Nape Nnauye: CCM ni chama bora, siwezi kuhama!

Nape Nnauye: CCM ni chama bora, siwezi kuhama!

Caroline Hans

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2017
Posts
723
Reaction score
386


Akizungumza na Waziri Mwakyembe na watendaji wengine mjini Dodoma wakati akikabidhi Ofisi kwa Waziri mpya, Nape amesema, "Kwanza sina kinyongo na Rais na ningeomba watu wasinilishe maneno wala kufanya assumption zao. I am stronger than they think, nimelelewa humu ndani na ninazijua ups and downs."

"CCM ni chama Bora sana sana siwezi kutoka. Kwa sasa wanaowaza kuwa labda nitatoka wanapoteza muda. I fought for this party and hata kama yapo mambo ya kurekebisha siwezi kurekebisha nikiwa nje nitarekebisha nikiwa ndani. Kwahiyo I wish walielewe hilo ili tusipotezeane muda", alisema Nape.

"Pia nichukue nafasi hii kumshukuru Rais kwa muda niliofanya nae kazi kwa miezi 15."

"Dkt. Wizara nzuri sana hii, inagusa watu wote bila kujali profession zao. Changamoto kubwa ni sheria zilizopitwa na wakati. Tulijikita kuzibadilisha ziendane na wakati. Tulianza na Habari na tulikuwa tunaelekea kwenye michezo, sanaa n.k. Nadhani wewe Mwanasheria ukiliweza hili uatakuwa umesaidia wizara na nchi pia ili hata mtu mwingine akija baadaye akute misingi ya kisheria ya kufanya mambo"
a4b9396db4a360314bd106e51a22ee5d.jpg

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akabidhiwa ofisi na Waziri aliyepita Nape Nnauye mjini Dodoma leo.
 
ujanja wa kuhama ccm hana kwani kwenye vyama vingine hakuna ulaji na ukikaa vibaya mkienda mahali ww ndio unanunulia chakula wanachama wenzako. Hivyo nguvu yake ipo ndani ya ccm hata kama itamshika makalio.

Hilo ni kweli kabisa.

Na mimi bado naamini atapewa tu majukumu mengine na rais.
 
Chadema bhana walikazana kumuita hero hero wakadhani atarowa sifa na kuhamia kwa wapiga salute ....mavi ya kunguru, bado naamini kuwa huyu jamaa sio wa kispotispoti ata kama ametofautiana na boss wake ila ni mtu wa misimamo isiyo yumba sio kama yule mzee white hair.
 
Back
Top Bottom