Nape si mzima!!

Nape si mzima!!

Kweli Mkuu huyo kijana Nape sio Mzima tumuwahishe milembe mapema.
 
Nape unataka kuniambia ukizaliwa nje ya ndo lazima ujifanye umelaaniwa, usimuite Slaa Babu huyo ni DR.acha wivu ukisoma utapta. nayeye akikuona mweupe sana akuite MR. karorite au mkorogo! siyo siri Nape unatatizo ukiisha kuwa kuwa kidog ukageuka nyuma kuangalia uliyo kuwa unayafanya utajisikitikia sana, kweli na kwambia, CCM isikuzingue sana itakufa kama ilivyo kufa CCJ baada ya hapo sijui nawewe utajiua!?
 
Nape ndege chichidodo, mtoto wa nje ya ndoa kwetu tunawaita mapaka shume. Slaa babu yako kakuzalia nani wewe?? Mamako au babako?? Mangula na wasira je, ni wajomba zako? Ndiyo maana huowi au si riziki? Slaa ni rais wa tz novemba 2015. Nyambaf.
 
Slaa angekuwa babu yako ange kunywa sumu afe kuliko kuwa na mjukuu mpuuzi kama wewe, au hicho juu ya shingo yako siyo kichwa ni dafu tusikulaumu bure
 
Nilidhani umeleta uthibitisho wa risiti za kulipia kadi ya Slaa.

Hoja ya kulipia kadi ndio wenzako waliikuza sana na wakaongeza kuwa mpaka 2016 imeshalipiwa!

Tunaweka kwenye rekodi UONGO mwingine toka kwa NAPE.
 
Kwa nini Aushwitz kuna makumbusho ya concentration camps?

Kwa nini Nürnberg, Germany kuna makumbusho ya ukatili wa Hitler dhidi ya Wayahudi?

Kwa nini Rwanda kuna makumbusho ya mauaji ya kimbari?

Je kila kumbukumbu inayowekwa ni kwa ajili ya jambo ambalo unalikumbuka kwa wema tu?

Uongozi alio nao Dr. Slaa, ni wa kuvuta watu kwenye sera zinazolenga maslahi ya watanzania, na si lengo lake kuwafanya watu wanakili maisha yake.

Nape kama kiongozi unapaswa kujua kuwa kuna mbwembwe za kisiasa ambazo zinaleta hamasa na kwa watu wengine kujiunga na chama, hizo hata CCM mnatumia, ingawa na wewe hujawaambia watu kadi yako ya CCJ umepeleka wapi.

Umebadili kabisa msisitizo wa hoja yako, baada ya kuona uongo wako ni dhahiri. Tunajua ulisema kuwa Dr. Slaa analipia kadi na kutishia kuanika hapa. Kwa kusema analipia ililenga uanachama, maana kwenye katiba ya CCM hakuna malipo ya kadi bali kuna malipo ya uanachama. Leo umekuja na kusema haihuisiki na uanachama.

NJIA YA MWONGO NI FUPI:
 
A fool at fourty is a fool indeed, haya endelea kukisaidia chama kwa nafasi uliyonayo
 
Nilidhani umeleta uthibitisho wa risiti za kulipia kadi ya Slaa.

Hoja ya kulipia kadi ndio wenzako waliikuza sana na wakaongeza kuwa mpaka 2016 imeshalipiwa!

Tunaweka kwenye rekodi UONGO mwingine toka kwa NAPE.

kweli mkuu wangu na mimi nimeifungua hii thread haraka haraka nikijua labda zile listi za malipo ya kadi ndo zimewekwa sasa.
Nape mimi ndiyo maana huwa nasema wewe ni kiazi kama viazi vingine,ulisema kuwa tukiendelea kubisha utatuletea listi za malipo ya uanachama wa Dr Slaa kwa kadi anayoimiliki,sasa leo unabwabwaja tena mengine.Ushauri wangu ni kuwa Slaa na wewe ni vitu viwili tofauti wala huwezi kutafuta ligi na yule Dr Slaa.Jiangalie pamoja na kubebwa na media na dola lakini huna hata punje ya postive effects katika taifa hili kama aliyonayo Dr Slaa.Muhimu endelea kuwalamba miguu mafisadi huna lolote.....................................
 
