unafiki ?

This is all nonsense!! Nape amekuwa akibadilisha kauli kila mara. Alisema kuna viongozi wa Chadema wenye kadi za CCM na tena wanazilipia, akiwemo Dr. Slaa. Alipopigwa shule ya hoja kuhusu umbumbu wa kile alichokisema na kumtaka alete orodha ya namba za risiti zinazolipiwa, akaja na hoja kuwa ataleta orodha ikiwa Dr Slaa ataendeleakubisha. Sasa ameendelea kubanwa vilivyo, analeta matusi na kusema alisema kuwa Dr. Slaa ana kadi ya CCM ambayo si kosa. Ushahidi ulioutaja wa risiki umeingia nao mitini. What a nonsense. Nape, acha kutupotezea muda!! Huna issue na nchi hii ina mambo mengi ya msingi ya kujadili ikiwa ni pamoja na katiba mpya. Dr. Slaa humwezi na ukweli ni kuwa unazidi kuijenga Chadema na Slaa mwenyewe.
 
Nape ana akili tena ana moyo na huruma ya kuwatumikia watanzania maskini - ila CCM wanamtumia wanamharibu believe me guys!!
bad enought the guy is still young - walio wengi ni wazee na wataondoka katika medani za kisiasa in next 5 to 10 yrs yeye atabaki - aelewe ushauri wa bure.
 
Dr. Slaa nafikiri ana umri wa miaka 60 hivi arround-- wewe Nape una arround 35 sasa UBABU na DR.Slaa umetoka wapi kama siyo udaku? huyu ni baba yako ki umri lazima umheshimu. mpinge kwa hoja za msingi na si stories za kuunga unga sis watanzania hatukuelewi kabisa.

Vijana wa 20''s na kushuka ndiyo wanaweza kumwita Babu. :becky: pia hawa vijana wanaweza kumwita wewe ni BABA.
 
Huyu kalelewa na makamba na ndo kampa mke. Sasa hapo unaweza tafakari uelewa wake
 
Msumari huo,nape yupo vizuri cha msingi ni kujibu hoja je ingekiwa zitto ingekuwa vipi ? Na je kauli ya padr mzinifu kwamba kuwa na kadi ya ccm ni laana nayo mnasemaje ? Na je kuwaadaa wenzakevwarudishe kadi za ccm wakati yeye bado anaitunza siyo unafiki ?


hakuna hoja ya msingi aliyoitoa Nape zaidi ya kupiga porojo zisizo na tija kwa Taifa. mm ningemsifu endapo angetujibu maswali yafuatayo-
1. nani aliiba fedha za EPA na ni hatua gani zimechukuliwa kwake;
2. Nani muasisi wa Richmond/Dowans na uwizi wake na ni hatua gani zimechukuliwa kwake
3. Nani aliuza Loliondo kwa waarabu na hatua gani zimechukuliwa kwa mhusika na kwanini ardhi iliyouzwa kwa waarabu wa omani haijarejeshwa kwenye himaya ya watanzania
4. Nani aliyehusika na anayehusika katika usafirishaji wa wanyama hai wakiwemo Twiga, tembo n.k. na hatua gani zimechukuliwa dhidi yake
5. Kinana na kundi lake ambao ni wasomali kwa asili ni lini wamepewa uraia
6. Kinana anayedaiwa kushiriki kuhujumu uchumi wa nchi kwa kuua tembo na kusafirisha meno ya tembo amechukuliwa hatua gani
7. Nani ni fisadi na mmiliki wa MEREMETA na hatua gani zimechukuliwa dhidi yake
8.Nani ni mlimiki wa mgodi wa kiwira uliouzwa kifisadi na hatua gani zimechukuliwa dhidi yake
9. kwanini baada ya miaka 50 ya uhuru Tanzaania bado maskini hatuana maji, umeme, huduma bora za afya, shule, barabara za uhakika na maendeleo yanayostahili.
10.Nani alikula rushwa wakati wa ununuzi wa Rada na hatua gani zimechukuliwa dhidi yake
11. Nani anahusika na biashara ya dawa za kulevya ndani ya chama chake na hatua gani zimechukuliwa dhidi yake.
12. Nani anahusika na biashara haramu ya binadamu ndani ya chama chake na hatua gani zimechukuliwa
13. je sera ya kujivua gamba imeishia wapi na nini mafanikio yake
14. endless list........................................

