Nape Nnauye, kujiuzulu ni uungwana

Nape Nnauye, kujiuzulu ni uungwana

Yani wewe ni hewa full haha haha haha haha hhaaNyerere hakuwa ***** kusema ccm sio baba yake wala mama yake ila nape uko kimaslahi jamani huna uwezo wa kiakili wala kimawazo wa kuchambua ushauri wa chief?? hata ushauri wa busara unautungia mipasho duhh wallah huitaji hata certificate ya std 7 kutambua kuwa wewe ni mzigo mwingine wa chama wallah angekuwa makamba angejibu hoja japo kwa jazba sasa wewe unajibu mipasho eti katibu mwenezi tehe tehe tehe subiri yakufike zaidi ukose hata pa kukimbilia unatia aibu badala ya kushukuru kwa ushauri unaopewa na watu wanaokupenda wewe unaleta mipasho, si wewe ulisema siku 90 haya ziko wapi? pokea changamoto wacha mipasho dogo nepi



Sikujua NAKIRI SIKUJUA KAMA NAWAKOSESHA USINGizi kiasi hichi....
 
mhhhhhhhhhhh,ndugu yangu uliyoyanena yote huenda yanaukweli ndani yake kwani hata nasi tulikuwa tukiyasoma ktk vyombo vya habari,lakini yasemekana Nape alikuwepo Igunga kwa kile kifo kilichotokea baada ya kijana mmoja kugongwa na gari

sasa hatujui kama alikwenda kwa nauri yake ama alikwenda kichama

yetu ni macho

ila namkubali sana Nape kwa misimamo yake,kinachoniuzi ni kufanya Siasa za kukomoana hicho ndicho sikipendi toka kwake

Alienda kichama kwani nilimshuhudia akiwa ndani ya Landcruiser LC Series nyeupe yenye namba T***BKW mali ya CCM.
 
atatumiwa na kumwagwa huko kama dodoki,akitaka ajivue gamba maana kashindwa kuwavua wenzake
 
Sikujua NAKIRI SIKUJUA KAMA NAWAKOSESHA USINGizi kiasi hichi....

Huna aibu kabisa wewe mjomba...wewe kama kiongozi hupaswi kukurupuka kwa majibu kama haya..pia kwani hufahamu serikali iliyo chini ya chama chako ndio chanzo cha kutukosesha usingizi waTZ kwa kukosa umeme wa uhakika, maji ya uhakika, elimu ya uhakika, afya ya uhakika, usafiri wa uhakika, ulinzi wa mali na maliasili zetu kwa uhakika n.k.
Hivyo hupaswi kabisa kusema ulivyosema...hakika unajidhihirisha ulivyo mweupe.

Shame on you!
 
Sikujua NAKIRI SIKUJUA KAMA NAWAKOSESHA USINGizi kiasi hichi....
Huna haja ya kujibu kwa kutumia maneno ya kwenye kanga, naamini cha muhumu hapa ni kujibu hoja ndo jambo la msingi hapa.
 
Sikujua NAKIRI SIKUJUA KAMA NAWAKOSESHA USINGizi kiasi hichi....

Kutoka Mwanahalisi, Septemba 14 - Alfred Lucas

NDANI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa hali si shwari tena. Wanaojiita waasisi wa “mpango wa chama wa kujivua gamba” wameanza kutuhumiana kukivuruga chama, imefahamika.

Taarifa zinasema mlengwa mkuu wa kinachoitwa, “kukivuruga chama” ni Nape Nnauye, katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi.
Nape anadaiwa kukivuruga chama kutokana na hatua yake ya kwenda Inguga, wiki mbili zilizopita. Inadaiwa hatua ya Nape kwenda Igunga imewaudhi baadhi ya wakubwa zake, akiwamo Rais Jakaya Kikwete na katibu mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, ambaye anadai kuwa uamuzi wa Nape waweza kudhoofisha nguvu ya CCM.
Hatua ya Mukama inatokana na uamuzi wa CCM kumpigia magoti Rostam Aziz, mmoja wa watuhumiwa watatu wa ufisadi wanaotakiwa kujiondoa ndani ya chama hicho. Wengine wanaotakiwa kuondoka ni Edward Lowassa na Andrew Chenge.

