Nape Nnauye: Toka moyoni mwangu

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Nape Nnauye
‎(('....TOKA MOYONI MWANGU...

Kwanza nianze kwa Kuipongeza Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM. (CC) Kwa kukutana na kufikia maamuzi ya busara na yenye tija kwa Taifa.

Na pia nimesoma kwa makini yaliyojadiliwa na kuridhiwa na Kamati kuu ya CCM (CC)

Kama taarifa ilivyotolewa na kusainiwa na katibu wa itikadi na Uenezi wa NEC Ndugu Nape Nauye.

*...MASWALI YANGU YA KITOTO NINAYOJIULIZA BILA MAJAWABU...*

1. Hivi kamati kuu haijajiuliza kwa nini Chama Cha Mapinduzi kimepoteza Mvuto na kushindwa kuwashawishi Vijana kukupenda....?

2. Hivi Kamati Kuu (CC) Haijajiuliza kwa nini ilishindwa Jimbo la Arumeru Mashariki.. Licha ya kutumia mabilioni ya fedha na raslimali watu....?

3. Hivi Kamati Kuu (CC) Haijajiuliza na kujadili Kwa nini wanachama na Viongozi wa CCM na wa Serikali wanakihama Chama cha CCM.......?

4. Hivi Kamati Kuu (CC) Haijajiuliza Chanzo cha mgogoro wa CCM Mkoani Arusha unaopelekea Vijana na Wanachama wake Kuhama......?

6. Hivi Kamati Kuu (CC) Haijajiuliza kwa nini mwaka huu 2012 ni Mwaka wa Uchaguzi kwa CCM.

Lakini ajabu kuanzia mshina (Mabalozi) na Matawi wanagomea kujaza fomu za uongozi karibia Nchi nzima.....?

Haya na Mengine kwangu yameonekana ni Maswali ya Kitoto Sana nimejiuliza Mwenyewe nikaishia Kupata Majibu,

Hapa Tanurini natajia Kupata MAJAWABU ya Maswali Yangu hayo))

SIJAAMINI KAMA HAYA NI MASWALI ANAJIULIZA SAMBALA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!​!!KWELI YA KITOTO!!KAMA ALIVYOSEMA
Nape anavyowaza kule fb. naomuomba msamaha kwa kuhamishia mawazo yako huku ila nadhani sio vibaya
 
kamnukuu mtu,halafu haya ndiyo majibu ya nape:

  • Nape Nnauye NAJIULIZA HAYA NDO MASWALI ANAJIULIZA KIJANA WA KITANZANIA??????!!! HUO MVUTO UNAOSEMWA UMEPOTEA KWA TAKWIMU AU KWA KUAMINISHWA GENERALI TU?43 minutes ago · 1

  • Nape Nnauye HAYA MABILIONI YALIYOTUMIWA ARUMERU NI YAPI NI TSHS NGAPI HASA MPAKA YAITWE MABILIONI?42 minutes ago

  • Nape Nnauye HIVI NI UJANJA MTU KUHAMA CHAMA NA CHAMA KINGINE KIKAMPOKEA AU CHAMA MAKINI KITAJIKITA KUTAFUTA WANACHAMA WAPYA KUTOKA KUNDI KUBWA LA WATANZANIA WASIO KUWA NA VYAMA??? UNAJIKITA KUCHUKUA SCREPERS?!!!!!!41 minutes ago

  • Nape Nnauye VIJANA WANAOHAMA ARUSHA NI KINA NANI NA HISTORIA YAO NDANI YA CHAMA ZAIDI YA KUTUKANA VIONGOZI WA CCM NI NINI?40 minutes ago

  • Sleim Salum CCM ni chama kikubwa40 minutes ago

  • Nape Nnauye TAKWIMU ZINAONYESHA KINONDONI PEKEAKE TENA KWENYE MATAWI TU ACHILIA MBALI KATA NA WILAYA TUNAO MAPROFESA, WANAJESHI WASTAAFU, MA DOCTARI, GRADUATES NK WAMEGOMBEA , ANAYEDANGANYA ETI WATU HAWATAKI KUJAZA FOMU NANI?38 minutes ago

kwa nini CC ichukue uamuzi baaada ya shinikizo la kumng'oa pm na kutishia kutopisha bajeti za wizara 8 endapo mawaziri hawataondolewa ???

Hadi hapa ni Chama kipi kinaongoza nchi hii kwa remote control ??
 
Safi sana nape, hawa wamefanya jf kama hati miliki ya chadema msikate tamaa hakuna kizuri kikachokuja bila vikwazo
 
Tumesha wazoea, AKIFA KWA NGOMA mtasema ALIKUFA KWA PRESHA ama Ki SUGAR....
Hata jana tulishuhudia MP akizomewa live lakini Mwenyewe akikanusha kuwa hakuzomewa.. Mtakanusha sana tu mwaka huu.. KIMBUNGA HIKI Kaka...
 
Lakini kuna watu si watafiti kazi yao ni kushabikia tu kama mazuzu, kwani ile kamati ya mashirika ya uma ni ya chadema au ni ya Bunge? CAG ni wa chadema au wa Serikali. Tambua hayo kwanza kuliko kuandika upuuzi wako wa kichadema hapa. @ duble.
 