......pamoja na kuwa mimi ndie niliyeanzisha mjadala huu, namheshimu sana Dr. Slaa kama mtu mzima sana kwangu na ndo maana huwa namuita babu,lakini bila kumumunya maneno ana mchango katika demokrasia ya nchi yetu bila kujali ni chanya au ni hasi.(HAPO SAWA)

........Chadema chini ya babu huyu kama katibu mkuu wa chama, wameshindwa mpaka leo kuweka bayana msimamo wao juu ya sera za ushoga ( HILI NI SUALA LA DUNIA NZIMA NADHANI HATA HAPO IKULU UNAJUA HAYA MAMBO YAPO HATA HUKO MNAPOENDAGA KUKOPA WALIOTAWALA HIZO OFISI/MABENKI HIZI NI SERA ZAO KWA HIYO HAPO USIWATUMBUKIZE CHADEMA KWENYE MGOGORO WA KIDUNIA)
 
Du naona Nape unajaribu kuchangamsha propaganda yako mfu. Watu wameikata hiyo mkubwa jaribu nyingine.
 
Msumari huo,nape yupo vizuri cha msingi ni kujibu hoja je ingekiwa zitto ingekuwa vipi ? Na je kauli ya padr mzinifu kwamba kuwa na kadi ya ccm ni laana nayo mnasemaje ? Na je kuwaadaa wenzakevwarudishe kadi za ccm wakati yeye bado anaitunza siyo unafiki ?


Daaa we kxxa una ID nyingi nape unatuma na kujijibu mwenyewe tunasema akina ritz kumbe Jr, faiza etc
 
Nape,

Unaweza ukamwambia nape kwamba ni mjinga kwa sababu ya kusema ukweli pole sana, mkubwa lakini lazima ukubari kwamba babu ana makosa kuendelea kumilki kadi ya ccm lakini baado mnamtetea kwamba hana kosa basi kumbe hata kuitelekekeza famila yake hakufanya kosa lolote!

Kwa nini ufikiri ni kosa??? Ni wapi imeandikwa kadi lazima irudishwe ...utashi wa mtu nalo ni kosa? Niambie katika Tanzania ya leo mtu aliyeiumbua CCM katika mambo lukuki kama Slaa. Kwa jalamba alilolipiga mpaka CCM akili zikaanza kuwarudi kichwani; inatosha kusema Slaa hata kama angemiliki kadi mia bado mtu safi.

suala la familia ni issue normal, mbona Mwenyekiti wenu amewatenda wake za watu kibao tena akiwa kwenye mamlaka??? alipozaaa na V.K alishariana na mke wake??? Je hakusaliti familia yake??????

Mbona CCM mnapenda siasa uchwara? kwa nini msiongelee mambo ya uchumi, elimu na afya??? Inasikitisha serikali ya CCM haijui idadi ya wanafunzi wanaokaa chini bila madawati wala wagonjwa wanaolala kwenye sakafu hospitalini. Kazi hiyo imeachiwa NMB na makampuni mengine.....shame!!
 
Kwa nini ufikiri ni kosa???Mbona husemi ugolo wako na CCJ? Ni wapi imeandikwa kadi lazima irudishwe ...utashi wa mtu nalo ni kosa? Niambie katika Tanzania ya leo mtu aliyeiumbua CCM katika mambo lukuki kama Slaa. Kwa jalamba alilolipiga mpaka CCM akili zikaanza kuwarudi kichwani; inatosha kusema Slaa hata kama angemiliki kadi mia bado mtu safi.

suala la familia ni issue normal, mbona Mwenyekiti wenu amewatenda wake za watu kibao tena akiwa kwenye mamlaka??? alipozaaa na Vick alishariana na mke wake??? Je hakusaliti familia yake??????

Mbona CCM mnapenda siasa uchwara? kwa nini msiongelee mambo ya uchumi, elimu na afya??? Inasikitisha serikali ya CCM haijui idadi ya wanafunzi wanaokaa chini bila madawati wala wagonjwa wanaolala kwenye sakafu hospitalini. Kazi hiyo imeachiwa NMB na makampuni mengine.....shame!!
 