kwangu kadi haina tofauti na ticket ya bus au kitambulisho cha shule ambavyo vingi watu huondoka navyo kama kumbukumbu, hicho ndicho hata Dr. Slaa alifanya. hakuna jipya ni porojo akumbuke iko siku atakua nje ya serikali ya ccm aawajibika kwa kila analolifanya yeye binafsi na sio chama

hatua gani zimechukuliwa kwa wanachama mafisadi wa aina hii katika kuwavua uanachama na kushitakiwa
 
DR. SLAA NA KADI YA CCM, NA UNAFIKI WA WATETEZI *WAKE

Kwa muda sasa wa karibu wiki tatu au nne pamekuwa na mjadala mkubwa juu ya kumiliki kadi ya CCM kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na padri aliye asi Dr. Wilbroad Slaa.Mjadala huu umeingiza watu wengi sana kwenye maeneo mbalimbali lakini ukigawa wajadiliji kwenye makundi matatu makubwa, kundi la kwanza la wanaoona Dr. Slaa kateleza hasa majibu yake juu ya kwanini anayo kadi ya CCM, kundi la pili la watetezi wake na kundi la tatu la watazamaji wasiokuwa na upande maalum.

Nikiri wazi kuwa pamoja na kuwa mimi ndie niliyeanzisha mjadala huu, namheshimu sana Dr. Slaa kama mtu mzima sana kwangu na ndo maana huwa namuita babu,lakini bila kumumunya maneno ana mchango katika demokrasia ya nchi yetu bila kujali ni chanya au ni hasi.

Nilipo hoji umiliki wake wa kadi ya CCM nikiri kuwa sikutegemea kama angekiri haraka kiasi kile kuwa kweli anamiliki kadi, tena anaitunza kama kumbukumbu. Ndio maana mara baada ya kukiri haraka sana nilitoka hadharani na kumpongeza kwa mara ya kwanza toka nimfahamu ameamua kuwa mkweli. Nikasema ameanza vizuri kujifunza kuwa mkweli,baada ya orodha ndefu ya uongo na uzushi mwingi aliouzoea katika maisha yake ya siasa na yale ya utumishi wa Mungu yaliyomfikisha kwenye kumuasi Mungu na kanisa achilia mbali familia yake yaani mke na watoto.

Jambo kubwa hapa ambalo wapambe wake wanalifanyia unafiki ni kuwa nilipohoji SIKUHOJI UANACHAMA WAKE, NILIHOJI KUWA NA KADI YA CCM MPAKA LEO, TOKA ATOKE CCM KWA MAKEKE. Natambua vizuri sana kuwa uanachama wa CCM kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 matoleo yote, moja ya sababu ya kukoma uanachama ni kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa. Kwa tafsiri rahisi inatosha kujua kuwa Dr. Slaa si mwanachama wa CCM tena. Swali langu likawa kwanini anamiliki kadi ya CCM mpaka leo?

Watetezi wake hebu muulizeni Dr. Slaa alipoasi upadri nyumba ile ya utawa aliyokuwa akiishi kama padri aliondoka na funguo za ile nyumba au vifaa vingine vya upadri kwa madai kuwa ni kumbukumbu kuwa alikuwa padri wakati flani katika maisha yake? Tusikurupuke kumtetea tukadhani tunamsaidia ,kumsaidia kwa kweli ni kumwambia ukweli kuwa hapa babu umeteleza.

Wapo wanaodai hoja hii haina mashiko eti kwasababu hawaoni kama itabadili maisha ya watu masikini. Hawana makosa kusema haya kwasababu ndipo uwezo wao wa kufikiri walipoamua uishie. Lakini hebu fumbueni macho mtazame ukweli huu, moja ya tatizo kubwa la binadamu wengi na hasa viongozi ni kuwa wazuri sana wa kusema wasiyoyaamini wala kuyaishi ndo maana nchi nyingi masikini, rasilimali zake hazifaidishi walio wengi bali wachache sana,huku wakidai tufunge mkanda wakati wao wanaongeza ukubwa wa suti kwani zinawabana zilizopo.

Wakati flani Kardinali Pengo aliwa kusema, wengi wa wanaopigia kelele ufisadi ni mafisadi watarajiwa lakini kwasasa kwasababu hawajapata furusa za kuwa mafisadi ndo maana wana piga kelele.

