Nape Nnauye: Toka moyoni mwangu

Wassira alitoka NCCR mkampokea na sasa ni waziri
Cheo ulichonacho kilikuwa kimeshikiliwa na SHAKAFU iliyotoka CUF..mbeta kuna akina Shitambala na wengineo..mbona huwa hamuwakatai..tena mnawapa kazi viongozi wakuu wa kitaifa kuwapokea
 
Duble unaakili sana, umejuaje?
Ndiyo Duble ana akili kuliko zako mchumia tumbo wakati wa kura za maoni Jimbo la Ubungo ulikuwa nazo timamu ila tangu Jakaya Kikwete akuteue kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi then Ideology and Publicity Secretary umekuwa na ukilaza mwingi sana cause wamekufix bila wewe kujua pole sana kwa kuchagua mafanikio ya muda mfupi yasiyodumu badala ya muda mrefu na yanayodumu!
 
Wassira alitoka NCCR mkampokea na sasa ni waziri
Cheo ulichonacho kilikuwa kimeshikiliwa na SHAKAFU iliyotoka CUF..mbeta kuna akina Shitambala na wengineo..mbona huwa hamuwakatai..tena mnawapa kazi viongozi wakuu wa kitaifa kuwapokea

Thanks you Inkoskaz! bila kumsahau Shaibu Akwilombe Kaimu katibu wa CCM katika mojawapo ya mikoa mipya iliyoanzishwa siku za karibuni!
 
tuliposema mna mafisadi ndani ya chama pale mwembe yanga mlikataa leo yanawatoa manundu.

kila wanalosema chadema ndilo mnafanya,hivi ilani yenu mtaenda kuitekeleza kuzimu?

chuo kikuu cha dodoma lini kilikuwa kwenye ilani yenu?
katiba mpya je?

tunasubiria siku mtakapobadili bendera kwa kuhisi ndiyo imepunguza mvuto wa chama.
 
NImegundua namna bora ya kufanya mjadala JF usitolewe ni kuanzisha FB then watauchukua kuuleta hapa na mjadala utaendelea sana! Ahsante kwa kutembelea wall yangu..... Karibuni tena
yuko wapi yule nape aliye fichua uozo kwenye majengo ya umoja wa vijana wa ccm ambao ulikuwa unafanywa na mzee wa nywele nyeupe!........nadhani sio huyu ninae mjua sasa ambaye hata rangi hajui kutofautisha, nyeusi anaita nyeupe!
 
Kwakuwa mnalipwa kunitukana hapa ndo maana mnaamini kila mtu analipwa kwa kila afanyalo hata kwenda uwani analipwa

Sikutegemea kama unaweza kutumia lugha ya namna hii kwa mwanasiasa na msemaji wa chama tawala, inasikitisha saana. Hivi chama kimefilisika mpaka kukosa lugha ya kujadili hoja?
 
Kaka wewe ni kijana bado, angalia unakokwenda lkn pima upepo unakoelekea kwa kufanya tathmini kule ulikotoka. Miaka mingi sana nilikuwa nikipenda sana chama cha mapinduzi, lkn kwa mtu yeyote anayeangalia chama cha mwaka 1995 tu na kilichopo sasa hawezi hata kuinua mdomo kutetea uozo uliomo achilia mbali kubaki. Sitaki ukwazike lkn nataka ufunguke kidogo viwavi ni wengine hata kama wanakulipa mshahara lakini uangalie mshahara huo utalipwa mpaka lini? Kaka nakushauri jikalie kimya wanakuponza na wamekuweka kama chambo.
 
wewe kak ndo unaonekana hujielew coz jf imeanzishwa bila kujal itikad za vyama sema kinachotokea sasa ni ishara tu kuwa watz hasa vijana waliokuwa wasom wamechoka na ccm na ndo maana hata vyuo vikuu ccm inapata shida sanaa.
 
POLE SANA NAPE UTAONGEA SANA UTADANGANYA SANA KAMA MLIVYOZOEA CCM NAKUPA HINT 1 TU UCHAGUZI WOWOTE MDOGO UKIFANYIKA NAAPA CCM HAISHINDI IFADHI KAULI YANGU TUNAANZIA UKONGA THEN MTAJUA CCM IMEKWISHA KAMA MSIPONUNUA SHAHADA ZA WAPIGA KURA "MTASHINDA TABORA NA DODONA TU".NA KWA TAARIFA YAKO WALE WOTE WANAOSHIRIKI HILO ZOEZI WAMECHOKA NA HAWATAWASAIDIA TENA HICHO KITI KIKALIE KWA SASA LAKINI 2015 UTALIA SANA PEOPLES POWER:rockon:JARIBU ​UGOMBEE UBUNGE POPOTE NCHINI NA MGOMBEA WA CHADEMA JIBU UTALIPATA THIS IS FACT.
 
yaani hata kuandika SCRAPER imemshinda ..... huyu sio kiongozi

Ni jambo la kawaida kukosea kuandika neno,alafu tambua kwamba kujua kingereza hakumaanishi kwamba wewe ni kiongozi mzuri! Mbona hauhoji kwa Wenje au Vincent au Lema au Msigwa wenye elimu duni na wengine za kuunga unga ambazo huwezi fananisha na elimu ya Mh Nape?
 
