Nape Nnauye: CCM ni chama bora, siwezi kuhama!

Nape Nnauye: CCM ni chama bora, siwezi kuhama!

Wewe ndo umenena! Hawezi kukata tawi ambalo kwa sasa bado analikalia!
Aisema anaenda kuwatumikia watu wa mtama kama mbunge wa ccm! Hata kama ana mpango wa kukihama chama laklni haiweizi kuwa sasa hata kama ungekuwa wewe!
habari itakuwa nyingine kabisa baada ya bunge kuvunjwa 2020 kuelekea uchaguzi mkuu! Nape si mjinga! Haiwezekani akizire chakula alichokipika mwenyewe halafu awaachie kina Bashite wajichane!
Upo sahihi mkuu
 
Alipomchafua Mzee Lowassa, alidhani yeye atabakia Malaika wa chama? Dalili ya mvua ni mawingu iko siku atajikuta walipo wengine waliotoka anapopang'ang'ania sasa.
 
Sindano imekuingia

JE WAKATI ULE APOTAKA KUHAMA YEYE NA KUNDI LAKE KUANZISHA CCJ, KWANI HIKI KILIKUWA CHAMA BOMU HADI AKATAMANI KUHAMA?????

AU WAKATI ULE WALIMUAHIDI KUGOMBEA URAIS KULE CCJ????

NA JUZI MBONA POVU LILIMTOKA PALE HOTELINI ALIPOZUILIWA KUFANYA MKUTANO????

MNAFIKI MKUBWA HUYU!!!!!
 
Siwapendi ccm to death, ila siwezagi kuchangia hoja kwa kufuatamkumbo sasa hivi kuna watu wanaumbuka.
Mtu juzitu alikuwa analialia watu wakaanza kumpa support wakati alionekana kuteleza kabisa kwa kushindwa kumsoma bosiwake.

Ukweli utatuweka huru.
 
nakumbuka hata mrema aliwahi toa kauli yake kule mtwara akisema kuwa anayehama ccm ni mwendawazimu sasa yeye sijui hakuwa mwendawazimu?
 
Hapo anasubiri 2020 ndo aseme maamzi yake maana saizi anaogopa kupoteza ugali
Ninavyomjua Nape ni ccm kindakindaki hawez fanya upuuzi wa kuhama. Kwanza aende wapi kwa sababu hakuna chama zaidi ya ccm kwa sasa. Vingine ni usanii mtupu. Huo ndio ukweli. Na hawez anzisha chama kipya kwa sababu hakitakuwa worth thamani yake ndani ya ccm
 
Mkuu umenichekesha sana......Afu ndio kwanza Wanacdaema WAMEANZA KUBADILISHA GIA nagani wanataka kumsimamisha LISSU 2020...wanajisahau ya kuwa KUNA MTU ANA HATI YA KUWA MGOMBEA wa urais WA MILELE....ni suala la muda tu...tutegemee kuona CHADEMA VIPANDE VIPANDE...

Hahahhahahahahah Sawa na MAFISI kusubiria mkono wa binadamu ukatike.Utaishia huko huko mliozoea kuua watu mpaka mnatuonyesha tabia ya kuua mnayo mpaka ndani.

Mwabieni Bashite aonyeshe vyeti
 
Ninavyomjua Nape ni ccm kindakindaki hawez fanya upuuzi wa kuhama. Kwanza aende wapi kwa sababu hakuna chama zaidi ya ccm kwa sasa. Vingine ni usanii mtupu. Huo ndio ukweli. Na hawez anzisha chama kipya kwa sababu hakitakuwa worth thamani yake ndani ya ccm
Wakati ukifika majibu yataonekana peupe kuwa yuko upande gani
 
Sasa kwa akili zenu mlitegemea awatangazie kuwa anahama?

Halafu ubunge wake?

Msiwe km mandondocha
 
Mwanasiasa huwa hatosheki na madaraka na pesa pia.
Huyu anajikomba CCM kwakuwa uchaguzi hauko karibu, anaogopa kutimuliwa kwenye chama akaukosa ubunge. Wabunge wengi jeuri waliipnyesha kuanzia Agosti 2015 -Octoba 2015 walipoona walipo ugali umemwagika.
Siasa ni jamaa wa shetani ingawa si wanasiasa wote wanamtukuza shetani.
 
Back
Top Bottom