Nnauye Jr. Nadhibitisha Leo Kuwa wewe sio mtoto wa ndoa na Kama ni wa ndoa basi we bwabwa sasa Unakuja na vihoja badala ya hoja? Katibu mwenezi ccm Tehe Tehe Tehe



DR. SLAA NA KADI YA CCM, NA UNAFIKI WA WATETEZI *WAKE

Kwa muda sasa wa karibu wiki tatu au nne pamekuwa na mjadala mkubwa juu ya kumiliki kadi ya CCM kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na padri aliye asi Dr. Wilbroad Slaa.Mjadala huu umeingiza watu wengi sana kwenye maeneo mbalimbali lakini ukigawa wajadiliji kwenye makundi matatu makubwa, kundi la kwanza la wanaoona Dr. Slaa kateleza hasa majibu yake juu ya kwanini anayo kadi ya CCM, kundi la pili la watetezi wake na kundi la tatu la watazamaji wasiokuwa na upande maalum.

Nikiri wazi kuwa pamoja na kuwa mimi ndie niliyeanzisha mjadala huu, namheshimu sana Dr. Slaa kama mtu mzima sana kwangu na ndo maana huwa namuita babu,lakini bila kumumunya maneno ana mchango katika demokrasia ya nchi yetu bila kujali ni chanya au ni hasi.

Nilipo hoji umiliki wake wa kadi ya CCM nikiri kuwa sikutegemea kama angekiri haraka kiasi kile kuwa kweli anamiliki kadi, tena anaitunza kama kumbukumbu. Ndio maana mara baada ya kukiri haraka sana nilitoka hadharani na kumpongeza kwa mara ya kwanza toka nimfahamu ameamua kuwa mkweli. Nikasema ameanza vizuri kujifunza kuwa mkweli,baada ya orodha ndefu ya uongo na uzushi mwingi aliouzoea katika maisha yake ya siasa na yale ya utumishi wa Mungu yaliyomfikisha kwenye kumuasi Mungu na kanisa achilia mbali familia yake yaani mke na watoto.

Jambo kubwa hapa ambalo wapambe wake wanalifanyia unafiki ni kuwa nilipohoji SIKUHOJI UANACHAMA WAKE, NILIHOJI KUWA NA KADI YA CCM MPAKA LEO, TOKA ATOKE CCM KWA MAKEKE. Natambua vizuri sana kuwa uanachama wa CCM kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 matoleo yote, moja ya sababu ya kukoma uanachama ni kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa. Kwa tafsiri rahisi inatosha kujua kuwa Dr. Slaa si mwanachama wa CCM tena. Swali langu likawa kwanini anamiliki kadi ya CCM mpaka leo?

Watetezi wake hebu muulizeni Dr. Slaa alipoasi upadri nyumba ile ya utawa aliyokuwa akiishi kama padri aliondoka na funguo za ile nyumba au vifaa vingine vya upadri kwa madai kuwa ni kumbukumbu kuwa alikuwa padri wakati flani katika maisha yake? Tusikurupuke kumtetea tukadhani tunamsaidia ,kumsaidia kwa kweli ni kumwambia ukweli kuwa hapa babu umeteleza.

Wapo wanaodai hoja hii haina mashiko eti kwasababu hawaoni kama itabadili maisha ya watu masikini. Hawana makosa kusema haya kwasababu ndipo uwezo wao wa kufikiri walipoamua uishie. Lakini hebu fumbueni macho mtazame ukweli huu, moja ya tatizo kubwa la binadamu wengi na hasa viongozi ni kuwa wazuri sana wa kusema wasiyoyaamini wala kuyaishi ndo maana nchi nyingi masikini, rasilimali zake hazifaidishi walio wengi bali wachache sana,huku wakidai tufunge mkanda wakati wao wanaongeza ukubwa wa suti kwani zinawabana zilizopo.

Wakati flani Kardinali Pengo aliwa kusema, wengi wa wanaopigia kelele ufisadi ni mafisadi watarajiwa lakini kwasasa kwasababu hawajapata furusa za kuwa mafisadi ndo maana wana piga kelele.