Ikumbukwe Dr. Slaa amekuwa akipiga kelele na kuwataka wana CCM waliochoka CCM warudishe kadi za CCM na mfano mzuri ni pale Jangwani ambapo baada ya kulewa ujinga akaamua kuubatiza jina jingine uwanja wa Jangwani, bahati mbaya watanzania wana akili wakampuuza na wakaendelea kuenzi historia nzuri ya uwanja wa Jangwani kwa kuuita jina lake la asili, nadhani ulevi ule ulipoisha wa babu na wapambe wake akagundua kuwa alikuwa amelewa tu ndio maana hawajakumbushia tena jina lile.

Kwanini kama ni mkweli wa nafsi yake asiwaambie wanaorudisha kadi za CCM ukweli kuwa hata yeye katunza yake kama kumbukumbu kwahiyo nao watunze zao kama kumbukumbu, badala ya kuwahimiza warudishe wakati yeye katunza yake? Wapambe wake hili pia mnalifanyia unafiki!!!

Wakati yeye akimiliki kadi ya CCM amekuwa bingwa wa kuwashutumu wenzake *kuwa ni mamluki eti wa CCM ndani ya Chama chake wakati kati ya hao anaowashutumu na wengine kuwafukuza wengine hawajawahi hata kuwa na kadi tu za CCM. Watetezi wa babu hebu tuwe wa kweli kama kadi hii angekiri anayo Zitto hali ingekuaje? Mngetoka kumtetea pia dhidi ya hasira za babu na wafuasi wake dhidi ya Zitto au hasimu wake yeyote mwingine?

Babu anatofauti gani na wanaohimiza watu kujikinga na ukimwi wakati wao hata kinga hawaijui? Wanahutubia mkutano wa kupinga rushwa mpaka mapovu yanawatoka wakishuka wao ndo wanaulizia rushwa tena kwa ukali mkubwa? Anatofauti gani na msimamizi wa hospitali anayehimiza watu wakatibiwe kwenye hospitali hiyo na huku yeye mwenyewe hana imani na tiba za pale matokeo yake hata homa tu anakwenda ng'ambo kuitibu? Huyu ndo mnataka awe kiongozi mkuu wa nchi yetu? Anasema asiyoyaamini na kuishi asiyoyasema??!!

Mnasema ni hoja ya kipuuzi huku bado kucha kuchwa mnaijadili? Kwanini mjadili hoja ya kupuuzi kama kweli ni ya kipuuzi? Huu ni unafiki haupaswi kufumbiwa macho, ni vizuri tujifunze kukubali kujikosoa na kukosolewa.

Sina tabu na umiliki wa babu wa kadi ya CCM kama tu angewahamasisha na wengine wafanye kama anavyofanya yeye, kuongoza ni kuonyesha njia. Si uongozi bora kusema fuateni maneno yangu na si matendo yangu, kiongozi wa namna hiyo hatumhitaji kwasasa.

Ndio maana tunashuhudia CHADEMA chini ya babu huyu kama katibu mkuu wa chama, wameshindwa mpaka leo kuweka bayana msimamo wao juu ya sera za ushoga huku wakiwa marafiki na wapokeaji wakubwa wa misaada kutoka kwa waumini wakubwa wa ushoga duniani. Wanasiasa wanaosema wasichoamini na hawatendi isipokuwa wanataka watu watende. Onyesheni upendo wa kweli kwa babu yangu huyu kwa kumwambia ukweli badala ya kumdanganya na kumfanya apumbazike. KUONGOZA NI KUONYESHA NJIA.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki CCM.

Imetolewa na;
NapeMoses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa
nipende kumweleza huyu mdudu mchafu tanzania(TOPE=NAPE) kuwa ipo sku itafika atakuwa km yule jamaa aliyesemekana alikufa(aliyewahi kuwa govenor) kumbe kaficha upuuzi na uchafu wa ccm.we tope ama utatupwa jararani km kondm ama utakufa ukiwa hai lkn kwa ufupi ni kwamba jiandae kukimbia Tanzania kukimbia kulipa dhambi za uongo wa uchochezi wa ukanda,udini nk
 
Kumbe slaa yuko kwa ajili ya mapambano ee! Ccm ipo kwa ajili ya kushughulikia mambo ya msingi na sio kupambana na watu. Sasa kama chadema mmeji tune kwa mapambano mtapambana na wengine lakini si CCM.

