Nape Nnauye hatanii, tazama juu ya korosho

Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya filauni.
Mbunge wa mtama Nape Mnauye amefunguka kweli juu ya serikali na zao la korosho,ebu pitieni hapo chini muone!View attachment 1026736

In God we Trust
Najua wapo wataoingiza siasa chafu juu ya kauli yako lkn mh nape umekuwa mkweli kabisa juu korosho yawezekana mh rais alidanganywa kwa makusudi au vinginevyo lkn yote kwa yote maneno yake na watumishi wake akiwemo waziri wa kilimo hayakuakisi uhalisia na leo inadhihirisha ukimya uliopo juu ya sakata la korosho na kuhakiki miti ya korosho hakuna majibu ya uhakiki wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini binadamu tunatakiwa kujifunza kama kuna matatu mazuri yamefanyika nyuma likaharibika moja tu tutoe suluhisho sio kuona akifai tena.

Lengo lao lilikuwa zuri na kama wasingechukua hii hatua Serikali kununua korosho hadi leo wangekuwa wanafanya majadiliano na wanunuzi na ingepata lawama kubwa isipokuwa tatizo awakujipanga fresh ila kwa misimu ijayo itakuwa poa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uliloliaandika ni uhalisia kabisa, tatizo imani imepungua na inaelekea kufa hasa pale wananchi wanapoona serikali ina udhalimu kwao... Mfano yule aliekuwa anasema alipima korosho october zikiwa grade I ila baadae anakuja kuambiwa korosho zake ni grade III.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simsemi vibaya kwa sababu ya yeye kumkomalia Dr. Slaa hapana.

Kwangu Nape ni mnafiki kama wanafiki wengine, akiwa Waziri alihusika kuhujumu Bunge live sijasahau fitna zake, alifanya juu chini mpaka bunge live likasitishwa.

Mungu analipa hapa hapa wale aliohusika nao kuhujumu bunge live wamemgeuka hana uwaziri tena ndio maana kawa mkosoaji, enzi akiwa Waziri anatembea na king'ora alikua upande wao kwa sasa kinachomsumbua kuwashambulia wenzake ni kukosa Uwaziri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza ukawa sahihi na unachokisema ni mafunzo makuu kwake na kwa wengine lakini, tangu ametoka katika uwaziri huo amekuwa "consistent" kwa kiwango cha kuaminika. Si mlinganishi na Mhe.Mwigulu Nchemba, Simbachawene na hata Anna Kilango Melecela. Hata huo ujasiri wa kukiri sioni kama ni kitu kidogo cha kubeza. Nadhani amekua na kujifunza mengi. Suala la kujiuliza ni Je, kile anachokipinga sasa ni cha kweli au anauonea utawala uliopo madarakani. Katika lugha ya kiswahili kuna neno "kuberi". Tusemapo amekuwa kuberi tunaimanisha amekuwa mzuri wa tabia ukilinganisha na huko nyuma.
Nashauri tumepe nafasi Mhe. Nape
 
Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya filauni.
Mbunge wa mtama Nape Mnauye amefunguka kweli juu ya serikali na zao la korosho,ebu pitieni hapo chini muone!View attachment 1026736

In God we Trust

Sisi kwetu Mwanza tunalima pamba na tunaweza kukadiria kiasi cha pamba itakayopatikana kulingana na ukubwa wa shamba. Zaidi ni kuwa miche ya pamba huwa inakatwa baada ya mavuno halafu msimu unaofuata, tunalima kwa kupanda mbegu upya, tofauti na mikorosho ambayo yenyewe inakuwa ni ile ile miaka na miaka. Itakuwa kitu cha kushangaza kwamba mikorosho ambayo idadi ya miche yake ipo fixed na imekuwa ikizalisha korosho miaka na miaka, wakulima wake washindwe kuweza kukadiria kiasi cha korosho wanayoweza kuzalisha halafu yule wa pamba aweze, wakati yeye huwa anapanda upya mwaka hadi mwaka. Tatizo la Nape ni kwamba ana kitu kingine rohoni ambacho ame-bank nacho ila kwa uhakika hakina uhusiano wa moja kwa moja na haya anayoendelea kung'ang'ana nayo siku hadi siku. Ni uhuru mawzao lakini, yuko sahihi!
 
Back
Top Bottom