Nape Nnauye ajiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Utalii

Kama ni kweli anatakiwa afukuzwe kabisa kwenye chama
Ardhi ni mali ya Jamhuri ya muungano,sheria ipo wazi ukimilikishwa unatakiwa kuendeleza ndani ya muda fulani
Watu wamepewa malaki ya ekari,ili walime na kutoa ajira,matokeo yake wamekopa benki za nje huku wameacha mapori na wananchi hawaruhusiwi kulima

Mkuu haya yote si yange semwa wakati wa kujadiliwa Bungeni kwa hiyo Ripoti ?.Kama mliwa nyang'anya kisheria Hofu ni ya nini mpaka mnyofoe Taarifa Muhimu ?

Mna Hofu na nini hasa kama mlitenda Haki ?
 
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukata kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.

--------------

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii. Kujiuzulu kwake, kunatokana kile kinachoitwa, “Kugoma kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji, kinyume na sheria.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya Kamati yake.

“Nape alitaka ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, iliombe Bunge kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge ili kuchunguza utaratibu uliotumika wa kufuta mashamba ya watu,” ameeleza mjumbe mmoja wa kamati hiyo.

Ameongeza, “Serikali haitaki kuundwa kwa Kamati hiyo. Hivyo imeamua kuitumia Kamati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumlazimisha Nape kujiuzulu.”

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, tayari Nape amemuandikia barua rasmi ya Spika kumjulisha kujiuzulu kwake.

Nape alihuhutubia waandishi wa habari leo akiwa chini ya vyombo vya usalama na kutetea msimamo wake.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku moja kabla ya Kamati yake kuwasilisha ripoti yake na zinaeleza kuwa Kamati hiyo ilikuwa inaleta mapendekezo ya kuundwa kwa Kamati Teule, jambo ambalo lilihofiwa kuwaumbua baadhi ya wakubwa.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo.

Mbunge huyo wa Mtama mkoani Lindi, alivuliwa wadhifa wake siku moja baada ya kupokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi juu ya tukio uvamizi wa kituo cha televisheni cha Clouds kwa kutumia silaha uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Ripoti ya kamati aliyoiunda Nape kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho majira ya saa 5 usiku wa Ijumaa ya tarehe 17 Machi 2017 na alifanya uvamizi huo akitumia askari wenye silaha. Nape aliahidi kulifikisha ripoti yake kwa mamlaka ya juu yake. Haijajulikana mpaka sasa, ripoti hiyo amekabidhiwa nani.

Nape ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Uenezi ya CCM, amesema atapata nafasi nzuri ya kutumikia wananchi wa jimboni wake baada ya kuachia nafasi hii.
Nape anaikosi na amb yanayohusu Ripoti.

As long as ni wao kwa wao hata wakikatama mapaga sisi haituhusu.

Nape anavuna alichopanda
 
Nape hata ajidai Mwema namna gani, simsamehi kosa la kukataa Bunge kwenda live kwa sababu za kijinga sana!

Watanzania ni watu wa ajabu sana, rahis sana kuhadaiwa na wanasiasa uchwara, eti leo kweli Mwanahabari Huru anamuona Nape mtu mwema??!
We unadhani ulikuwa uamuzi wa nape ule? Mbona sasa halioneshwi live baada ya nape kutoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukata kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.

--------------

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii. Kujiuzulu kwake, kunatokana kile kinachoitwa, “Kugoma kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji, kinyume na sheria.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya Kamati yake.

“Nape alitaka ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, iliombe Bunge kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge ili kuchunguza utaratibu uliotumika wa kufuta mashamba ya watu,” ameeleza mjumbe mmoja wa kamati hiyo.

Ameongeza, “Serikali haitaki kuundwa kwa Kamati hiyo. Hivyo imeamua kuitumia Kamati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumlazimisha Nape kujiuzulu.”

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, tayari Nape amemuandikia barua rasmi ya Spika kumjulisha kujiuzulu kwake.

Nape alihuhutubia waandishi wa habari leo akiwa chini ya vyombo vya usalama na kutetea msimamo wake.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku moja kabla ya Kamati yake kuwasilisha ripoti yake na zinaeleza kuwa Kamati hiyo ilikuwa inaleta mapendekezo ya kuundwa kwa Kamati Teule, jambo ambalo lilihofiwa kuwaumbua baadhi ya wakubwa.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo.

Mbunge huyo wa Mtama mkoani Lindi, alivuliwa wadhifa wake siku moja baada ya kupokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi juu ya tukio uvamizi wa kituo cha televisheni cha Clouds kwa kutumia silaha uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Ripoti ya kamati aliyoiunda Nape kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho majira ya saa 5 usiku wa Ijumaa ya tarehe 17 Machi 2017 na alifanya uvamizi huo akitumia askari wenye silaha. Nape aliahidi kulifikisha ripoti yake kwa mamlaka ya juu yake. Haijajulikana mpaka sasa, ripoti hiyo amekabidhiwa nani.

Nape ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Uenezi ya CCM, amesema atapata nafasi nzuri ya kutumikia wananchi wa jimboni wake baada ya kuachia nafasi hii.
mshahara wa goli la mkono..... inaitwa karma.

na bado.... wote walioshiriki ile dhambi October 2015 watapata taabu sana kwani Mungu hataniwi.

up next...... January Ma-rope!
 
Back
Top Bottom