Pole Sana Betlehem. Najua unaelewa ila ni namna unavyotaka jamii ikuone. Ni vizuri kuwa jasiri hata kama unaona narrow gate!. Jipeni moyo pengine mtaona mlango wa kutokea. Sisi tunaona CHADEMA wanasonga mbele. Ni vizuri pengine mkajifunza kwao kama vile ambavyo mmeanza kutekeleza sera za CHADEMA kimya kimya. Hii inaweza kuwasaidia badala ya kuendelea kuwapiga mawe mchana, usiku mwaiba Hekima kwao. Mtaheshimika.
 
1. Hongera kwa Nape kukiri mchango wa Dr. Slaa ktk Taifa hili.
2. Chadema imeshatoa misimamo mara nyingi kuhusu ushoga. INAPINGA USHOGA. Nape asipotoshe. Rejea kauli za Mkurugenzi wa Habari na Uenezi - John Mnyika.
3. Baba yangu ana miaka 65, lakini ana nguvu za akili na mwili. Sijui nimuite Babu. Nina Kaka yangu ana miaka 35 lakini ni mvivu kufikiri na amechakaa kwa kuutumikisha mwili wake kwa starehe. watu wa rika humsalimia wakidhani ni Babu - sijui nimwite Babu. Watanzania wataamua.
 
Pole Sana Betlehem. Najua unaelewa ila ni namna unavyotaka jamii ikuone. Ni vizuri kuwa jasiri hata kama unaona narrow gate!. Jipeni moyo pengine mtaona mlango wa kutokea. Sisi tunaona CHADEMA wanasonga mbele. Ni vizuri pengine mkajifunza kwao kama vile ambavyo mmeanza kutekeleza sera za CHADEMA kimya kimya. Hii inaweza kuwasaidia badala ya kuendelea kuwapiga mawe mchana, usiku mwaiba Hekima kwao. Mtaheshimika.
kumbe chadema wanawatumia kina kalumanzira bwana.aisee! si umesikia alivyo sema zitto?
 
Ukisoma post hiyo siyo ya graduate wa masters mie nakataa kwa sababu zifuatazo:

Una lugha ya matusi,

Una lugha ya dharau,

Una chembe chembe za ubaguzi wa kiumri, na kidini,

Unajiona wewe ndio bora kuliko wengine.

Ningekuwa mimi ndo TCU ningekuvua digrii zako za kuchakachua
na mbaya zaidi anajichubua huu kama siokutafuta mme huku mwaka huu tutajua tu,madaraka yameingiliwa.
 
Nape angejiimarisha kisiasa kama angeliongelea namna nchi yetu ingejitoa katika ufisadi uliokubuhu,
chaguzi zinazotawaliwa na rushwa, mfumuko wa mkubwa wa bei, nk nk
Lakini kwa hili la kusimamia kadi ambayo haina uhusiano na maisha ya watanzania, nina mashaka na uwezo wake kisiasa na kiuongozi
 
Watanzania wanakufa njaa,maliasiri wageni wamemilikishwa,mafisadi wanaimaliza nchi hii,watanzania wengi wamekosa ajira,madakitari hawatoshi nchini,hakuna dawa mahosipitalini,kuna sehemu hapa nchini hawajui kitu kinachoitwa barabara,watoto wa wakulima wanakosa elimu ya juu kwa kukosa mikopo,watoto wa watanzania wanasoma shule za kata ambazo hazina walimu,hazina vitendea kazi.Tujadili namna ya kumkomboa mtanzania ili aweze kutoka kwenye lindi la umasikini wa kupandikizwa sio kujadili kadi.I think we are not serious to what should be discussed here in relation to normal Tanzanian lives.Only cracy people will continue this CCM card discussion.
 
Jamani msipoteze muda, Nape ni mjinga sana bila kipimo. Anadhani watanzania hawa wa leo ni sawa na wale wa mwaka 1995 waliodanganywa na CCM kwamba vyama vya upinzani vikishinda vitataleta fujo kama Burundi na Ruwanda, nonsense kabisa. Mwambieni arudi shuleni kujifunza propaganda aache ujinga. Tumekomaa tunafahamu ukweli hatudanganyiki kama wanavyodhani.
 
kaospitl ti ya moj ya aya anasem huwez kuhimiz wananch kutibiw hospza ndan halaf wew unatibiw nje.viongoz wa nchi watibiw wap?
 
Back
Top Bottom