Nape Nnauye: CCM ni chama bora, siwezi kuhama!

Nape Nnauye: CCM ni chama bora, siwezi kuhama!

Unafki mwingine bhana wakati siku ile alikuwa analia kama toto
 
ha


Akizungumza na Waziri Mwakyembe na watendaji wengine mjini Dodoma wakati akikabidhi Ofisi kwa Waziri mpya, Nape amesema, "Kwanza sina kinyongo na Rais na ningeomba watu wasinilishe maneno wala kufanya assumption zao. I am stronger than they think, nimelelewa humu ndani na ninazijua ups and downs."

"CCM ni chama Bora sana sana siwezi kutoka. Kwa sasa wanaowaza kuwa labda nitatoka wanapoteza muda. I fought for this party and hata kama yapo mambo ya kurekebisha siwezi kurekebisha nikiwa nje nitarekebisha nikiwa ndani. Kwahiyo I wish walielewe hilo ili tusipotezeane muda", alisema Nape.

"Pia nichukue nafasi hii kumshukuru Rais kwa muda niliofanya nae kazi kwa miezi 15."

"Dkt. Wizara nzuri sana hii, inagusa watu wote bila kujali profession zao. Changamoto kubwa ni sheria zilizopitwa na wakati. Tulijikita kuzibadilisha ziendane na wakati. Tulianza na Habari na tulikuwa tunaelekea kwenye michezo, sanaa n.k. Nadhani wewe Mwanasheria ukiliweza hili uatakuwa umesaidia wizara na nchi pia ili hata mtu mwingine akija baadaye akute misingi ya kisheria ya kufanya mambo"
a4b9396db4a360314bd106e51a22ee5d.jpg

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akabidhiwa ofisi na Waziri aliyepita Nape Nnauye mjini Dodoma leo.

hana pa kwenda, tabasamu analolazimisha ni kama lile la kinyago cha mpingo, kinatabasamu lakini uki kibonyeza ni kigumu.
 
Nape sasa akili imeshamrudia,anajutia kuita waandishi haraka kabla ya kutafakari siku aliotumbuliwa
 
Nape!wewe ni mwanasiasa bora umekuzwa na mzee Moses katika mazingira ya siasa na utumishi wa umma.Vyote viwili vinapaswa kukupa a certain degree of tolerance.Nakushauri usiwe mpumbavu kwa kitumiwa tumiwa na wajanja fulani. Naamini kabisa una malengo katika maisha yako,ili yatimie kupanda na kushuka ni lazima maana ndiyo kuishi kwenyewe huko.
So I believe your strong as you said but not stubborn.
Ubarikiwe.
 
Hata Lowasa alisema hawezi kuhama CCM lakini now yupo Chadema, wanasiasa siyo watu wa kuamini sana.
Sabodo alihamia chadema akakuta wapigadili akarudi ccm sasa nape kaona Kule atakutana na wauza unga,wanywa viroba,bangi kwa uwingi,sultan mbowe,wanaotaka babu Seya aachiwe akaona bora abaki ccm
 
Kwa pumba za vyama pinzani..... huwezi nufaika ukivifata hata km ccm wakiwa vichaa.... tiba haiwez patikana toka chama pinzani... kwa sera zao mbovu. . Majungu na hulka walionao...
 
sasa alikuwa analalama nini aliposhikiwa bastola?
Huyo aliyemtishia si alitumwa na watu wa chama chake!
Hata kama hana mpango wa kuhama ni dhahiri kuna mambo hayafurahii. Kusema hivo kwa sasa ni obvious ili kuepusha kuonyesha chuki au hasira.
kwa sasa ccm si taasisi bali ni mtu. Mustakabali wake si wa kitaasisi bali matakwa ya mtu na yeye hana nafasi yoyote kwa sasa kuijenga tena! Aiyemfukuza anajua hilo
 
ujanja wa kuhama ccm hana kwani kwenye vyama vingine hakuna ulaji na ukikaa vibaya mkienda mahali ww ndio unanunulia chakula wanachama wenzako. Hivyo nguvu yake ipo ndani ya ccm hata kama itamshika makalio.

Wewe msokile umesema kweli, huyo Nape ana overestimate mchango wake humo ccm kana kwamba bila yeye hayo yaliyofanyika yasingewezekana!! Atambue tu tena haraka sana kuwa yeye nje ya ccm si lolote si chochote!! Namshangaa hata anaposema "nitarekebisha mambo nikiwa ndani ya chama" yeye kujifanya ni chimbuko la fikra za mabadiliko huko kwenye chama ni kujipa chakula kisaikolojia tu!!
 
Makamanda mko wapi.. Yericko juzi juz alisema Wabunge 20 wa CCM wanahamia Chadema, sijui tayari
 
Sabodo alihamia chadema akakuta wapigadili akarudi ccm sasa nape kaona Kule atakutana na wauza unga,wanywa viroba,bangi kwa uwingi,sultan mbowe,wanaotaka babu Seya aachiwe akaona bora abaki ccm
Sultani Mbowe!!! Hahahaaa
 
Sabodo alihamia chadema akakuta wapigadili akarudi ccm sasa nape kaona Kule atakutana na wauza unga,wanywa viroba,bangi kwa uwingi,sultan mbowe,wanaotaka babu Seya aachiwe akaona bora abaki ccm
Mkuu ni bora ukajitabulisha kuwa unatokea mkoa gani kabla ya kukuhukumu.
 
Back
Top Bottom