Ikumbukwe Dr. Slaa amekuwa akipiga kelele na kuwataka wana CCM waliochoka CCM warudishe kadi za CCM na mfano mzuri ni pale Jangwani ambapo baada ya kulewa ujinga akaamua kuubatiza jina jingine uwanja wa Jangwani, bahati mbaya watanzania wana akili wakampuuza na wakaendelea kuenzi historia nzuri ya uwanja wa Jangwani kwa kuuita jina lake la asili, nadhani ulevi ule ulipoisha wa babu na wapambe wake akagundua kuwa alikuwa amelewa tu ndio maana hawajakumbushia tena jina lile.

Kwanini kama ni mkweli wa nafsi yake asiwaambie wanaorudisha kadi za CCM ukweli kuwa hata yeye katunza yake kama kumbukumbu kwahiyo nao watunze zao kama kumbukumbu, badala ya kuwahimiza warudishe wakati yeye katunza yake? Wapambe wake hili pia mnalifanyia unafiki!!!

Wakati yeye akimiliki kadi ya CCM amekuwa bingwa wa kuwashutumu wenzake *kuwa ni mamluki eti wa CCM ndani ya Chama chake wakati kati ya hao anaowashutumu na wengine kuwafukuza wengine hawajawahi hata kuwa na kadi tu za CCM. Watetezi wa babu hebu tuwe wa kweli kama kadi hii angekiri anayo Zitto hali ingekuaje? Mngetoka kumtetea pia dhidi ya hasira za babu na wafuasi wake dhidi ya Zitto au hasimu wake yeyote mwingine?

Babu anatofauti gani na wanaohimiza watu kujikinga na ukimwi wakati wao hata kinga hawaijui? Wanahutubia mkutano wa kupinga rushwa mpaka mapovu yanawatoka wakishuka wao ndo wanaulizia rushwa tena kwa ukali mkubwa? Anatofauti gani na msimamizi wa hospitali anayehimiza watu wakatibiwe kwenye hospitali hiyo na huku yeye mwenyewe hana imani na tiba za pale matokeo yake hata homa tu anakwenda ng'ambo kuitibu? Huyu ndo mnataka awe kiongozi mkuu wa nchi yetu? Anasema asiyoyaamini na kuishi asiyoyasema??!!

Mnasema ni hoja ya kipuuzi huku bado kucha kuchwa mnaijadili? Kwanini mjadili hoja ya kupuuzi kama kweli ni ya kipuuzi? Huu ni unafiki haupaswi kufumbiwa macho, ni vizuri tujifunze kukubali kujikosoa na kukosolewa.

Sina tabu na umiliki wa babu wa kadi ya CCM kama tu angewahamasisha na wengine wafanye kama anavyofanya yeye, kuongoza ni kuonyesha njia. Si uongozi bora kusema fuateni maneno yangu na si matendo yangu, kiongozi wa namna hiyo hatumhitaji kwasasa.

Ndio maana tunashuhudia Chadema chini ya babu huyu kama katibu mkuu wa chama, wameshindwa mpaka leo kuweka bayana msimamo wao juu ya sera za ushoga huku wakiwa marafiki na wapokeaji wakubwa wa misaada kutoka kwa waumini wakubwa wa ushoga duniani. Wanasiasa wanaosema wasichoamini na hawatendi isipokuwa wanataka watu watende. Onyesheni upendo wa kweli kwa babu yangu huyu kwa kumwambia ukweli badala ya kumdanganya na kumfanya apumbazike. KUONGOZA NI KUONYESHA NJIA.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki CCM.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa
 
Sioni shida kama nape ameandika haya kwenye face book wall yake au hapa JF. Lakini jinsi taarifa ilivyosainiwa nahisi kama ni taarifa rasmi ya chama. Kama hivyo ndivyo, kuna shida kubwa
 
Pole Nnauye Jr,sisi tumeshatoka huko kwenye makadikadi,tunasonga mbele,tafuta hoja nyingine Vuvu Zii!
 
Pole Nnauye Jr,sisi tumeshatoka huko kwenye makadikadi,tunasonga mbele,tafuta hoja nyingine Vuvu Zii!
 
Back
Top Bottom