Tayari Rostam amejiuzulu nafasi zake zote kwenye chama hicho, ukiwamo ubunge wa Igunga na ujumbe wa NEC.
Mukama na Kikwete ndio waliasisi mpango wa chama wa kujivua gamba, Aprili mwaka huu, kwa madai kuwa watuhumiwa hao watatu wa ufisadi wanakishushia hadhi chama hicho mbele ya jamii.
Habari kutoka ndani ya CCM mjini Dar es Salaam na makao makuu mjini Dodoma zinasema, Mukama alimtuhumu Nape kwa hatua yake ya kwenda Igunga gafla, akisema imelenga kukidhoofisha chama hicho.
Nape alikwenda Igunga tarehe 4 Septemba 2011, kwa kile alichodai kutoa pole kwa familia ya wazazi wa mtoto Peter Ezekiel, aliyefariki dunia papohapo baada ya kugongwa na gari la mizigo, wakati mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu akichukua fomu.
Taarifa zinamnukuu Mukama akimueleza Nape, “…nimeambiwa umekwenda Igunga, wakati Kamati Kuu ya chama imekuzuia kwenda huko. Unataka nini? Mbona unataka kutuharibia uchaguzi,” alifoka Mukama.
Vyanzo vya taarifa kutoka CCM vinasema, Mukama aliamua kuchukua hatua hiyo ili kumfurahisha Rostam ambaye sasa anaonekana lulu ndani ya chama hicho.
Wachambuzi wa mambo wa ya kisiasa wanasema, hatua ya CCM kumdhoofisha Nape kwa kukumbatia watuhumiwa wa ufisadi, inazidi kukimaliza chama hicho kikongwe nchini.

Kwa mujibu wa waliokaribu na Nape, safari ya kiongozi huyo mjini Igunga ililenga kuwatambia baadhi ya wapinzani wake wa kisiasa waliodai Rais Kikwete amempiga marufuku kukanyaga huko wakati huu wa kampeni.
Kuthibitisha madai hayo, Nape aliandika katika mtandao wa JamiiForum, mara baada ya tukio hilo la Igunga, “Mlisema chama kimempiga marufuku Nape kukanyaga Igunga, nikasema tusubiri. Leo, mmeona nilivyotinga Igunga…”

Kwa mujibu wa mashuhuda, mara baada ya Nape kutoka nyumbani kwa wazazi wa Peter Ezekiel, alikwenda moja kwa moja kwenye baa maarufu iitwayo The Peak, ambapo inadaiwa alinisurika kichapo kutoka kwa mmoja wa mabaunsa wa CCM.

Inadaiwa kijana huyo wa miraba minne aliyefahamika kwa jina moja la Shaban, ambaye inadaiwa ni kutoka kwa kundi la Rostam Aziz, mara baada ya kumuona Nape kwenye baa hiyo alifoka, “Wewe unatafuta nini hapa?”
Naye Nape akajibu, “Wewe unafahamu unaongea na nani?” Shaban akajibu, “Ndiyo. Nafahamu kwamba wewe ni Nape Nnauye.”
Kauli hiyo ilianza kumfanya Nape anyong’onyee kidogo, lakini mtoa taarifa anasema alijipa nguvu na kusema, “…Nimekuja kikazi. Tupishe tunamazungumzo yetu.”

Shaban aligoma kuondoka na kisha akasema, “…Ondoka hapa, vinginevyo tutakuonyesha. Umekuja kutuharibia uchaguzi siyo?”

Mara baada ya kauli hiyo, taarifa zinasema Nape aliondoka katika eneo hilo na kuingia kwenye gari lake haraka kuelekea Singida.
Alipoulizwa na waandishi wa habari mjini Igunga kwa nini anadhani amefanyiwa vurugu, Nape alisema, “Hakuna kitu. Nilikuwa napita njia tu.”

Sokomoko hilo lilitinga hadi kwa viongozi wake wakuu wa chama, Mukama na Rais Kikwete.

Inadaiwa mara baada ya kupata taarifa hizo, Mukama kwa hasira alihoji, “Nape kwa nini umekwenda Igunga?”



Alisema, “Umekatazwa na Kamati Kuu usiende Igunga, sasa mbona umekwenda?” Alipojaribu kujitetea kwamba alikwenda huko kuhani, Mukama alisema, “Nani amekutuma? Nani amekuruhusu? Kijana, tafadhali usituharibie uchaguzi,” Mukama anaripotiwa kufoka.