Wassira alitoka NCCR mkampokea na sasa ni waziri
Cheo ulichonacho kilikuwa kimeshikiliwa na SHAKAFU iliyotoka CUF..mbeta kuna akina Shitambala na wengineo..mbona huwa hamuwakatai..tena mnawapa kazi viongozi wakuu wa kitaifa kuwapokea

Fuatilia vizuri Wassira alikuwa CCM akahama kwenda NCCR na kurudi tena CCM hili ni zao la CCM kama walivyo wengine huko CDM nao tunaamini watarudi tu nyumbani CCM siku moja kwa sababu wamelelewa kisiasa CCM na kukulia CCM na wakirudi kama ni wasafi wanapokelewa kwa mikono miwili!
 
Sikutegemea kama unaweza kutumia lugha ya namna hii kwa mwanasiasa na msemaji wa chama tawala, inasikitisha saana. Hivi chama kimefilisika mpaka kukosa lugha ya kujadili hoja?

umesahau mwanza alikuja na kauli ya kushikishwa ukuta
 
Lakini kuna watu si watafiti kazi yao ni kushabikia tu kama mazuzu, kwani ile kamati ya mashirika ya uma ni ya chadema au ni ya Bunge? CAG ni wa chadema au wa Serikali. Tambua hayo kwanza kuliko kuandika upuuzi wako wa kichadema hapa. @ duble.
CCM kazi yenu ni kutishia tu ili kuwapoza wananchi lakini shinikizo la kujiuzulu limetoka kwa ZITTO na TUNDU LISSU pekee. Filikunjombe kakiri kuwa CCM ni waoga; Kama CAG ni ya serikali kwa nn KIKWETE hakuwawajibisha hao mawaziri mpaka aliposubiri sign 70++ Chini ya usimamizi wa ZITTO na mkakati wa CDM na CUF kufanya maandamano nchi nzima??
Mngeacha kuitisha kikao cha dharura muone kama hii nchi ni ya CCM au la.
 
Hao maprofesor na ma doctor wenu wenye vyeti vya kukirimiwa kama Boss wenu J Kalumekenge!
 
NImegundua namna bora ya kufanya mjadala JF usitolewe ni kuanzisha FB then watauchukua kuuleta hapa na mjadala utaendelea sana! Ahsante kwa kutembelea wall yangu..... Karibuni tena

Nafikiri uwanja wa kiongozi yeyote ni kwenye ofisi zao rasmi tulizowapa badala ya FB, twiter, nk.

Nguvu(power) tulizowapa zinatosha kutengeza tovuti zenye habari za kutosha na mipango yenu ya kuleta maendeleo. Badala yake nguvu hizo mnazitumia kuwanyanyasa wananchi, na kuacha ofisi zetu hazina chochote. Mali na hela zetu mnawaachia wajanja wanatamba nazo kwa kujenga magorofa na magari ya anasa.

Yako wapi maisha bora kwa kila mtanzania?
  1. Tunataka watoto wetu wapate huduma kama wengine.
  2. Tunataka wazee wetu waishi mpaka siku zao walizopangiwa na Mungu wao zifike.
  3. Tunataka huduma kwa watu wote - barabara, afya, akiba, nk
  4. Tunataka kila mtu apate nafasi ya kuzalisha na kupata kipato - sio wanasiasa waingize mamilioni kwa mwezi wengine hata shilingi kumi ni ndoto
  5. Tunataka tujivunie serikali yetu - serikali inalinda nchi na wanachi, sio kulinda wezi na kuua wanachi.
  6. Tunataka tujivunie nchi yetu
  7. Tunataka uhuru wa mawazo, kuamini na kufanya tunayoamini kulingana na katiba - sio wengine wanachinjwa kama kondoo eti ni wapinzani au wanakosa kazi kwa sababu baba zao hawakuwa viongozi au sio marafiki au waamini wa siasa, dini au falsafa fulani
 
Back
Top Bottom