Kwakuwa mnalipwa kunitukana hapa ndo maana mnaamini kila mtu analipwa kwa kila afanyalo hata kwenda uwani analipwa
Mkuu sijui mpwa wako Benjamini au Baraka (kama anapita JF)atajisikiaje kusoma hii sentesi!!
Utasema eti hizi ni mbinu na lugha za kisiasa!!!No!
Siasa ni sayansi.Hamkusoma hivyo Kivukoni Chuo cha Chama miaka hiyo?
Hiyo kauli haibebi taswira ya 'Binadamu wote ni ndugu zangu'.
Ulikuwa na maneno zaidi ya 100 kutumia kumjibu mhusika bila kulazimika kutumia hayo maneno uliyotumia.
Kuhusu wanachama 'SRAPERS' kama wakuu walivyokusahihisha,hujaweza kufafanua ukaeleweka.
Katika siasa tunachojali ni idadi na ubora.Unapopata 'kondoo' mpya,hakuna muda wa kujiuliza kondoo huyo alikuwa chama gani kabla..Hata kama kujua hilo ni muhimu, hilo huja baadaye na wala haliwezi kuwa kipaumbele cha kwanza.
Yesu Kristo alitumia mkakati huo huo...aliwafuata watoza ushuru,wasio na elimu ,makahaba na mafarisayo..na alipowageuza nia zao hakujali tena historia zao,na wote wakawa na hadhi na fursa sawa katika ufalme mpya.Petro,asiye na elimu,alikuja kuwa MWAMBA imara wa kanisa la Kristo.
Ndio maana wewe Nape,pamoja na vyeo vyako,bila kujali Digrii yako ya UZAMILI linapokuja suala la kupiga kura, unaruhusiwa kupiga kura MOJA tu ,sawa na mama muuza supu sokoni.
Watu hutofautiana vipaji na karama.Vivyo hivyo ushawishi.Tunapopata mtu moja au wawili wenye ushawishi toka chama fulani ni furaha kwetu maana tunakuwa na uhakika wa kuwavutia wale akina mama wauza supu zaidi kuwa wanachama na hatimaye kuwa wapiga kura.
Kwa mfano,CHADEMA ikimpata LUSINDE itakuwa imepata hasara,lakini itapata faida kwa kumpata DEO FILIKUNJOMBE!
Right?