Gazeti hili lilipomtafuta Nape kuthibitisha madai hayo, alijibu kwa sauti ya unyonge, “Alfred, mimi sina la kusema juu ya hilo.” Akauliza, “Jamani, mimi kijana mwenzenu. Nimewakosea nini? Niambieni basi.”

Kwa upande wake, Mukama alipoulizwa alianza kwa kucheka, “Aaah aaah aaah…umeyapata wapi hayo?” Akasema, “Sikiliza Alfred, hilo suala la Nape achana nalo. Si suala la magazeti…”
“…Fahamu sisi hatufanyi kazi za kiutendaji na magazeti. Isitoshe si vema kuzungumza mambo mazito kama haya kwenye simu. Nakwenda Zanzibar, nitarudi kesho (jana Jumanne). Njoo ofisini keshokutwa (leo Jumatano), tuzungumze.”
Alipoelezwa gazeti liko mbioni kwenda mtamboni, Mukama alisema, “Sawa, lakini kwanini usije ofisini?”
Kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa, tarehe 9 Septemba 2011, Nape akiwa Dodoma anajiaanda kuelekea Igunga kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za chama chake, ghafla aliitwa na Mukama na kuambiwa, “…hutakiwi kukanyaga Igunga.”

Alisema, “Nimeambiwa unajiandaa kwenda Igunga? Mbona wewe kijana husikii,” alisikika Mukama akimueleza Nape. Pamoja na kwamba Nape ndiye katibu mwenezi wa CCM, hakuwapo Igunga wakati wa ufunguzi wa kampeni hizo na hatarajiwi kutia mguu.

Mbali na Nape, CCM inadaiwa kumzuia Samwel Sitta, Christopher ole Sendeka na Dk. Harrison Mwakyembe ambao walipendekezwa na Nape kuendesha kampeni hizo, kwa kile kilichoitwa, “Kutomuudhi Rostam.”

Baada ya ufunguzi wa kampeni, Mukama akiwa mwenye furaha, aliwaambia baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho waliokuwapo mjini Igunga, “Tumefanikiwa sana katika mkutano wetu huu. Kuna watu wengine bwana, hawana discipline (nidhamu); hawana adabu wanajiona wanaweza kuvuta watu kwenye mkutano.

“Mwiguru (Nchemba) anafanya kazi nzuri sana. Ameratibu mkutano huu vizuri. Kampeni zimekwenda vema. Ni kijana mwenye busara sana yule,” ameeleza mtoa taarifa akimnukuu Mukama.

Masikini Nape, ni kama toto tundu
linalofokewa na Mukama,
linadharauliwa na mafisadi
na limetelekezwa na CCM
lakini lazidi tu kujikomba kwa magamba.
Akukataaye hakwambii toka !

​
 
"Jamani. mimi kijana mwenzenu nimewakosea nini niambieni basi" ha ha ha... NAPE bwana aaaha! CCM vigeugeu.
 
Mhhhh,
BADO HAMPATI USINGIZI TU WAUNGWANA??????? ONCE KIONGOZI WA CHINA ALISEMA UKIONA ADUI YAKO ANAKWAMBIA USIPITE HUKO, HUKO NDO KWA KUPITA COZ NDIO NJIA SAHIHI hahahahahahahahahaaahahahahahahahahhh!!!!!
 
Mhhhh,
BADO HAMPATI USINGIZI TU WAUNGWANA??????? ONCE KIONGOZI WA CHINA ALISEMA UKIONA ADUI YAKO ANAKWAMBIA USIPITE HUKO, HUKO NDO KWA KUPITA COZ NDIO NJIA SAHIHI hahahahahahahahahaaahahahahahahahahhh!!!!!
Unamuiga @NYC kucheka hovyo! Serikali legelege ndo matokeo yake haya! Kipi cha kukuchekesha hapo? Nadhan hata marehemu baba yako angekuonya uachane na siasa za maji taka! Kujiuzulu ni uungwana? Kumbuka wametumia vibaya kodi zetu na ulizunguka nchi ukihubiri watoke, leo unawaalika ktk kampeni, inaleta maana? Nadhan you need to rethink matendo na maneno ya chama they r two contradicting things.
 
