Nape si mzima!!

Nape si mzima!!

DR. SLAA NA KADI YA CCM, NA UNAFIKI WA WATETEZI *WAKE

Kwa muda sasa wa karibu wiki tatu au nne pamekuwa na mjadala mkubwa juu ya kumiliki kadi ya CCM kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na padri aliye asi Dr. Wilbroad Slaa.Mjadala huu umeingiza watu wengi sana kwenye maeneo mbalimbali lakini ukigawa wajadiliji kwenye makundi matatu makubwa, kundi la kwanza la wanaoona Dr. Slaa kateleza hasa majibu yake juu ya kwanini anayo kadi ya CCM, kundi la pili la watetezi wake na kundi la tatu la watazamaji wasiokuwa na upande maalum.

Nikiri wazi kuwa pamoja na kuwa mimi ndie niliyeanzisha mjadala huu, namheshimu sana Dr. Slaa kama mtu mzima sana kwangu na ndo maana huwa namuita babu,lakini bila kumumunya maneno ana mchango katika demokrasia ya nchi yetu bila kujali ni chanya au ni hasi.

Nilipo hoji umiliki wake wa kadi ya CCM nikiri kuwa sikutegemea kama angekiri haraka kiasi kile kuwa kweli anamiliki kadi, tena anaitunza kama kumbukumbu. Ndio maana mara baada ya kukiri haraka sana nilitoka hadharani na kumpongeza kwa mara ya kwanza toka nimfahamu ameamua kuwa mkweli. Nikasema ameanza vizuri kujifunza kuwa mkweli,baada ya orodha ndefu ya uongo na uzushi mwingi aliouzoea katika maisha yake ya siasa na yale ya utumishi wa Mungu yaliyomfikisha kwenye kumuasi Mungu na kanisa achilia mbali familia yake yaani mke na watoto.

Jambo kubwa hapa ambalo wapambe wake wanalifanyia unafiki ni kuwa nilipohoji SIKUHOJI UANACHAMA WAKE, NILIHOJI KUWA NA KADI YA CCM MPAKA LEO, TOKA ATOKE CCM KWA MAKEKE. Natambua vizuri sana kuwa uanachama wa CCM kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 matoleo yote, moja ya sababu ya kukoma uanachama ni kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa. Kwa tafsiri rahisi inatosha kujua kuwa Dr. Slaa si mwanachama wa CCM tena. Swali langu likawa kwanini anamiliki kadi ya CCM mpaka leo?

Watetezi wake hebu muulizeni Dr. Slaa alipoasi upadri nyumba ile ya utawa aliyokuwa akiishi kama padri aliondoka na funguo za ile nyumba au vifaa vingine vya upadri kwa madai kuwa ni kumbukumbu kuwa alikuwa padri wakati flani katika maisha yake? Tusikurupuke kumtetea tukadhani tunamsaidia ,kumsaidia kwa kweli ni kumwambia ukweli kuwa hapa babu umeteleza.

Wapo wanaodai hoja hii haina mashiko eti kwasababu hawaoni kama itabadili maisha ya watu masikini. Hawana makosa kusema haya kwasababu ndipo uwezo wao wa kufikiri walipoamua uishie. Lakini hebu fumbueni macho mtazame ukweli huu, moja ya tatizo kubwa la binadamu wengi na hasa viongozi ni kuwa wazuri sana wa kusema wasiyoyaamini wala kuyaishi ndo maana nchi nyingi masikini, rasilimali zake hazifaidishi walio wengi bali wachache sana,huku wakidai tufunge mkanda wakati wao wanaongeza ukubwa wa suti kwani zinawabana zilizopo.

Wakati flani Kardinali Pengo aliwa kusema, wengi wa wanaopigia kelele ufisadi ni mafisadi watarajiwa lakini kwasasa kwasababu hawajapata furusa za kuwa mafisadi ndo maana wana piga kelele.

