Nape Nnauye ajiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Utalii

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukataa kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.

--------------

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii. Kujiuzulu kwake, kunatokana kile kinachodaiwa ni “Kugoma kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji, kinyume na sheria.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya Kamati yake.

“Nape alitaka ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, iliombe Bunge kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge ili kuchunguza utaratibu uliotumika wa kufuta mashamba ya watu,” ameeleza mjumbe mmoja wa kamati hiyo.

Ameongeza, “Serikali haitaki kuundwa kwa Kamati hiyo. Hivyo imeamua kuitumia Kamati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumlazimisha Nape kujiuzulu.”

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, tayari Nape amemuandikia barua rasmi ya Spika kumjulisha kujiuzulu kwake.

Nape alihuhutubia waandishi wa habari leo akiwa chini ya vyombo vya usalama na kutetea msimamo wake.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku moja kabla ya Kamati yake kuwasilisha ripoti yake na zinaeleza kuwa Kamati hiyo ilikuwa inaleta mapendekezo ya kuundwa kwa Kamati Teule, jambo ambalo lilihofiwa kuwaumbua baadhi ya wakubwa.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo.

Mbunge huyo wa Mtama mkoani Lindi, alivuliwa wadhifa wake siku moja baada ya kupokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi juu ya tukio uvamizi wa kituo cha televisheni cha Clouds kwa kutumia silaha uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Ripoti ya kamati aliyoiunda Nape kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho majira ya saa 5 usiku wa Ijumaa ya tarehe 17 Machi 2017 na alifanya uvamizi huo akitumia askari wenye silaha. Nape aliahidi kulifikisha ripoti yake kwa mamlaka ya juu yake. Haijajulikana mpaka sasa, ripoti hiyo amekabidhiwa nani.

Nape ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Uenezi ya CCM, amesema atapata nafasi nzuri ya kutumikia wananchi wa jimboni wake baada ya kuachia nafasi hii.
 
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukata kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.
Mungu ibariki Tanzania

In God we Trust
 
Back
Top Bottom