Nape Nnauye, kujiuzulu ni uungwana

Nape Nnauye, kujiuzulu ni uungwana

Kinachotusumbua watanganyika wengi ni kufanya siasa kuendeshea maisha! Mtu hana njia nyingine! Hawana misimamo, wanadhalilishwa hovyo! Hawawezi kujiuzulu!
Naamini wanaweza ( ashakum si matusi) wakacheka cheka tu!

Mkuu umenena kweli tupu Nape yupo makini sana kujenga hoja za kutetea maslahi ya nchi hii. Nilimsikia vizuri alipo kuwa anaeleza habari ya tulipo kuwa tulipo na lengo kujivua gamba na muonekano wa CCM mpya. Pia nilimuelewa vizuri alipo kuwa anazungumzia tatizo la muuza duka kuuza bidhaa kwa bei ya juu tofauti na aliyo pangiwa na mwenye duka " hotuba hii aliitoa Mbeya "

Tatizo analokumbana nalo ni kufanya kazi na wazee watupu wa ngazi ya juu ya chama Wazee hawa hawabadiliki kabisa na hawashauriki

NAPE hama uliko unapoteza chama chako ndiyo kina kufa ndiyo maaana wazee wako hawashauriki

Muoneeni huruma Nape jamani, atoke CCM ataishi vipi? Maisha yake yote kalelewa CCM kuanzia chipukizi, umoja wa vijana, karani Nkrumah pale na mpaka sasa Katibu Mwenezi... Hajawahi kuajiriwa nje ya CCM!! Ni ngumu kwake kuishi nje ya CCM... Hana ujanja bali ni kuendelea kumtumikia kafiri ili maisha yake na familia yake yaendeleee...

Cha kumuomba tu ni kwamba aache kutukana wenye "akili" ambao wapo nje ya CCM na akubali kwamba yeye na Tambwe Hiza hakuna tofauti!!!

Arafat, this is more than punching Nape from both left and right hadi kwenye map**b*, ila Mzee Makamba alimwambia kafungiwa duniani hadi mbinguni! I miss his jokes...

Not real aiming to punch him anymore, just analysing the situation and his capability as if he stands at his own stance, the scenario which I seen like is impossible to him nevertheless he might admire to so!

Sure, he could have learnt from Makamba's wisdoms in joke and took right measures from the right time, that could
have assisted him, but he didn't and it seems he has no ability to understand and analyses the situation ahead him.

It's only a stupid can advocacy against the vehicle's exhaust pipe by-product and emissions rate and and later if given opportunity, agrees to drive the same vehicle with the notion that he can drive and reduce the emissions and exhaust by-product since the former drivers where reckless drivers and the main cause of the problem.

uzuri au ubaya wa ccm wakikuona tu unapenda kuchonga kama nape wanakuita wanakupa cheo kisha wanakupa fursa ya kishika hela uzizoe. Kama nape na mkama sio muda mrefu hamtawasikia tena.

Chief Mkwawa, Siko la kufa halina dawa. Nilimwambia Nape hapa hapa JF mapema wakati akichaguliwa ya kwamba ni kawaida ya JK kuwachagua wale wanaopiga kelele na kuwapa lishe, mamlaka yasiyoweza kutoa maamuzi isipokuwa kuwakwaza zaidi na hata kuharibu majina yao. Wapo vijana wengi CCM ambao walikuwa mwiba wa Mafisadi na wameenguliwa ktk uchaguzi wa UVCCM, kisha wamefungiwa ktk zizi la mbuzi walikilishwa majini kwa majira ili hali wengine wakila kwa marefu ya kamba zao. Hii sisi wenye hekima huita - HIFADHI ya MBUZI.

Mbuzi alofugwa zizini akilia sana huwa ni dalili ya njaa, wanachokupa ni lisho la majani na maji kukidhi njaa yako ukiwa bado bandani. Na ukisha shiba unajiona beberu ndani ya zizi usione uzio ule upo kwa ajili yako usitoke bandani na wala usije kuliwa na mbwa mwitu. Umehifadhiwa tu mdogo wangu.

T

Mnamdanganya Nape. Ni chama gani nchi hii ambacho viongozi wote wanakubaliana na kulewana mambo yote? Ahamie CHADEMA ambako Zitto amezikataa posho ambazo wenzake akina Mnyika, Regia na Mbowe wanazisaini? Ahamie CUF ambayo tayari ina ubia na CCM? Siasa za nchi hii zioneni hivohivo. Mimi namshangaa zaidi Rostam kuliko Nape.

Hivi ule mkutano wao wa NEC waliokuwa wanasema utafanyika mwezi tisa umeishia wapi?

Nape mbishi yaani alihakikisha ya kwamba anafika Igunga pamoja na kupigwa marufuku! Ati alienda kutoa pole!! Kisha akaandika kwenye mtandao ati nimefika Igunga!!

Hivi kama msemaji wa CHAMA hayupo igunga ni nani anayetoa matamko na KUENEZA sera na propaganda za Chama? Kwa kifupi ni kwamba Nape amepelekwa likizo fupi na madaraka yake amepewa Mwigulu. Duh hapa napo kuna mambo.

Nape mbishi yaani alihakikisha ya kwamba anafika Igunga pamoja na kupigwa marufuku! Ati alienda kutoa pole!! Kisha akaandika kwenye mtandao ati nimefika Igunga!!