Ikumbukwe Dr. Slaa amekuwa akipiga kelele na kuwataka wana CCM waliochoka CCM warudishe kadi za CCM na mfano mzuri ni pale Jangwani ambapo baada ya kulewa ujinga akaamua kuubatiza jina jingine uwanja wa Jangwani, bahati mbaya watanzania wana akili wakampuuza na wakaendelea kuenzi historia nzuri ya uwanja wa Jangwani kwa kuuita jina lake la asili, nadhani ulevi ule ulipoisha wa babu na wapambe wake akagundua kuwa alikuwa amelewa tu ndio maana hawajakumbushia tena jina lile.

Kwanini kama ni mkweli wa nafsi yake asiwaambie wanaorudisha kadi za CCM ukweli kuwa hata yeye katunza yake kama kumbukumbu kwahiyo nao watunze zao kama kumbukumbu, badala ya kuwahimiza warudishe wakati yeye katunza yake? Wapambe wake hili pia mnalifanyia unafiki!!!

Wakati yeye akimiliki kadi ya CCM amekuwa bingwa wa kuwashutumu wenzake *kuwa ni mamluki eti wa CCM ndani ya Chama chake wakati kati ya hao anaowashutumu na wengine kuwafukuza wengine hawajawahi hata kuwa na kadi tu za CCM. Watetezi wa babu hebu tuwe wa kweli kama kadi hii angekiri anayo Zitto hali ingekuaje? Mngetoka kumtetea pia dhidi ya hasira za babu na wafuasi wake dhidi ya Zitto au hasimu wake yeyote mwingine?

Babu anatofauti gani na wanaohimiza watu kujikinga na ukimwi wakati wao hata kinga hawaijui? Wanahutubia mkutano wa kupinga rushwa mpaka mapovu yanawatoka wakishuka wao ndo wanaulizia rushwa tena kwa ukali mkubwa? Anatofauti gani na msimamizi wa hospitali anayehimiza watu wakatibiwe kwenye hospitali hiyo na huku yeye mwenyewe hana imani na tiba za pale matokeo yake hata homa tu anakwenda ng'ambo kuitibu? Huyu ndo mnataka awe kiongozi mkuu wa nchi yetu? Anasema asiyoyaamini na kuishi asiyoyasema??!!

Mnasema ni hoja ya kipuuzi huku bado kucha kuchwa mnaijadili? Kwanini mjadili hoja ya kupuuzi kama kweli ni ya kipuuzi? Huu ni unafiki haupaswi kufumbiwa macho, ni vizuri tujifunze kukubali kujikosoa na kukosolewa.

Sina tabu na umiliki wa babu wa kadi ya CCM kama tu angewahamasisha na wengine wafanye kama anavyofanya yeye, kuongoza ni kuonyesha njia. Si uongozi bora kusema fuateni maneno yangu na si matendo yangu, kiongozi wa namna hiyo hatumhitaji kwasasa.

Ndio maana tunashuhudia CHADEMA chini ya babu huyu kama katibu mkuu wa chama, wameshindwa mpaka leo kuweka bayana msimamo wao juu ya sera za ushoga huku wakiwa marafiki na wapokeaji wakubwa wa misaada kutoka kwa waumini wakubwa wa ushoga duniani. Wanasiasa wanaosema wasichoamini na hawatendi isipokuwa wanataka watu watende. Onyesheni upendo wa kweli kwa babu yangu huyu kwa kumwambia ukweli badala ya kumdanganya na kumfanya apumbazike. KUONGOZA NI KUONYESHA NJIA.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki CCM.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa

Hakika nape unalaana ulilelewa mitaani????
 
mwanachama wa ccm haruhusiwi kugombea uongozi cdm wala chama kingine kisheria mbona kitu kidogo!uelewa wako ni wa mashaka sana.kadi ni mali ya mwanachama kikatiba.akihama chama katiba haisemi arudishe kadi ndio maana inslipiwa.una akili gani hata usijue jambo dogo kiasi hiki!usikubali kuika ovyo ovyo.
 
Kwahiyo mnamana nape kafa au taira sjaelewa s mzima ki vipi msimlaumu ndo mwisho wa akili yake hapo tatzo la elm za kuunga unga
 
Back
Top Bottom