Mhhhh,
BADO HAMPATI USINGIZI TU WAUNGWANA??????? ONCE KIONGOZI WA CHINA ALISEMA UKIONA ADUI YAKO ANAKWAMBIA USIPITE HUKO, HUKO NDO KWA KUPITA COZ NDIO NJIA SAHIHI hahahahahahahahahaaahahahahahahahahhh!!!!!

Ok sasa nimekuelewa kumbe huu ndiyo mtazamo wako, watu wanaokushauri au wale wenye msimamo tofauti na wewe unawaita maadui!!!!!!!! No wonder hilo linchi liko namna hiyo 50yrs after independence..................Kama viongozi wenyewe wa chama kinachoendesha serikali mna mitizamo hasi kiasi hiki!!!!
 
Nape ashakuwa m**aya wa siasa, acha wakutumie kotekote, utamu unakaribia kuisha na ndo itakuwa mwisho wako kwny safari ya siasa. We unaambiwa ukweli unaleta tabia za kishosti, sasa unamchekea nani hapa? Bulshiit!
 
Ndo huyo anajitapa kushindana na Zitto ama Dr. Slaa, yahani kama hiyo ndo CCM tunasubiri 40 yao 2015, na patakuwa hapashikiki maana watawaita mpaka kina Mramba, Yona na wengine wawasaidie maana uongozi sasa umepwaya sana wa CCM toka juu mpaka chini.
 
Chifu Mkwawa, ulichosema ni ukweli mtupu. Wala haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa uwazi huo. Kwa mtazamo wangu KINACHOMSUMBUA NAPE NI KUONA AIBU. Anashindwa kujitoa kwa kuwa alitumia nguvu kubwa kuamini na kukipigia debe kitu ambacho baadae nadhani ameshagundua kuwa NI KWELI ANATUMIWA TU kwa maslahi ya wengine. Na anajua akijivua gamba, basi wale mapacha watatu watamshukia kama mwewe. Mwacheni abembee kama bendera hadi itakapochakaa kwa upepo.
 
Mhhhh,
BADO HAMPATI USINGIZI TU WAUNGWANA??????? ONCE KIONGOZI WA CHINA ALISEMA UKIONA ADUI YAKO ANAKWAMBIA USIPITE HUKO, HUKO NDO KWA KUPITA COZ NDIO NJIA SAHIHI hahahahahahahahahaaahahahahahahahahhh!!!!!
you sold your soul for buying your favourates!
how can you liberate your people?
 
Mhhhh,
BADO HAMPATI USINGIZI TU WAUNGWANA??????? ONCE KIONGOZI WA CHINA ALISEMA UKIONA ADUI YAKO ANAKWAMBIA USIPITE HUKO, HUKO NDO KWA KUPITA COZ NDIO NJIA SAHIHI hahahahahahahahahaaahahahahahahahahhh!!!!!
Kha!
Nape, hiyo ndo nukuu ya leo bila hata kumtaja kiongozi anaitwa nani! AU Mao tse Tung
 
Kha!<br />
Nape, hiyo ndo nukuu ya leo bila hata kumtaja kiongozi anaitwa nani! AU Mao tse Tung

huyu ni kilaza then anajidai eti zitto kamkimbia singida. Hv ww Nape unadhani IQ yako unaweza ku compare na ya zitto? Subiri sasa uisnme namba vizuri.
 
Mhhhh,
BADO HAMPATI USINGIZI TU WAUNGWANA??????? ONCE KIONGOZI WA CHINA ALISEMA UKIONA ADUI YAKO ANAKWAMBIA USIPITE HUKO, HUKO NDO KWA KUPITA COZ NDIO NJIA SAHIHI hahahahahahahahahaaahahahahahahahahhh!!!!!
\
Jibu hoja iliyopo mezani, acha kucheka hovyo kama Rambuza.
 
Nape naona wale malaika watatu wanakuzidi nguvu. Mmoja kajisafisha makanisani na misikini anapiga hodi ikulu. Mmelala na nyoka sasa kawa chatu mtamweza kumtoa ndani mlango mdogo. Aliingia kama kimjusi mlango ulitosha ;Chatu ndani labda mvunje ukuta ndio atoke. La sivyo nyumba inakwenda chini ama mumkubali humo ndani.
 
Back
Top Bottom