Hivi kama msemaji wa CHAMA hayupo igunga ni nani anayetoa matamko na KUENEZA sera na propaganda za Chama? Kwa kifupi ni kwamba Nape amepelekwa likizo fupi na madaraka yake amepewa Mwigulu. Duh hapa napo kuna mambo.
hapo kwenye bold ndipo nilipo conclude kwamba nape ana akili za kitoto especially alipowatambia watu kama ameshafika Igunga ilihali haonekani hata kwenye kampeni. anyway, ukiwa mwana CCM hata kama ukiwa ni kijana au mzee mwenye mvi mpaka masaburini , woote ni kama watoto wadogo tu!

Kule Igunga bwana hatari sana, Wamempeleka Mzee Mkapa ameacha kampeni anajisafisha na Kuuza NBC...sasa hapo Saed Kubenea anahuliza alisubiri nini mpaka ayasemehe Igunga? Na kama haitoshi Nape anasemekana alifika pale akataka kupigwa na vijana wa CCM na zaidi akaulizwa na Mkama je alifuata nini huko wakati amekatazwa? Soma Mwanahaisi ya Sept 12-20 mtajua zaidi!.. NAPE umeishapata nafasi ya kuongea sema na wewe tukusikie!!

hapo kwenye bold ndipo nilipo conclude kwamba nape ana akili za kitoto especially alipowatambia watu kama ameshafika Igunga ilihali haonekani hata kwenye kampeni. anyway, ukiwa mwana CCM hata kama ukiwa ni kijana au mzee mwenye mvi mpaka masaburini , woote ni kama watoto wadogo tu!

Mkuu mimi nadhani kwa dhati kabisa ya kwamba Nape si kwamba tu ana utoto ila pia haitakii mema CCM na anaonyesha kwamba hayuko nao!! Mtu kama umekatazwa usiende mahala unakurupuka unaenda na unaanza kutamba kwamba nimeenda sasa watanifanya nini!! Japo kuwa kwenda kwenyewe siyo kwenye kampeni ila kupita tu!!

Wakuu hapa kuna kitu: Sita yupo serikalini lakini anaipinga serikali; Nape yupo Chamani lakini anapingana na viongozi wake: Mimi si mtabiri ila naona kama CCJ bado ipo vile!!

Kwakweli maelezo yako ni sahihi sana kazi kwako Nape fanya maamuzi magumu usitumiwe kama kondom.

"Leo wanamhitaji Rostam kuliko wewe kesho watamhitaji Chenge Mwanza kuliko wewe kesho watamhitaji E lowasa Arusha kuliko wewe kesho kutwa watamhitaji Manji kuliko wewe, wewe utangojea kutumwa tu pale wasipotaka kuharibu urafiki wao. Hapo ndipo elimu na uelewa binafsi unapohitajika unapigania nini??

Fikiria mara mbili ujumbe huo then amua

Kule Igunga bwana hatari sana, Wamempeleka Mzee Mkapa ameacha kampeni anajisafisha na Kuuza NBC...sasa hapo Saed Kubenea anahuliza alisubiri nini mpaka ayasemehe Igunga? Na kama haitoshi Nape anasemekana alifika pale akataka kupigwa na vijana wa CCM na zaidi akaulizwa na Mkama je alifuata nini huko wakati amekatazwa? Soma Mwanahaisi ya Sept 12-20 mtajua zaidi!.. NAPE umeishapata nafasi ya kuongea sema na wewe tukusikie!!

Mkuu hakika nakuambia CCM kumbe haiko salama hata kidogo! Minyukano imekuwa minyukano. Sijui wapi penye usalama.

Nina ndoto: Naota kwamba Lowasa atateuliwa kuwa mgombea wa Urais CCM mwaka 2015 na CCM itamegeka mapande mawili ili kutimiza yaliyonenwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Burito

DUUUUUUUU, ujumbe umefika kabisa ila Nepi nafsi yake inamsuta , kikubwa kwake kwa sasa itakuwa ni tumbo tuuu !! Kweli nyumba ya udongo haipigwi deki !!!

Mkuu wa magamba na maswahiba zake wanajua yote kuhusu mwenendo mzima wa CCJ pamoja na waasisi wake walioko ndani ya CCM.Kinachofanyika sasa ni kujaribu kuisambaratisha kwa kupanga mkakati maalum.NAPE,na MKAMA walipewa nyadhifa hizo kwa makusudi Pengine kama njia ya kuweza kuwanusuru kina LOWASA na CHENGE japokuwa LOSTAM alikubali kucheza sarakasi mapema.Mkuu wa kaya na maswahiba zake walijua kabisa kuwa NAPE anaweza kutumika kama vuvuzela tu lakini kelele zake hazitobadili matokeo.Menye maamuzi ya mwisho

Naomba nianze kwa kunukuu maneno ya NAPE mwenyewe aliyoyatoa mwaka 2010 katikati ya wafuasi wa CDM wakati wanamshauri ahamie CDM "...aah jaman kuhama CCM ni kazi sana."

Katika muktadha huo ni vigumu sana kwa sasa kuondoka hasa ikizingatiwa, amekwishapozwa na Ukuu wa Wilaya na N/K- Uenezi.

Hoja atakayoitumia ni kuwa kulikimbia tatizo si kulitatua, ambayo ina mashiko, but kama kijana mwenzake ni bora kumkumbusha kuwa uwezo wa Uyoga ni kubeba kofia yake tu.

Ushauri uliotolewa ni wa msingi sana hasa kwa kijana mwenye caliber yake, ni vyema akauchukua na kupima uzito wake kisha afanye kile ambacho viongozi thabiti na makini wangefanya.

Karibuni kahawa wanakwetu

Sikujua NAKIRI SIKUJUA KAMA NAWAKOSESHA USINGizi kiasi hichi....

Back
Top Bottom