Sina haja ya kunukuu maneno yaliyoandikwa kwenye vitabu wakati sijazaliwa. hebu twende hapo Iraq tu, baada ya majeshi ya Marekani kuiteka Baghdad lakini bado yule waziri wa Habari Al Sahaf alikuwa na ushuja wa kijinga na kujisifu kwamba hakuna hata Mmarekani mmoja atakaekanyaga Baghdad na Baghdad ndio litakuwa kaburi lao na kwamba Baghdad ilikuwa haijatekwa!!

Lakini ukweli halisi yule jamaa mpaka sasa anaishi uhamishoni, sasa Nape ni mganga njaa tu, subilini kwenye uchaguzi wao wa ndani mwaka huu JK amuweke kando hamtoamini masikio yenu.

Nape ni mtu ambaye hajui alifanyalo na nadhani bado hamfahamu vyema JK kwamba anaweza kuteuwa sura mpya kwenye CCM Taifa baadaye mwaka huu, na ndio mtawajuwa walivyo wanafki hawa vVijana wazee.
 
Mimi ningeomba anijibu kati ya CCM na CDM ni yupi anayecheza ngoma ya mwenzake?
 
Lakini kuna watu si watafiti kazi yao ni kushabikia tu kama mazuzu, kwani ile kamati ya mashirika ya uma ni ya chadema au ni ya Bunge? CAG ni wa chadema au wa Serikali. Tambua hayo kwanza kuliko kuandika upuuzi wako wa kichadema hapa. @ duble.
Hoja ya msingi ni kwa nini waongozwe kwa shinikizo it doen't matter ni shinikizo la nani elewa kuwa hiki ni chama tawala tena kikubwa lakini mambo wanayo yafanya hayaendani na wao walivyo

Jaribu kutafakari japo kidogo tu je hili wazo la kupangua baraza la mawaziri lililolewa lini , kwa nini , na wao walikuwa wapi kuchukua hatua mapema hadi hadi wanashinikizwa

Chama kimekosa sifa kinaendeshwa external force
 
Kwa nini tunajitahidi kuwaamsha ccm waliolala? je tunataka waendlee kuitafuna na kuididimiza nchi hii?

Nionanyo mimi ccm hawana majibu (practically viable solutions) kwa maswali hayo. So tusishangae Nape alivyojibu
 
kamnukuu mtu,halafu haya ndiyo majibu ya nape:

  • Nape Nnauye NAJIULIZA HAYA NDO MASWALI ANAJIULIZA KIJANA WA KITANZANIA??????!!! HUO MVUTO UNAOSEMWA UMEPOTEA KWA TAKWIMU AU KWA KUAMINISHWA GENERALI TU?43 minutes ago · 1
  • Nape Nnauye HAYA MABILIONI YALIYOTUMIWA ARUMERU NI YAPI NI TSHS NGAPI HASA MPAKA YAITWE MABILIONI?42 minutes ago
  • Nape Nnauye HIVI NI UJANJA MTU KUHAMA CHAMA NA CHAMA KINGINE KIKAMPOKEA AU CHAMA MAKINI KITAJIKITA KUTAFUTA WANACHAMA WAPYA KUTOKA KUNDI KUBWA LA WATANZANIA WASIO KUWA NA VYAMA??? UNAJIKITA KUCHUKUA SCREPERS?!!!!!!41 minutes ago
  • Nape Nnauye VIJANA WANAOHAMA ARUSHA NI KINA NANI NA HISTORIA YAO NDANI YA CHAMA ZAIDI YA KUTUKANA VIONGOZI WA CCM NI NINI?40 minutes ago
  • Sleim Salum CCM ni chama kikubwa40 minutes ago
  • Nape Nnauye TAKWIMU ZINAONYESHA KINONDONI PEKEAKE TENA KWENYE MATAWI TU ACHILIA MBALI KATA NA WILAYA TUNAO MAPROFESA, WANAJESHI WASTAAFU, MA DOCTARI, GRADUATES NK WAMEGOMBEA , ANAYEDANGANYA ETI WATU HAWATAKI KUJAZA FOMU NANI?38 minutes ago

yaani hata kuandika SCRAPER imemshinda ..... huyu sio kiongozi
 
Hizi ndizo statements zilizotolewa na Saif Al-Islam wakati vita inaanza:!
  1. To fight and die in Tripoli
  2. To fight and die in Tripoli
  3. To fight and die in Tripoli
Mwisho wa siku alikamatiwa Awbari na siyo Tripoli kama alivyokuwa anajigamba mwanzo.

Mytake: Huwa wanazikana Statement zao baadaye!
 
NAPE NAKUONEA HURUMA SANA KWANI UTAKONDA NA MWISHO UTAKUFA KABLA YA WAKATI WAKO KWA KUAMUA KUIJIBIA CCM....MADUDU WAFANYE WENGINE ALAFU WEWE UPEWE KAZI YA KUISEMEA SISIEMU ILIYOKUFA NA WALIOIUA WAPO KIMYA.......HUONI UNAPOTEZA MUDA WAKO NAPE KUENDELEA KUJIFANYA CCM WAKATI PIA ULIKUWA MBIONI KUKIHAMA?......HUONI KUENDELEA HIVYO PIA MACHINI MWA VIJANA NA WATZ UNAONESHA UNAFIKI WAKO?...KWELI NAPE UKO TAYARI "kusema kitu fulani ni cheupe wakati unajua kuwa ni cheusi"?
 
...analipwa kwa kazi hiyo, hawezi kukiuka mkataba wake kwa sasa.
 
Back
Top Bottom